Baadhi ya wanachama na wananchi katika Manispaa ya Lindi wakishangilia wakati Mke wa Rais na Mjumbe wa NEC Taifa ya CCM anayewakilisha Manispaa hiyo Mama Salma Kikwete na viongozi wengine wakiingia uwanjani hapo.
Mke wa Rais na Mjumbe wa NEC Taifa ya CCM anayewakilisha Lindi Manispaa Mama Salma Kikwete akipokea kadi kutoka kwa aliyekuwa mwanachama wa CUF na Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mitandi Ndugu Laibu Kaisi aliyeamua kurejea Chama Cha Mapinduzi wakati wa sherehe za uzinduzi rami za kampeni za Chama hicho katika Manispaa hiyo.
Mke wa Rais na Mjumbe wa NEC Taifa ya Chama cha Mapinduzi Mama Salma Kikwete akihutubia mamia ya wananchi wa Lindi Manispaa wakati wa uzinduzi rasmi wa kampeni za Uchaguzi Mkuu wa Rais, wabunge na Madiwani utakaofanyika tarehe 25.10.2015
Mjumbe wa NEC Taifa ya CCM na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akimtambilisha rasmi Mgombea Ubunge kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi katika Manispaa ya Lindi Ndugu Hassan Suleiman Kaunje kwa wanachama wa CCM na wananchi wakati akizindua rasmi kampeni hizo kwenye uwanja wa Fisi huko Lindi tarehe 3.9.2015.
Mke wa Rais MamaSalma Kikwete akimkabidhi Ndugu Hassan Kaunje ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi wakati wa uzinduzi rasmi wa kampeni hizo tarehe 3.9.2015.
Baadhi ya
vijana wakimshangilia kwa vifijo Ndugu Hassan Kaunje, Mgombea Ubunge kwa tiketi
ya Chama Cha Mapinduzi mara baada ya kumalizika kwa sherehe za uzinduzi rasmi
wa kampeni hizo katika Wilaya ya Lindi Mjini tarehe 3.9.2015.
Na Magreth Kinabo –Maelezo,Lindi
MKE wa Rais
Mama Salma Kikwete amewataka wananchi wa Jimbo la Lindi Mjini kuhakikisha kwamba wanapiga kura ya ndiyo kwa
mgombea wa kiti cha urais,Dkt. John Magufuli , mgombea kiti cha Ubunge Hassan
Kaunje na wagombea viti cha udiwani ili waweze
kupata maendeleo.
Kauli hiyo
imetolewa jana jioni na Mama Kikwete ,ambaye pia ni
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi(NEC) wa Wilaya Lindi ,wakati
wa uzinduzi wa kampeni ya chama hicho ya
wilaya hiyo ili iliyoambatana na
uzinduzi wa Ilani ya CCM kwa lengo la kuinadi na kuwanadi wagombea hao iliyofanyika kwenye
uwanja wa Fisi.
“Leo
nimekuja kufanya kazi hii moja ya
kuhakikisha mgombea wa kiti cha urais,
anashinda akiwemo mgombea wa kiti
cha ubunge na wagombea wa viti vya udiwani,” alisema Mama Kikwete huku akiinadi
picha ya mgombea wa kiti cha urais na
kumnadi mgombea wa kiti cha Ubunge na
wagombea viti vya udiwani katika kata
mbalimbali kupitia chama hicho.
Mama Kikwete
aliongeza kwamba ikiwa kila mtu
atatoka na kufanya kampeni ya nguvu jimbo hilo litapata kura ya ndiyo viti
hivyo.
Alisema wananchi hao endapo watafanya hivyo ifikapo Oktoba 25, mwaka huu,
watakuwa wamefanya kazi iliyokamilika na watapata maendeleo kwani amani
inapatikana mahali ambapo kuna maendeleo.
Pia aliwataka wananchi hao kuhakikisha watunza kadi zao za kupigia kura, wasije
wakapoteza nafasi hiyo muhimu.
Mama Kikwete
aliwataka wananchi hao, kukipa chama hicho kura ya ndiyo kwa sababu kina ilani,
ni chama makini na kinafanya kazi kwa mipango.
Akizungumzia
kuhusu ilani ya chama hicho,Mama Kikwete alisema,ina mambo makubwa manne,
ambayo ni kuondoa umasikini, kupunguza tatizo la ukosefu wa ajira, kuendeleza
vita ya kupambana na rushwa na ubadhirifu wa mali ya umma.
Katika
uzinduzi huo, Mama Kikwete alimkabidhi
vitendea kazi mgombea wa kiti cha Ubunge
,ambavyo ni Katiba ya CCM na
ilani hiyo ili aweze kufanya kazi huku akishangiliwa na mamia ya watu
walijitokeza uwanjani hapo wengi wao wakiwa ni vijana.
Kaisi
na waliokuwa wagombea wenzake wa kiti
cha Ubunge 10 wameungana ili kumwuunga mkono Kaunje, hatua ambayo ilipongenzwa
na Mama Kikwete.
“ Kura
zipotosha huwezi kuhama kwenda chama kingine, bali mnaungana na kuwa kitu
kimoja ni maneno mazuri ya kuiga mfano,” alisisitiza Mama Kikwete.
Kwa upande
wake Mwenyekiti wa CCM, mkoa wa Lindi, Mzee Ally Mtopa aliwakemea watu
wanaosema kuwa chama hicho hakijafanya maendeleo, ambapo alisema mtu anayesema hivyo, sawa na kumdharau baba yake
aliyempeleka shule.
No comments:
Post a Comment