DAKTARI DHAMANA KANDA YA UNGUJA DOKTA FADHIL RAMADHAN AKITOA MAELEKEZO KWA
MADAKTARI BINGWA KABLA YA KUANZA ZOEZI
LA MATIBABU KATIKA KIJIJI CHA KITOPE.
DAKTARI FEI JIE AKIMPIMA MTOTO SARA SHAABAN
MARADHI YA MENO NA KOO MKAAZI WA KITOPE WILAYA YA KASKAZIN B”.
WAKAAZI MBALI MBALI WA MJI WA KITOPE
WAKIPATIWA MATIBABU.
MTOTO HALILA HAMZA NAE AKIPATA HUDUMA ZA KUPIMWA
UZITO.
DOKTA MKUU XU ZHUOQUN AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA
HABARI JUU YA WANAVYO ENDELEA NA ZOEZI LA KUWAPATIA HUDUMA ZA MATIBABU WANANCHI
WA ZANZIBAR.
PICHA NA ABDALLA OMAR - MAELEZO ZANZIBAR.
DAKTARI DHAMANA KANDA YA UNGUJA DOKTA FADHIL RAMADHAN AKITOA MAELEKEZO KWA
MADAKTARI BINGWA KABLA YA KUANZA ZOEZI
LA MATIBABU KATIKA KIJIJI CHA KITOPE.
DAKTARI FEI JIE AKIMPIMA MTOTO SARA SHAABAN
MARADHI YA MENO NA KOO MKAAZI WA KITOPE WILAYA YA KASKAZIN B”.
WAKAAZI MBALI MBALI WA MJI WA KITOPE
WAKIPATIWA MATIBABU.
MTOTO HALILA HAMZA NAE AKIPATA HUDUMA ZA KUPIMWA
UZITO.
DOKTA MKUU XU ZHUOQUN AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA
HABARI JUU YA WANAVYO ENDELEA NA ZOEZI LA KUWAPATIA HUDUMA ZA MATIBABU WANANCHI
WA ZANZIBAR.
PICHA NA ABDALLA OMAR - MAELEZO ZANZIBAR.
Mwashungi
Tahir- Maelezo Zanzibar 14/09/2015
Jumla ya
madaktari bingwa tisa kutoka nchini China Medical team wako Zanzibar kwa ajili
ya kutoa huduma kila sehemu mbalimbali
hapa vijijini kwa ajili ya kuwarahisishia wananchi kupata huduma ili waweze kuelewa kujua afya
zao.
Hayo
yamesemwa na daktari Dhamana wa kanda ya
Unguja DR Fadhil Mohammed Abdullah huko katika shehia ya Kaskazini B Kitope
wakati wa zoezi hilo huko kijijini hapo.
Amesema
lengo la madaktari hao kutoa huduma hiyo vijijini ni kuweza kuwarahisishia
wananchi wa vijijini kuweza kupima na kujua afya zao ambapo zoezi hili hufanyika
kila baada ya miezi mitatu na hutolewa bure.
Pia
amesema
madaktari hao wapo nchini wakishirikiana na madaktari wa wizara ya Afya
kwa kutoa huduma hizo huko kijijini na wanachi kuweza kujitambua afya
zao.
Dr Fadhil
amewaomba wananchi wa vijijini huduma hii inapowafikia wasiidharau kwani ni
vizuri kila binaadamu kujua afya yake ili aweze kujitambua na kupata matibabu .
“Lengo hasa
ni kuwa kila mtu aweze kujielewa afya yake kwani endapo utapojua afya yako
baada ya kufanya vipimo itakuwa rahisi kupata matibabu ambayo tayari ushaletewa
hapohapo karibu bila kuifuata sehemu za mbali “. Alisema Daktari huyo.
Kwa upande
wa madaktari hao kiongozi wa madaktari hao Xu Zhuqun amesema amefurahishwa sana
kwa kuona kila kijiji wanachokwenda wananchi wanajitokeza kwa wingi hii ni
ishara tosha wananchi kutaka kuelewa afya zao.
Madaktari
hao ni maspeshalisti wa maradhi mbali mbali yakiwemo sukari, pua , kinywa na
meno. Presha ,matatizo ya mkojo na huduma za watoto na akina mama masikio na
maradhi mengineyo.
Na kwa
upande wa wananchi hao Asha Abdullah
na Haji Duwani Mjombo ambapo wote ni wakaazi wa Kitope wamesema wamefurahishwa sana kwa kuletewa
huduma hizi vijijini ambapo zinapatikana bure .
Pia wameishukuru
serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kuwajali wananchi wake kwa kuwapelekea
huduma hii vijijini ambapo wananchi wengi wanakuwa wana maradhi mbalimbali
lakini hawana pesa za vipimo wala
hawawezi kufika huko hospitali ya Mnazi mmoja.
Sambamba na hayo
sheha wa Shehia ya Kitope Mbaleni Haji
Shaali Makame amefurahishwa kuona wananchi wamejitokeza kwa wingi kwa kujipatia
huduma hii ambapo kila binaadamu anayo haki ya kujua afya yake.
Akitoa wito
sheha huyo amesema likitokea jambo hili ni vizuri tujitokeze kwa wingi kwa
sababu hii ni bahati pekee tulioletewa na serikali na kuweza kuwatoa hofu
wananchi wajitokeze wasiwe na woga.
Hili ni
zoezi maalum ambalo limepangwa na serikali kwa kuwaleta madaktari hao nchini na
kuwafatia wananchi vijijini kwa kuwafanyia
vipimo na kujua afya zao na pia huduma za dawa zinatolewa hapo hapo na kama
matatizo makubwa wanakuomba kufika katika hospitali ya mnazi Mmoja kwa ajili ya matibabu zaidi.
Hivi
karibuni zoezi hilo lilifanywa Katika kijiji cha Kisauni.
No comments:
Post a Comment