Mhe. Mohamed Chande Othman, Jaji Mkuu wa
Tanzania akifungua rasmi kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa Mahakama ya
Tanzania mapema leo katika Ukumbi wa Mikutano wa St. Gaspar uliopo mjini
Dodoma, katika hotuba yake ya ufunguzi Mhe. Jaji Mkuu amewaasa Watumishi wa
Mahakama kutimiza wajibu wao wa utoaji haki nchini kwa uadilifu.
Kundi la baadhi ya Wahe. Majaji na wajumbe
wengine wa Baraza la Wafanyakazi wakiwa katika Mkutano Mkuu wa Baraza la
Wafanyakazi linalofanyika katika Hoteli ya St. Gasper mjini Dar es Salaam.
Mhe. Hussein A. Kattanga, Mtendaji Mkuu,
Mahakama ya Tanzania akitoa taarifa ya Maendeleo ya Mahakama katika ufunguzi wa
kikao cha Baraza la Wafanyakazi kinachofanyika mkoani Dodoma.
Wajumbe wa Baraza wakiwa katika kikao hicho,
lengo la kikao cha Baraza la Wafanyakazi ni kuwawezesha Watumishi kuainisha
matatizo yanayowakabili na kutafuta njia za kutatua na kuboresha huduma za
Mahakama.
Mhe. Mohamed Chande Othman, Jaji Mkuu wa
Tanzania (katikati), Mhe. Shaban Ali Lila, Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya
Tanzania (wa pili kulia), Mhe. Clarensia Makuru, Jaji Mfawidhi, Mahakama Kuu
Kanda ya Dodoma, Mhe. Haruna Songoro, Kaimu Jaji Mfawidhi, Mahakama Kuu
Divisheni ya Biashara (wa kwanza kushoto), Bi. Rose Tengu, Katibu Mteule wa
Baraza la Wafanyakazi-Mahakama ya Tanzania (wa tatu kushoto) na Wajumbe wengine
wa Baraza wakiwa katika picha ya pamoja na Wahe. Wajumbe ya Kikao cha Baraza
(waliosimama) wanaowakilisha mikoa mbalimbali. (Picha na Mahakama)
No comments:
Post a Comment