Monday, September 7, 2015

KATIBU MKUU WA WIZARA YA UCHUKUZI, DKT. SHAABAN MWINJAKA AZUNGUMZA NA UONGOZI WA MAMLAKA YA VIWANJA VYA NDEGE TANZANIA (TAA)

 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Mhandisi Suleiman Suleiman, akimtabulisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dkt. Shaaban Mwinjaka (wa pili kutoka kulia), kabla ya kuongea na watumishi wa Serikali kutoka taasisi Mbalimbali za Serikali wanaofanya kazi kwenye Kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), mwishoni mwa wiki. Katibu Mkuu alikutana na Watumishi hao ili kujadili namna bora ya kufanya kazi katika Viwanja vya Ndege na kuwkumbusha wajibu wao wanapokuwa kiwanjani hapo.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dkt. Shaaban Mwinjaka, akiongea na watumishi kutoka Ofisi mbalimbali za Serikali wanaofanya kazi Kwenye Kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA),, mwishoni mwa wiki.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dkt. Shaaban Mwinjaka (wa nne kutoka kulia mstari wa kwanza), akiwa katika picha ya pamoja na Uongozi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania(TAA) na watuumishi wa Serikali wanaotoka kwenye ofisi mbalimbali za Serikali wanaofanya kazi katika Kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), mwishoni mwa wiki. Katibu Mkuu alikutana na Watumishi hao ili kujadili namna bora ya kufanya kazi katika Viwanja vya Ndege.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dkt. Shaaban Mwinjaka akiangalia Daraja jipya la kupandia ndege “Aero Bridge” lililokamilika hivi karibuni wakati alipotembelea Kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), na kukutana na Uongozi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) pamoja na watumishi wanaotoka kwenye ofisi mbalimbali za Serikali wanaofanya kazi kiwanjani cha Uwanja huo, mwishoni mwa wiki. Katika mkutano huo Katibu Mkuu aliwakumbusha watumishi hao kukumbuka majukumu yao na kutambua kuwa wanafanya kazi katika sehemu nyeti inayoonyesha picha ya Tanzania).
(Habari Picha na Kitengocha Mawasiliano Serikali-Uchukuzi)

No comments: