Friday, September 25, 2015

GHARIKA LA MAGUFULI NDANI YA MJI WA KAHAMA LEO


Wananchi wa Nyarugusu wakifuatilia hotuba ya mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli.
Wakifuatilia mkutano wa kampeni wa Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli,uliofanyika wilayani Mbongwe jioni ya leo
Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi wa Wilaya ya Bukombe mapema leo mchana,alipokuwa akielekea mkoani Shinyanga kuendelea na kampeni zake za kuomba ridhaa kwa wananchi ya kuiongoza Tanzania katika kipindi cha awamu ya tano.
Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli akimnadi mgombea Ubunge wa jimbo la Bukombe Ndugu Dotto Biteko,kwa wananchi wa wilaya hiyo ya Bukombe waliojitokeza kwa wingi kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika jioni ya leo mkoani Geita.
Baadhi ya wananchi wakifuatilia hotuba ya Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli





Wanafuatilia mkutano wa kampeni wa Dkt Magufuli.
Baadhi ya Wachimbaji wadogo wadogo wakiwa wamemsimamisha Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli katika kijiji cha Masumbwe,ili wamueleze kero zao kuhusiana na suala zima la uchimbaji madini kwa wachimbaji wadogo wadogo.
 Dkt Magufuli akiwasili kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni mjini Kahama jioni ya leo.
 Kiongozi wa msafara wa Kampeni za Mgombea Urais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania,kupitia chama cha CCM,Ndugu Abdallah Bulembo akimkaribisha Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli kuwahutubia wananchi wa Kahama jioni ya leo kwenye uwanja wa CCM mkoani Shinyanga.
 Nyomi la watu likifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye mkutano huo wa kampeni.
 Mjumbe wa kamati ya ushindi ya kampeni za Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli,Mh.Samweli Sitta akiwahutubia wananchi wa mji wa Kahama jioni ya leo kwenye mkutano wa kampeni za Urais,uliofanyika kwenye viwanja vya CCM mjini humo na kuhudhuriwa na umati mkubwa wa watu,Mh.Sitta a.k.a Mzee wa viwango na kasi pia alimnadi Dkt Magufuli na kumwombea kura kwa wananchi hao za ushindi na hatimaye akaibuke mshindi kwa nafasi ya Rais na kupata ridhaa ya kuwaongoza Watanzania katika kipindi cha awamu ya tano.
 Nyomi la wakazi wa mji wa Kahama jioni ya leo kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni
 Wananchi wa Kahama mjiji wakishangilia
 Maelfu ya wananchi wa mji wa Kahama wakiwa wamekusanyika mkutano wa hadhara wa kampeni,uliofanyika katika viwanja vya CCM mjini Kahama jioni ya leo.
Maelfu ya Wakazi wa Mji wa Kahama na Vitongoji vyake wakimsikiliza  Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa chama cha Mapinduzi CCM Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akimwaga sera zake na kujinadi kwa kuwaomba wampigie kura ya ndio asubuhi na mapema Oktoba 25 mwaka huu kwenye uchaguzi mkuu,ili aibuke mshindi na kupata ridhaa ya kuwaongoza Watanzania katika awamu ya tano.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa chama cha Mapinduzi CCM Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia maelfu ya Waananchi waliojitokeza kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni,uliofanyika katika viwanja vya CCM mjini Kahama jioni ya leo.

Dkt.Magufuli leo amefanya mikutano yake ya kampeni  katika wilaya za Mbogwe, Bukombe mkoani Geita  na baadae halmashauri mpya ya Ushetu baadaye mkutano mkubwa wa kampeni  uliofanyika mjini Kahama mkoani Shinyanga na kuhudhuriwa na umati wa watu uliorushwa moja kwa moja na kituo cha Televisheni cha Star TV .

Akizungumza katika mkutano huo wakati akiwaomba wananchi kujitokeza kwa wingi Oktoba 25 mwaka huu kumpigia kura za ndiyo,Dkt Magufuli amesema kuwa Serikali yake itashughulikia migogoro ya madereva na kuhakikisha wanapata mikataba kutoka kwa waajiri wao ili kuboresha maslahi yao.

Amesema Madereva ni watu muhimu katika sekta ya usafirishaji na wanafanya kazi ngumu,lakini maslahi yao hayatiliwi maanani,hivyo amesema kuwa atahakikisha yanaboreshwa ili na waone faida ya kazi yao,na iwe yenye kuthaminika ,hivyo serikali ya awamu ya tano itakayoongozwa na Dk. John Pombe Magufuli italifanyia kazi ipaswavyo.
Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi wa Wilaya ya Bukombe mapema leo mchana,alipokuwa akielekea mkoani Shinyanga kuendelea na kampeni zake za kuomba ridhaa kwa wananchi ya kuiongoza Tanzania katika kipindi cha awamu ya tano.
Mgombea Urais wa CCM Dkt Jonh Pombe Magufuli akiwanadi Mgombea Ubunge wa Kahama Ndugu Jumanne Kishimba pamoja na Mgombea Ubunge wa jimbo la Msalala Ndugu Ezekiel Maige mbele ya maelfu ya wakazi wa mji huo kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni.
Wachimbaji wadogo wadogo waishieo eneo la Nyarugusu,Wilayani Geita wakimshangilia mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli mapema leo jioni alipokuwa akielekea mkoani Shinyanga kuendelea na kampeni zake

No comments: