Katika hali isiyotarajiwa na wengi katika Jimbo la Moshi Mjini, Mgombea Ubunge kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi Davis Mosha ameanza utekelezaji wa ahadi zake katika Jimbo hilo, wiki chache baada ya kuzungumza na wanamuziki na wasanii kuhusu kazi zao na wasanii hao kuomba kupata kituo cha Redio cha kisasa na Studio ya kisasa ambavyo vitaweza kufanya kazi zao kwa ubora zaidi na pia kufika mbali.
Katika kutekeleza hilo Mh. Davis Mosha amekwishaanza ujenzi wa Studio ya Kisasa ya Kituo cha Redio chini ya Kampuni yake ya Africa Swahili Media na ujenzi huo unatarajiwa kukamilika mapema na vifaa vya Studio huyo vinatarajiwa kuwasili muda wowote kutoka Dar es Salaam baada ya kuwasili Bandarini vikitokea Nchini Italy. Mh. Davis Mosha aliwaahidi wasanii hao kufungua kituo cha Redio kitakachoweza kusikika Tanzania Nzima na Duniani kote kwa njia ya Satelite. Pia aliwahakikishia kufungua na kituo cha televisheni. Kituo hicho cha Redio na Studio ya kisasa kianatarajiwa kufunguliwa katika jingo la Kilimanjaro Commercial Complex Maarufu kama jingo jipya la NSSF lililopo Moshi Mjini.
|
Mh. Davis Elisa Mosha |
|
Hati ya Kontena la Vifaa vya Studio lililotoka Italy Baada ya kuingia Bandari ya jiji la Dar es Salaam. |
Mbali na utekelezaji huo wa Kero ya Wasanii, Mh. Davis Elisa Mosha wiki iliyopita aliweza kufanya Ziara ya kimya kimya katika Soko la Mitumba la King George Memorial na kutazama Changamoto za Soko hilo lakini pia alipata fursa ya kuzungumza na uongozi wa Soko hilo na wafanyabiashara wa Soko hilo. Kwa pamoja walieleza MAzingira magumu wanayofanyia Biashara huku ikiwa Miundombinu mibovu ikiwemo vyoo na Soko halina Paa inapelelea iwapo mvua itanyesha basi kunakua hakuna biashara kabisa maana Bidhaa hunyeshwa na Mvua na mbali na Mvua pia jua ni lao. Katika kutatua changamoto hizo Davis Mosha aliwaahidi kulifanyia kazi mapema tatizo lao na hatosubiri mpaka muda wa uchaguzi ufike maana adha hiyo wanayoipata ni wananchi wa Moshi wakiwemo mama zake na baba zake waliopo hapo Sokoni.
|
Mh. Davis Mosha alipotembelea Soko la Mitumba la Memorial na kujionea changamoto mbalimbali. |
|
Mh. Davis Mosha akisalimiana na wafanyabiashara wa soko la Memoria alipotembelea soko hilo. |
Kutokana na Ahadi hiyo Jana Mh. Mosha aliwasili Sokoni hapo na Mainjinia kutoka Kampuni ya Group Six ltd ambao ni Raia wa China kwa lengo la kufanya kufanya vipimo na Michoro ya uboreahwaji wa Soko hilo ili kuweza kuondoa changamoto zinazowakabili wafanyabiashara wa Soko hilo. Mainjinia hao walizunguka katika Soko hilo na kutazama eneo la Soko ili kuweka mipango ya kuanza ujenzi wa Soko hilo ambapo ujenzi huo hautoathiri wafanyabashara hao kuendelea kufanya biashara zao.
|
Mainjinia Raia wa China kutoka Kampuni ya Group Six wakiwa soko la Mitumba la Memorial kwa ajili ya kufanya ukaguzi wa Matengenezo ya soko hilo. |
|
Mh. Mwigulu Nchemba akimkaribisha Mh. Davis Mosha azungumze na Wafanyabiashara wa Soko la Memorial |
|
Mh. Davis Mosha akizungumza na wafanyabiashara wa Soko la Mitumba la Memorial |
Kutokana na utekelezaji huo wa ahadi wananchi mbalimbali wameonekana kufurahishwa na aina ya kiongozi waliompata ambaye anaomba Ridhaa ya kuchaguliwa kuongoza Jimbo la Moshi Mjini. Haata hivyo katika mkutano wa Hadhara uliofanyika jana katika Soko hili ulihudhuriwa na Viongozi mbalimbali wakiongozwa na Mh. Mwigulu Nchimbi ambaye alipata fursa ya kumzungumzia Davis Mosha. Mwigulu alisema kazi ngumu kuliko zote ni kutomchagua Davis Mosha kuwa Mbunge wa Moshi mjini na kazi Rais sana ni kumchagua Davis Mosha. Aliwaambia wakazi wa Moshi kuwa wana bahati ya kipekee kupata Mbunge ambaye ameanza utekelezaji wa ahadi zake kabla ya kusubiri bajeti ya serikali na viongozi kama hao ndi o Tanzania inawahitaji, Kwahiyo ikifika 25 mwezi wa Kumi wasifanye kosa wamchague Davis Elisa Mosha awe Mbunge wa Moshi Mjini pamoja na Madiwani wake wa ccm na bila kusahau kumpa kura za Kishindo Mgombea Urais wa ccm Ndugu John Pombe Magufuli.
No comments:
Post a Comment