Baadhi ya wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na wananchi wakiwa
katika mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa kiti cha urais Bi. Samia
Suluhu Jimbo la Ukonga jijini Dar es Salaam jana.
Baadhi ya wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na wananchi wakiwa
katika mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa kiti cha urais Bi. Samia
Suluhu Jimbo la Ukonga jijini Dar es Salaam jana.
Mgombea mwenza wa kiti cha urais, Bi. Samia Suluhu akizungumza na
wanaCCM na wapenzi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) huku akiwaonesha ilani
ya chama hicho na kuainisha mipango mizuri ambayo imewekwa katika
kuimarisha huduma katika sekta mbalimbali.
Baadhi ya wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na wananchi wakiwa
katika mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa kiti cha urais Bi. Samia
Suluhu Jimbo la Ukonga jijini Dar es Salaam jana.
Meya wa Ilala Jerry Slaa ambaye pia ni mgombea ubunge CCM Jimbo la
Ukonga akizungumza katika mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa kiti
cha urais Bi. Samia Suluhu (hayupo pichani) eneo la Kipawa jijini Dar es
Salaam.
Baadhi ya wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na wananchi wakiwa
katika mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa kiti cha urais Bi. Samia
Suluhu Jimbo la Ukonga jijini Dar es Salaam jana.
MGOMBEA
mwenza wa nafasi ya urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bi. Samia
Suluhu amesema Serikali watakayoiunda endapo watapewa ridhaa ya kuongoza
nchi watahakikisha wanadhibiti wizi wa dawa kwenye hospitali za
Serikali ambazo zimekuwa zikiuziwa wananchi katika maduka ya dawa
mitaani. Bi. Suluhu katoa kauli hiyo jana alipokuwa akihutubia katika
mikutano ya anuai ya hadhara Jimbo la Ilala kuinadi ilani ya Chama Cha
Mapinduzi, ambapo amebainisha kuwa dawa zote zitakuwa zinaingizwa katika
mtandao maalum na kuzifuatilia na endapo zitatumika nje ya utaratibu
itabainika na hatua kuchukuliwa.
Alisema
mtandao huo utafanikiwa kukabiliana na kero ya ukosefu wa dawa katika
hospitali za serikali kwani dawa hizo zimekuwa zikiibwa kwenye hospitali
za Serikali na kuuzwa nje katika maduka ya dawa binafsi na hospitali
binafsi. "...Tunaamini mfumo huu utatusaidia kukabiliana na wizi wa dawa
na rushwa hospitalini...unakuta daktari anakuandikia dawa alafu
anakuelekeza duka la kwenda kununua sasa unajiuliza huyu mtu kajuaje
kama sio yeye kapeleka pale," alisema Bi. Suluhu.
Pamoja
na hayo mgombea huyo mwenza, aliwashauri wananchi kuukubali utaratibu
wa kutumia mfumo wa bima ya afya kwa matibabu ambao umekuwa ukimlazimu
mwananchi kuchangia kiasi kidogo cha fedha na kutibiwa mwaka mzima bure
katika hospitali zote zinazotumia utaratibu huo, kwani alidai
utawasaidia wengi. "...Unajua ugonjwa unampata mtu ghafla na muda wowote
haijalishi una fedha za kujitibu au la, lakini kama unabima ya afya
waweza kutibiwa muda wowote hata kama hauna fedha wakati huo,"
alisisitiza Bi. Suluhu.
Aidha,
Bi. Suluhu alisema serikali watakayoiunda itajitahidi kupima maeneo
mengi ya ardhi na kuyatoa kwa wananchi ili kukabiliana na migogoro ya
ardhi.
Alisema
Serikali yao pia imekamilisha utaratibu wa kuwalipa fidia wananchi wa
Kipunguni ambao wanadai fidia na itawalipa wananchi hao kwa thamani ya
sasa ya ardhi kwani 2004 hadi sasa ni muda mrefu na ardhi imepanda
thamani.
Akizungumzia
kero ya foleni, alisema ili kumaliza kero hiyo na msongamano wa magari
jijini Dar es Salaam, Serikali imepanga kujenga miji mipya maalum na ya
kisasa pembezoni wa jiji hili na kwa kuanzia itajenga mjini huo eneo la
Kibaha ili shughuli nyingine ziwe zikifanyika katika mji huo na Dar es
Salaam kupunguza msongamano, zoezi litakaloenda sambamba na ujenzi wa
barabara ndogondogo za mitaani ambao utapunguza msongamano na foleni
katika barabara kubwa.
Aidha
Bi. Suluhu alisema zitajengwa barabara za juu katika makutano ya
barabara ikiwa pamoja na kuzijenga barabara ndogondogo zikiwemo za Mbezi
Morogoro-Malamba Mawili-Tangi Bovu-Kimara Baruti-Goba na nyinginezo ili
kupunguza msongamano katika barabara kubwa.
*Imeandaliwa na www.thehabari.com
No comments:
Post a Comment