Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa benki ya Maendeleo TIB
Prof. William Lyakurwa (wapili kushoto) na Msajili Hazina Bw. Lawrence Mafuru
(wa pili kulia) wakibadilishana mikataba ya makubaliano ya kiutendaji kwenye
hafla fupi iliyofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.Mkataba huo
unalenga kufungua milango kwa serikali kuweza kusimamia na kukagua ufanisi wa
benki hiyo katika kuleta tija kwa taifa. Wanaoshuhudia ni pamoja na Msajili
Hazina msaidizi Bw. Mwakibinga Mihalale (wa pili kulia) na Mkurugenzi Mtenddaji
wa benki
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa benki ya Maendeleo TIB
Prof. William Lyakurwa (kushoto) na Msajili Hazina Bw. Lawrence Mafuru (kulia)
wakionyesha mikataba ya makubaliano ya kiutendaji baina yao mara baada ya
kuisaini kwenye hafla fupi iliyofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa
wiki.Mkataba huo unalenga kufungua milango kwa serikali kuweza kusimamia na
kukagua ufanisi wa benki hiyo katika kuleta tija kwa taifa.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa benki ya Maendeleo TIB
Prof. William Lyakurwa (kushoto) na Msajili Hazina Bw. Lawrence Mafuru (kulia)
wakibadilishana mikataba ya makubaliano ya kiutendaji kwenye hafla fupi
iliyofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.Mkataba huo unalenga
kufungua milango kwa serikali kuweza kusimamia na kukagua ufanisi wa benki hiyo
katika kuleta tija kwa taifa.
Na
Mwandishi wetu
BENKI ya Maendeleo
TIB imesaini mkataba wa kiuetendaji na Serikali hatua inayofungua milango kwa
serikali kuweza kusimamia na kukagua ufanisi wa benki hiyo katika kuleta tija
kwa taifa.
Kusainiwa
kwa mkataba huo kunaifanya benki hiyo kuwa miongoni mwa mashirika na taasisi za
awali kabisa za umma zilitoa fursa kwa serikali kuzikagua na kupima ufanisi wao
kiutendaji kila mwaka kupitia msajiri wa hazina.
Akizungumza
kwenye hafla fupi ya kusaini mkataba huo iliyofanyika jijini Dar es Salaam
mwishoni mwa juma lilipita, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa benki hiyo
Prof. William Lyakurwa alisema hatua hiyo itaisadia kuongeza msukumo zaidi kwa
benki hiyo kuweza kuweza kutimiza malengo yake na kufanya kazi kwa ufanisi
zaidi.
“Licha ya ukweli kuwa tumekuwa tukitimiza wajibu wetu siku zote
kwa kuhakikisha kwamba tunatoa huduma kwa weledi na ufanisi zaidi lakini
tunaamini kuwa uwepo wa mkataba huu utasaidia kutusukuma zaidi na hatimaye si
tu tufikie malengo yetu bali pia hata kupitiliza malengo tuliyojiwekea,’’
alisema.
Aliongeza kuwa mkataba huo pia utaongeza ari kwa
waafanyakazi wa benki hiyo kwa kuwa utawajengea dhana ya uwepo wa nguvu ya ziada
inayowasukuma zaidi kukamilisha majukumu yao kwa wakati na kwa ufanisi zaidi
sambamba na matumizi sahihi ya fedha zinazotengwa kwa ajili ya uendeshaji wa
benki hiyo.
“Mkataba huu kwetu ni ushahidi kwamba tunatimiza wajibu wetu kwa
uwazi na zaidi tupo tayari kupimwa kwenye hilo.Lengo ni kuwa miongoni mwa
taasisi bora kabisa za fedha hapa nchini na ulimwenguni kwa ujumla,’’ alisema.
Akizungumza kwenye hafla hiyo Msajiri Hazina Bw Lawrence Mafuru
alisema mikataba ya aina hiyo inalenga kuisaidia serikali kupunguza
hasara kubwa ambayo imekuwa ikapata kutoka kwenye mashirika na taasisi za umma
zinazoshindwa kujiendesha kwa ufanisi unaotakiwa.
Alibainisha kuwa mashirika na taasisi za
umma nyingi hapa nchini zinashindwa kujiendesha kwa ufanisi kwa
kuwa kuna ombwe la ufuatiliaji wa utendaji na matumizi ya pesa
zinazotengwa kwa ajili ya uendeshaji wa mashirika hayo.
Akizungumzia mikataba hiyo Bw Mafuru alisema kuwa licha
ya utaratibu huo kuwa mgeni hapa nchini lakini unalenga kutambua
taasisi na mashirika ya umma yanayoshindwa kujiendesha kwa ufanisi sambamba na
matumizi mabaya ya fedha za umma ili kutoa fursa kwa serikali kufanya
maamuzi sahihi kulingana na aina ya changamoto zinazoyakabili mashirika hayo.
“Tunaamini huu ni mwanzo mpya kwenye usimamizi wa mashirika na
taasisi hizi za umma na zote zinatakiwa ziwe na mkataba wa aina hii na tutakuwa
wakali tukibaini udhaifu wowote ikiwemo kuwachukulia hatua kali wale wote
watakaobainika kuhusika na udhaifu huo,’’ alisema.
Pia alitoa wito kwa wanasiasa wakiwepo wabunge kujitoa kwenye bodi
za mashirika mbalimbali ya umma ili kuondoa mgongano wa kimaslahi kwa kuwa wao
wana jukumu la kukagua mashirika hayo kupitia kamati za bunge.
No comments:
Post a Comment