Baadhi ya Wahandisi
wahitimu kutoka katika vyuo na taasisi mbalimbali wakiapa kiapo cha utii kwa
Taaluma yao mbele ya Kamishna wa Viapo wakati wa maadhimisho ya Siku ya
Wahandisi yanayoendelea jijini Dar es salaam.
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi
Ombeni Sefue akizungumza na Wahandisi kutoka maeneo mbalimbali nchini wakati wa
ufunguzi wa Siku ya Wahandisi nchini mwaka 2015 jijini Dar es salaam.
Katibu Mkuu
Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akikabidhi vyeti na miongozo mbalimbali ya
utendaji wa kazi kwa Wahandisi baada ya kuapishwa nchini leo jijini Dar
es salaam.
Katibu Mkuu Kiongozi
Balozi Ombeni Sefue akiwa katika picha ya pamoja na Watendaji wa Bodi ya
Usajili wa Wahandisi nchini Tanzania (ERB) Mara baada ya ufunguzi wa
Siku ya Wahandisi 2015 leo jijini Dar es salaam. Picha na Lorietha
Laurence Maelezo)
Na
Lorietha Laurence
Katibu Mkuu Kiongozi,
Balozi Ombeni Sefue amewataka wahandisi nchini kuwa waadilifu na kuweka bidii na maarifa
katika kazi zao ili kuleta mapinduzi ya uhakika kwa taifa.
Akizungumza katika ufunguzi wa mkutano wa 15
wa Wahandisi wenye kauli mbiu ya “Utekelezaji
wa Dira ya Maendeleo ya mwaka 2025 mtazamo wa Mhandisi” leo (Alhamisi 3.
Septemba, 2015) Jijini Dar es Salaam, Balozi Sefue alisema fani ya uhandisi ni muhimu kwa kuwa inagusa
maisha ya kila ya jamii.
“Mhandisi ni mtu muhimu katika maendeleo ya nchi kwa kuwa sekta nyingi
zinategemea ujuzi wake ikiwemo Nishati
,Madini, barabara, maji, uvuvi na kilimo na nyingine nyingi” alisema Balozi sefue.
Aliongeza kuwa kwa kutambua umuhimu wa wahandisi katika maendeleo ya nchi, Serikali imeweka mikakati mbalimbali
ikiwemo kuweka maabara katika shule za umma ili kuwavutia wanafunzi kupenda
masomo ya sayansi na baadaye kusomea uhandisi pamoja na kuanzishwa vyuo vya umma vya uhandisi.
Kwa mujibu wa Balozi
Sefue alisema Serikali itaendelea kutenga fedha kwa ajili ya mafunzo kwa njia ya vitendo kwa wanafunzi watakaosoma masomo ya
uhandishi katika ngazi mbalimbali.
Aidha Balozi Sefue
aliupongeza Ubalozi wa Norway nchini kwa mchango wake kiasi cha dola milioni 2
za kimarekani zilizosaidia kuwawezesha wahandisi wa kike 217 kusajiliwa na hivyo
kuongeza idadi ya wahindisi wanawake nchini.
“Ninawaomba watoto wa kike wa Tanzania wapende
masomo ya sayansi ili baadaye waweze kusomea uhandisi na hivyo kuongeza idadi
ya wahandisi nchini na kuchochea maendeleo zaidi” alisema Balozi Sefue.
Naye Katibu ya Bodi ya Wahandisi
Nchini, Mhandisi. Prof. Ninatibu Lema ameiomba serikali kujenga mazingira
mazuri kwa wahandisi wa serikali na wa sekta binafsi ili kuleta matunda mazuri
kwa nchini.
Kwa upande wake Msajili
wa Bodi ya Wahandisi, Mhandisi Steven Mlote alisema ili dira ya maedndeleo ya
mwaka 2025 iweze kukamilika ni budi udahili wa wahindisi uongezeke kwa kuwa
uhitaji wake kwa sasa ni mkubwa.
“Mpaka sasa tuna
wahandisi 15364 waliosajiliwa na Bodi ya Usajili nchini idadi ambayo ni ndogo
ukilinganisha na uhitaji wa watu katika kuleta maendeleo kupitia sekta
mbalimbali” alisema mhansisi Mlote.
Katika Mkutano huo
wahandisi 96 waliapa kiapo cha uadilifu mpango uliozinduliwa na Waziri wa
Ujenzi Mhe. Dkt.John Magufuli wakati wa mkutano wa 13 wa wahandisi uliofanyika
September 05 2013.
No comments:
Post a Comment