Na Mwandishi Wetu, Dar
Kwa
miaka mingi upatikanaji wa wataalamu wa Afya na matibabu ya uhakika unakabiliwa
na changamoto kuu mbili inayowakumba wagonjwa wengi Tanzania.Watanzaniawamekuwa
wakisafiri nje ya nchi kupata matibabu ya Figo na magonjwa yanayohusiana na
kibofu. Hivyo wataalamu wawili waliobobea katika magojwa ya Figo na Kibofu
kutoka Hospitali za Apollo walitembelea nchini Tanzania wakishirikiana na madaktari
kutoka Hospital ya Hindu Mandal ili kuwafanyia uchunguzi, kutoa tiba na kutoa
ushauri kwa wagonjwa mbalimbali Tanzania. Dkt V. Rajagopal ambaye ni mtaalamu
wa magonjwa ya njia ya mkojo na mfumo wa uzazi wa kiume na amekuwa mshauri
mwandamizi wa magonjwa ya kibofu katika Hospitali za Apollo huko Hyderabad
India tangu mwaka 1994. Dkt. Sanjay Maaitra ambaye ni mtaalamu wa magonjwa ya
Figo kwa kutoa huduma za matibabu ya figo na magonjwa yanayoambatana na Figo
ikiwa lengo kuu la ujio wao ni kuhakikisha wagonjwa wanapata uchunguzi sahihi
bila kuingia gharama kubwa za kwenda nje ya nchi.
Wagonjwa
wanaosubuliwa na magonjwa yanayohusiana na figo pamoja na mkojo walihudhuria na
kushiriki katika tukio hili. Madaktari
hao waliwafanyia wagonjwa uchunguzi kwa kupitia taarifa zao nyuma na kuzipitia
upya, kutoa historia ya matibabu na kutoa ushauri wa matibabu na tiba kwa
wagonjwa wapya waliojitokeza.
Kama
ilivyoelezwa hapo juu lengo la ujio wa madaktari hawa ni kupata taarifa za
wagonjwa wote ambao walipata huduma za matibabu kutoka kwao iwe ndani ya nchi
au katika Hospital za Apollo huko Hyderabad. Lengo la Dkt. Rajagopal na Sanjay Maitra
ilikuwa ni kuangalia jinsi gani wagonjwa wao wamepata nafuu na kama wanahitaji
vipimo zaidi na marekebisho ya tiba. Kwa mfano mgonjwa ambaye amepandikishwa
figo anahitaji muda mrefu wa ushauri na uchunguzi wa mara kwa mara. Ujio wa madokta hawa hapa nchini umekuwa
jambo jema kwa kuwa umewarahisishia wagonjwa kupata matibabu kwa urahisi na uchunguzi
wa muda mfupi. Endapo kama afya za wagonjwa zilitambulika kuzorota hivyo
madaktari walipendekeza wapate vipimo zaidi katika Hospitali za Apollo,
Hyderabad au Hospitali zozote zile.
Taasisi ya
Upandikizaji ya Apollo (ATI), ni sehemu ya Hospitali za Apollo ambayo niTaasisi
kubwa na imara katika mpango wa upandikizaji figo duniani. Wanatoa huduma za uchunguzi
wa figo, Ini, Upandikizaji figo,
upandikizaji wa ‘Corneal’ ‘GI’,
matibabu ya tumbo na huduma nyinginekwa watoto. Taasisi hii inatoa
ushari mbalimbali, vipimo na tiba.
Wakati
wa ujio wa madaktari, tulipata fursa ya maohijiano na Dkt. V. Rajagopal pamoja
na Dkt. Sanjay Maitra, tuliwauliza kama wameona mabadiliko yoyoteya afya Tanzania
tangu walipokuja safari yao ya mwisho. Pia madaktari hawa walitaja idadi ya
wagonjwa ambao waliofika katika kliniki na kuona idadi kubwa kuongezeka
kutokana na watu kutambua upatikanaji wa huduma hizo na mafanikio ya watu
waliowahi kutibiwa na kushauriwa na madaktari
hao wa kimataifa wenye ujuzi mkubwa. Hata
hivyo Watanzania bado wanakosa njia za kupambana na magonjwa haya tangu mwanzo.
Madokta walikuwa na maoni kwamba, mwamko utaongezeka kama watu wanatapata elimu
ya kutosha kutoka kwa madaktari juu ya
uzuiaji wa magonjwa haya kwa kutambua dalili za mwanzo.
Daktari.
V. Rajagopal na SanjayMaitra walisisitiza umuhimu kuzuia magonjwa haya na pia
kufanya vipimo mara kwa mara. Waliendelea
kusema kwamba magonjwa haya huwapata hasa watu wenye umri mkubwa lakini pia
huweza kuzuilika. Watanzania wanatakiwa kuwa makini kutokana magonjwa mengi
yanayotokana na figo hasa kwa watu wazima ni kutokana na Shinikizo la Damu,
Kisukari, wingi wa Lehemu, kutofanya mazoezi, Ulaji mbaya pia utumiaji usio
sahihi wa dawa hasa za kutuliza maumivu. Hivyo
husababisha ulemavu wa figo.
Pia
Dkt. Sanjay Maitra alitoa ushauri ni
vyema kuzingatia vipimo mara kwa mara kwani inasaidia watu kujua afya zao.Alitoa mfano wa mtu mmoja, ambaye ni dereva mwenye ujuzi wa miaka hamsini na
kipindi chote alikuwa anaumwa miguu na mwishowe aligundulika kuwa na kisukari
kwa miaka kumi na tano. Pia mgonjwa huyo hakujua kuhusu shinikizo la damu wala
hakuwa na walipompima walimgundua hana uwezo wa kuona vizuri. Dkt. Sanjay Maitra
aligundua kuwa ana ugonjwa wa kisukari. Pia kwa bahati mbaya pia watanzania
wengi wanashabihiana na mfano huo kwa kuwa hawajui dalili mwanzo za magonjwa
haya. Aliongeza kwa kusema kuwa ni muhimu kwa wao kutembelea kwani wameleta mwamko
mkubwa.Pia Madokta hawa wametoa wito kwa Watanzania kupata taarifa zaidi juu ya
kupambana na magonjwa haya ili kuishi kwa afya njema na maisha marefu.
Tukio hili la madaktari kutembelea taasisi za afya hapa
nchini lengo ni kuleta ushirikiano
katika huduma za afya na mafunzo kwa madaktari wa hapa nchini.
Dkt. Sanjay Maitraamesema ni jambo gumu na linahitaji hela
nyingi kwa wagonjwa kusafiri nje ya
nchi, hivyo yeye ameona ni vyema kuweka muda ili kuja kutoa huduma kwa ukaribu zaidi. Anatumaini kwamba wagonjwa watatibiwa kwa
urahisi hata wakiwa nje ya nchi.
Lengo
la ujio wao si kwamba kuwachukua wagonjwa na kuwatibia katika Hospitali za
Apollo bali ni kuwapa ushauri sahihi na kuwasaidia kufanya maamuzi sahihi ya
matibabu. Mbali na suala la wagonjwa lakini tumeona pia wachache kati yao wataweza
kwenda Apollo kama watahitaji matibabu.
Alipoulizwa
kuhusu watanzania watakachopata wakienda Hospitali za Apollo, Dkt. V Rajagopal
alisema kwamba mpango wa Kimataifa wa Apollo ni kusaidia wagonjwa na washirika
wao ili kurahisisha huduma za afya. Pia wanatoa ratiba ya uteuzi, usafirishaji,
na huduma za ukalimani kwani Hospitali za Apollo pia zinatoa huduma ya
ukalimani kwa lugha ya Kiswahili ili kuwahudumia wagonjwa wanaotoka Kenya,
Uganda na Tanzania kwa urahisi. Hospitali
za Apollo zinajulikana kwa kwenda mbali zaidi kuwafanya wagonjwa kuhisi unafuu.
Mwaka
2014, Mji wa Apollo (Apollo Health City) Hderabad, ulipata tuzo ya heshima ya KIMATAIFA
YA MATIBABU NA UTALII kutoka Jarida la
Kimataifa la Matibabu na Usafiri
kutokana na utoaji wa huduma bora kwa wateja.
Hospitali
za Apollo zinamfanya mgonjwa ajisikie kama yupo nyumbani kwani huwaandalia
wagonjwavyakula vikuu kama ugali, ndizi mtori, ingawa wagonjwa wengi wa
kiafrika wanapenda kujaribu vyakula vya kihindi. Pia mapishi yanaenda mbali
zaidi kwa kuandaa chakula cha watoto na watu wazima. Chakula ni muhimu sana kwa
wagonjwa ili kuwa na afya. Hospitali za Apollo zinaamini kwamba “kama
tunafahamu chakula basi pia tunafahamu tamaduni husika”.
Kuhusu
Apollo:
Mnamo mwaka 1993, Dkt. Prathap C. Reddy,
mbunifu wa afya nchini India, alianzisha hospitali ya kwanza ya ushirika nchini
India, Hospitali za Apollo Chenai. Kwa miaka mingi, Hospitali za Apollo
zimeweza kukua kufikia moja ya shirirka kubwa la afya barani Asia likiwa na
uwezo wa zaidi ya vitanda 8,500 ndani ya Hospitali 50, zaidi ya maduka 1350 ya
dawa na zaidi ya kliniki za uchunguzi 100.
Pia hospitali za Apollohutoa huduma za matibabu kwa utaratibu wa
kibiashara, huduma za bima za afya na kitengo cha tafiti za kitabibu kwa lengo
la kufanya tafiti za magonjwa ya milipuko, seli shina za mwili na maumbile.
Kuendeleza vipaji ili kumudu hitaji linaloongezekaa katika utoaji huduma za
hali ya juu, Hospitali za Apollo zina jumlaa ya vyuo 11 vya madaktari pamoja na
wauguzi. Mafanikio haya yamezifaidisha Hospital za Apollo kupata tuzo mbali
mbali, ikiwa ni pamoja na tuzo ya kituo bora iliyotolewa na serikali ya India
pamoja na kutambulika na tume ya pamoja ya kimataifa ( Hospitali saba za Apollo
zinatambuliwa na kutunikiwa na tume ya pamoja ya kimataifa). Katika hesima
nadra, serikali ya india ilitoa mhuli wa kumbukumbu wa kuutambua mchango wa
Hospitali za Apollo Dkt. Prathap C Reddy,
alitunukiwa tuzo ya heshima ya Padma Vbhushan’ mnamo mwaka 2010.
Ushirika wa Hospitali za Apollo kwa zaidi ya miaka 50, umeendelea kuboresha
uongozi katika uvumbuzi wa kitabibu, huduma za kimataifa na maendeleo ya
kiteknolojia. Hospitali zetu zimekuwa katika nafasi ya juu kimatifa katika
huduma za kitabibu pamoja na utafiti.
No comments:
Post a Comment