Mgombea mwenza wa CCM nafasi ya urais, Bi. Samia Suluhu akiwasikiliza akinamama wakimuelezea kero ya maji baada ya kumsimamisha na kumpa kero hizo Jimboni Longido. Wakinamama wilayani Longido wakiendelea kuteka maji kwa zamu baada ya kumaliza kumueleza kero zao Bi. Samia Suluhu aliepita maeneo hayo. Baadhi ya wanaCCM na wananchi wa Jimbo la Monduli wakiwa kwenye mkutano wa hadhara wa mgombea mwenza nafasi ya urais wa CCM, Bi. Samia Suluhu. Baadhi ya wanaCCM na wananchi wa Jimbo la Monduli wakiwa kwenye mkutano wa hadhara wa mgombea mwenza nafasi ya urais wa CCM, Bi. Samia Suluhu. Baadhi ya wanaCCM na wananchi wa Jimbo la Monduli wakiwa kwenye mkutano wa hadhara wa mgombea mwenza nafasi ya urais wa CCM, Bi. Samia Suluhu. Mgombea mwenza wa CCM nafasi ya urais, Bi. Samia Suluhu akiwa katika vazi la kimasai alilopewa kama zawadi na wanaMonduli. Baadhi ya wajumbe wa kamati ya kampeni ya CCM taifa wakiwa katika mkutano wa hadhara wa mgombea mwenza Bi. Suluhu. Baadhi ya wanaCCM na wananchi wa Jimbo la Monduli wakiwa kwenye mkutano wa hadhara wa mgombea mwenza nafasi ya urais wa CCM, Bi. Samia Suluhu. Bi. Samia Suluhu akimnadi mgombea ujumbe wa Jimbo la Monduli, Bi. Namelok Sokoine (kushoto) kwenye mkutano wa hadhara. Baadhi ya wanaCCM na wananchi wa Jimbo la Monduli wakiwa kwenye mkutano wa hadhara wa mgombea mwenza nafasi ya urais wa CCM, Bi. Samia Suluhu.
Na Joachim Mushi, Longido
WANAWAKE wa Wilayani Longido wamemsimamisha mgombea Mwenza wa urais Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bi. Samia Suluhu njiani akielekea jukaani kuhutubia wananchi wakimlilia kuwatatulia kero ya maji katika Kata ya Longido ambapo kila familia imekuwa ikipata huduma hiyo mara moja kwa wiki hali ambayo wamesema haikidhi mahitaji.
Bi. Samia alilazimika kusimama eneo ambalo wanawake walikuwa wamefurika wakichota maji kwa zamu huku kila familia ikipewa idadi ya ndoo kumi mara moja kwa kila wiki kiwango ambacho akinamama wengi walisema akikidhi mahitaji kwa familia zao.
Mgombea huyo wa CCM aliwahakikishia akinamama hao kuwa yeye kama mwanamke anajua shida ya maji inavyowatesa akinamama katika familia ikiwa huduma hiyo inapokuwa tatizo katika upatikanaji wake, hivyo atalisimamia suala hilo.
Alisema Serikali ya CCM itakapoingia madarakani imetenga shilingi bilioni 13 kwa ajili ya kupeleka maji eneo la Longido mradi ambao utamaliza kero ya maji eneo hilo.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara Longido Bi. Suluhu alisema kwa kuwawezesha wafugaji wa eneo hilo wamepanga kujenga mabwawa ya kuvuna na kuhifadhi maji kwa ajili ya matumizi ya nyakati za ukame kwa baadhi ya maeneo, ikiwa ni pamoja na kujenga majosho ya mifugo na kuwezesha madawa ya mifugo kwa wafugaji ili kuwaendeleza.
"...Kazi hii tutaifanya ndani ya kipindi kifupi mara tu baada ya kufanikiwa kurudi madarakani, Serikali inayomaliza muda wake imefanya mengi na sisi tutaendeleza na kuboresha zaidi. Alisema wanajua kilio cha mahakama katika wilaya ya Longido hivyo mara baada ya kuingia madarakani wataijenga.
Alisema akiwa njiani katika mikutano ya kampeni zake ameshuhudia uwepo wa ukame katika vijiji lakini anawahakikishia hakuna mwananchi ambaye atakufa na njaa endapo hali hiyo ya ukame itaendelea, kwani serikali ya CCM katika ghala la chakula ina akiba ya kutosha.
Mgombea huyo mwenza wa CCM pia alifanya mkutano wa hadhara katika Jimbo Monduli aliwaomba wanaMonduli kumpigia kura ya ndio mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Dk. John Pombe Magufuli ili aweze kutekeleza ilani ya chama hicho ambayo pia imejumuisha ujenzi wa barabara ya Sanya Juu hadi Longido na Longido hadi Mto wa Mbu wilayani Longido.
Aliwaomba wanaMonduli kumchagua mgombea ubungw wa Jimbo la Monduli kwa tiketi ya CCM, Bi. Namelok Sokoine kwani mgombea huyo anarekodi na historia nzuri ya utendaji kama alivyokuwa babayake marehemu, Edward Moringe Sokoine. Aliwaomba pia kuwachagua madiwani wa CCM ili waweze kufanya kazi kwa ushirikiano kama timu.
No comments:
Post a Comment