Mwenyekiti
wa Shirikisho la Vyama vya Wachimbaji Madini Tanzania (FEMATA), Gregory
Kibusi akiwasilisha mada kuhusu wachimbaji wadogo wa madini katika
Semina ya Wathamini Madini ya Vito na Almasi nchini, iliyofanyika hivi
karibuni (Agosti 12 na 13, 2015) katika Hoteli ya Gold Crest jijini
Mwanza.
Mkurugenzi
wa Utawala na Rasilimaliwatu, Mrimia Mchomvu, akitoa hotuba ya kufunga
Semina ya Wathamini Madini ya Vito na Almasi nchini iliyofanyika hivi
karibuni (Agosti 12 na 13, 2015) katika Hoteli ya Gold Crest jijini
Mwanza.
Baadhi
ya washiriki wa Semina ya Wathamini Madini ya Vito na Almasi nchini,
wakifuatilia kwa umakini mada zilizokuwa zikiwasilishwa. Semina hiyo
ilifanyika hivi karibuni (Agosti 12 na 13, 2015) katika Hoteli ya Gold
Crest jijini Mwanza.
Mkurugenzi
wa Kitengo cha Uthaminishaji wa Madini ya Almasi na Vito cha Wizara ya
Nishati na Madini (TANSORT), Archard Kalugendo, akiwasilisha mada kuhusu
majukumu ya Kitengo hicho katika Semina ya Wathamini Madini ya Vito na
Almasi nchini iliyofanyika hivi karibuni (Agosti 12 na 13, 2015) katika
Hoteli ya Gold Crest jijini Mwanza.
Baadhi
ya washiriki wa Semina ya Wathamini Madini ya Vito na Almasi nchini,
wakifuatilia kwa umakini mada zilizokuwa zikiwasilishwa. Semina hiyo
ilifanyika hivi karibuni (Agosti 12 na 13, 2015) katika Hoteli ya Gold
Crest jijini Mwanza.
Afisa
kutoka Kitengo cha Uthaminishaji wa Madini ya Almasi na Vito cha Wizara
ya Nishati na Madini (TANSORT), Salome Tilumanywa, akiwasilisha mada
kuhusu uchimbaji na biashara ya tanzanite katika Semina ya Wathamini
Madini ya Vito na Almasi nchini, iliyofanyika hivi karibuni (Agosti 12
na 13, 2015) katika Hoteli ya Gold Crest jijini Mwanza.
Kaimu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Ngosi Mwihava (Wa
pili kushoto – waliokaa mbele), akiwa katika picha ya pamoja na
Washiriki wa Semina ya Wathamini Madini ya Vito na Almasi. Wengine
kutoka Kulia (waliokaa) ni Kamishna Msaidizi wa Madini Kanda ya Ziwa
Victoria - Magharibi, Mhandisi David Mulabwa, Mkurugenzi wa Utawala na
Rasilimaliwatu Mrimia Mchomvu, pamoja na Mkurugenzi wa Kitengo cha
Uthaminishaji wa Madini ya Almasi na Vito cha Wizara ya Nishati na
Madini (TANSORT), Archard Kalugendo.
Wachimbaji madini wadogo waipongeza Serikali
Na Veronica Simba – aliyekuwa Mwanza
Shirikisho
la Vyama vya Wachimbaji Madini Tanzania (FEMATA), limetoa pongezi kwa
Serikali kupitia Wizara ya Nishati na Madini, hususani Kitengo cha
Uthaminishaji Madini ya Vito na Almasi (TANSORT), kwa jitihada
inazofanya kuwainua wachimbaji wadogo nchini.
Pongezi
hizo zilitolewa hivi karibuni na Mwenyekiti wa FEMATA, Gregory Kibusi
wakati akiwasilisha mada kuhusu wachimbaji wadogo wa madini katika
Semina ya Wathaminishaji Madini ya Vito na Almasi iliyofanyika Agosti 12
na 13, Hoteli ya Gold Crest jijini Mwanza.
“Kwa
niaba ya uongozi wa FEMATA, naipongeza Serikali hasa Kitengo cha
TANSORT kupitia Wizara ya Nishati na Madini, kwa jitihada za makusudi
kabisa za kuwainua wachimbaji wadogo nchini.”
Akifafanua
zaidi, Kibusi alisema kuwa wachimbaji wadogo wamekuwa wakikutana na
changamoto nyingi lakini kutokana na ushirikiano ambao Serikali inautoa,
hakuna shaka malengo yaliyomo katika Sera ya Madini ya Mwaka 2009
yatatimia.
Kibusi
alisema, kupitia jitihada zinazofanywa na Serikali, wachimbaji wadogo
wamekuwa na mwamko wa kupata taarifa za mipango na mikakati ya Serikali
juu ya maendeleo yao.Pia,
alisema jitihada za Serikali zimewezesha wachimbaji wadogo kushiriki
maonesho ya madini ya vito na usonara ya ndani na nje ya nchi.
“Aidha,
Serikali kupitia Wizara ya Nishati na Madini imeanza kutoa ruzuku kwa
wachimbaji wadogo sambamba na Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) kuwa
mlezi wa wachimbaji wao,” alisema Kibusi.
Kibusi
alisema wachimbaji wadogo wanakumbana na changamoto kadhaa ikiwa ni
pamoja na uwezo mdogo wa kifedha katika kuendesha shughuli zao za
uchimbaji na ukosefu wa elimu ya juu ya madini hasa ya vito.
Alitaja
changamoto nyingine kuwa ni wachimbaji wadogo wa madini kutotambuliwa
na baadhi ya Taasisi za Serikali na zisizo za kiserikali kama wadau
wakubwa wa maendeleo hasa kiuchumi na kijamii.
Akiwasilisha
maombi ya FEMATA kwa Serikali, Kibusi alisema wachimbaji wadogo
wanahitaji wataalamu wa madini ya vito ili wawasaidie katika masuala
mbalimbali ikiwa ni pamoja na kutambua, kuthamini, kusaidia kutafuta
masoko pamoja na kutoa ushauri juu ya uongezaji thamani madini na namna
bora ya kufanya biashara ya madini.
No comments:
Post a Comment