Thursday, August 27, 2015

TIMU ZA FC BONGO NA FC KILIMANJARO ZILITOKA SARE YA MABAO MAWILI MAWILI KATIKA MECHI ILIYOFANYIKA KTK JIJI LA HELSINKI NCHINI FINLAND

Mechi ilianza kwa kasi na dakika 1 tu ya mchezo fc bongo walipata bao lao la kwanza kwa mkwaju wa penalt lililofungwa na mchezaji wao machachari Abass Kunha.

Kilimanjaro ilikuja juu na kufanikiwa kusawazisha kwa kona iliyopigwa na Richard Joseph ambayo ilimshinda nguvu kipa wa fc Bongo baada ya purukushani ndani ya lango hilo.

Kipindi cha pili kilianza kwa nguvu na kwenye dkk ya 80 Abass Kunha aliongeza bao la pili, vijana wa kilimanjaro waliongeza nguvu na baada ya dkk 5 wakafanikiwa kukomboa kwa goli maridadi kabisa lililofungwa na Captein wa kilimanjaro Mohamed Machupa.

Mechi ilikuwa nzuri na ya kupendeza.
Kikosi cha Fc Kilimanjaro
kikosi cha Fc Bongo
Vikosi vyote kwenye picha ya pamoja kabla ya bambano.
Wachezaji, viongozi na mashabiki wakipata dinner la pamoja.




No comments: