Monday, August 24, 2015

TATIZO LA MAJI KILOLO NA ISMANI LAISUMBUA SERIKALI WADAI KUTOKUTHAMINIWA NA VIONGOZI

WANANCHI wa vijiji vya Ilole, kitumbuka, Ilambilole, Ikengeza, Chamdindi  na vingine vilivyopo Katika wilaya ya Kilolo na Ismani mkoani Iringa wailalamikia serikali kwa kushindwa kutatua kero ya maji iliyodumu kwa muda mrefu Katika maeneo hayo.

Wakizungumza kwa huzuni mbele ya mkuu wa mkoa wa Iringa aliyefanya ziara ya kugagua miradi ya maji Katika wilaya hizo Mh Amina Masenza wananchi hao walisema kumekuwa na ubabaishaji wa kisiasa juu ya namna ya kupelekewa maji jambo ambalo linawafanya waweze kutumia maji yasiyo salama kwa afya zao.

Wananchi hao walisema kumekuwa na miradi ya maji mingi ambayo ilitajiwa kuwanzishwa Katika wilaya zao lakini mpaka sasa hakuna utekerezaji wowote juu ya kutatua kero hizo pamoja na kuwa na vyanzo vizuri vya maji.
 “mh mkuu wa mkoa tumeahidiwa sana juu ya kuletewa maji safi huku vijijini matokeo yake hakuna lililofanyika tumekuwa watu wa kudanganywa kabisa hata tukiangalia umbali wakilipo chanzo cha maji hata wangesema tuchimbe mitalo wenyewe tungechimba ila wanatudanganya na siasa zao hatuyajui maji ya baridi toka tunazaliwa tunatumia maji ya chumvi tuoneeni huruma jamani” walisema wananchi

Akijibu kero za wananchi hao mkuu wa mkoa Amina Masenza alisema kumekuwa na watumishi wa serikali ambao wamepelekwa kusomea utalamu huo lakini bado hawafanyi kazi sawasawa na elimu zao ambapo ameahidi kulishughulikia jimbo hilo pamoja na kusimamia miradi mipya iliyopo ili iweze kuwanufaisha wananchi kwa kupata huduma hiyo kwa urahisi.

“nimesikia kilio cha wananchi sitakubali haya yaenelee kutokea wakati kuwa watu wanapelekwa kusoma na serikali halafu hafanyi inavyotakiwa tafadhari nataka kuona kazi mnayo ifanya ili wananchi hawa waweze kupata maji kwa wakati kulinga na elimu zenu haiwezekani wananchi wangu wakawa wanaumia na nyie mpo hapa haitawezekana”alisema Masenza

Aidha aliwaagiza watendaji wa halmashauri na wataalamu wa sekta ya maji kufanya uchunguzi Katika maeneo ambayo yanalalamikiwa na wananchi ili kubaini chanzo cha tatizo na kukiondoa ili kuruhusu upatikanaji wa huduma hiyo ikiwa n sambamba na wafugaji wanaotumia maji ya mto kunywesha mifungo yao swan a watumiaji wengine wa kawaida ili kulinda usawa Katika matumizi ya maji.

“ninawaagiza kuanzia leo nendeni kuchunguza nini tatizo nataka majibu kuanzia sasa na mniambie tatizo ninini linalofanya wananchi hawa wasipate maji mradi umefika na pia wanaelimishwa juu ya matumizi ya mita na wale wanaonywesha mifugo kwa mito wanatakiwa kulipiwa maji kwa kadiri na idadi ya mifugo aliyonayo”alisema masenza

Kwa upande wake Injinia wa Maji na meneja mradi wa Maji vijijini Bw Endru Kisaru alisema kwasasa wanaongeza nguvu ya udhibiti wa matumizi ya maji kwa kufunga mita kwani kwa sasa Katika jimbo la ismani idadi ya watumiaji inakaribia 15000 ambapo kila kaya inaweza kulipa kiasi cha sh 5000 kwa mwaka ambapo tayari Unit 267 zimefungwa Katika maeneo hayo hivyo amewahakikishia wananchi kwa tatizo na kero hiyo ya maji itamalizika kwa wakati muafaka


“tutajitahidi kutengeneza miundombinu ya maji itakayo hakikisha tunawafikishia huduma ya maji wananchi wengi zaidi nawaomba wananchi wawe na uvumilivu wakati tunaendelea kutatua baadhi ya changamoto zilizopo”alisema kisaru.

No comments: