Wednesday, August 12, 2015

SIMU TV: HABARI ZA USIKU HUU

Watanzania na raia wa China 60 waanza safari za baiskeli kutoka Dar es salaam hadi Arusha kwa lengo la kuongeza uelewa wa jamii juu ya mauaji ya wanayama pori hasa Tembo.http://youtu.be/b_fF32KxHtY

Wakazi wa Musoma wataka uwepo wa mikakati imara ya kutokomeza vitendo vya uvuvi haramu ndani ya ziwa Victoria na kutoruhusu zana haramu za uvuvi. http://youtu.be/65zSwdtdL5w

Serikali yashauriwa kuboresha miundombinu ya reli ili kuokoa asilimia 25 hadi 30 ya bei ya mazao ya chakula na biashara amabayo wakulima wanapoteza wakati wa usafirishaji. http://youtu.be/IV84pQibgOY

Baada ya kumalizika mchakato wa kura za moani ndani ya CCM baadhi ya wananchi wakishauri chama hicho kuyaengua majina ya wagombea watakao thibitika kujihusisha na rushwa. http://youtu.be/4UF98zLPpqU

SUMATRA yatoa mafunzo kwa wanafunzi wa shule za msingi jijiini Dar es salaam ili kujua haki za msingi za utumiaji wa usafiri hususani kwa wanafunzi. http://youtu.be/09wllfEjapo

Watumiaji wa barabara zipitazo ndani ya mfumo wa barabara za mabasi yaendayo kasi jijini Dar es salaam watakiwa kuzingatia alama za barabarani kuepuka ajali zisizo za rasmi. http://youtu.be/M2MK3COd35g

Maisha ya baadhi ya wakazi wa Segerea yako shakani kufuatia uwepo wa kiwanda haramu cha kuchakachua gesi katika eneo lao. http://youtu.be/UHg-eKX6LKo

Waziri wa nishati na madini akanusha uwepo wa uchimbaji usafirishaji holela wa madini ya urani wilayani Namtumbo. http://youtu.be/1YZb7CxvTNQ

Chama cha CUF kimetangaza wagombea wake wa ubunge na nafasi za uwakilishi katika majimbo yote visiwani Zanzibarhttp://youtu.be/irMQcsmtOhA

Wakazi wa mkoa wa Kilimanjaro washiriki kuuaga mwili wa aliyekuwa mwasisi wa TANU na ASP Peter Kisumohttp://youtu.be/whw4awoBmg8

Katibu mkuu wizara ya habari,vijana utamaduni na michezo,wataka vijanan chini kujitokeza kwa wingi na kushiriki kikamilifu katika uchaguzi mkuu ujaohttp://youtu.be/RIojci20vMU

Serikali yasema hakuna athari yeyote mbaya iliyojitokeza nchini kufuatia machafuko na mgogoro unao endelea kurindima nchini Burundi. http://youtu.be/6Mwy0G_OffQ

Baraza la vijana la chadema BAVICHA,yaiomba tume ya taifa ya uchaguzi NEC kuongeza siku za uhakiki katika daftari la mpiga kura kwani siku zilizotolewa hazitoshi. http://youtu.be/e68EPPsRHiw

TANESCO yasisitiza mikoa yote iliyounganishwa kwenye gridi ya Taifa kuendelea kupata mgao wa umeme mpaka ujenzi wa mitambo utapo kamilika. http://youtu.be/cMIN3EQyN_k

Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzana awaongoza wananchi wa Masasi kuaga mwili wa Mbnge wa CUF Clara Mwatuka, aliyefariki kwa ajali ya ajalihttp://youtu.be/9jyjC13xqOM

Baada ya mamlaka ya TCRA kuanisha kuanza kwa matumizi ya sheria ya mtandao baadhi ya wadau walalamikia uwepo wa vipengele kandamizi.

Chama cha Mapinduzi CCM,kimeamuru kurudiwa kwa uchaguzi katika jimbo la Chilonya Mkoani Dodoma kufuatia mapungufu ya awali. http://youtu.be/XMd2giiYrew

Baadhi ya wanachama katika Manispaa ya Ilala walalamikia kutolipwa stahili zao baada ya kumaliza zoezi la uandikishaji la BVR kufuatia kutoa huduma. http://youtu.be/Y0sngRZoD2k

Makada wa CCM wapuuza hatua za makada wenzao kuhamia vyama pinzani wakisema hilo ni swala la kawaida katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu. http://youtu.be/4EWvFDgDgpA

Chama cha Mapinduzi CCM,kimeamuru kurudiwa kwa uchaguzi katika jimbo la Chilonya Mkoani Dodoma kufuatia mapungufu ya awali. http://youtu.be/XMd2giiYrew

Baadhi ya wanachama katika Manispaa ya Ilala walalamikia kutolipwa stahili zao baada ya kumaliza zoezi la uandikishaji la BVR kufuatia kutoa huduma. http://youtu.be/Y0sngRZoD2k

Makada wa CCM wapuuza hatua za makada wenzao kuhamia vyama pinzani wakisema hilo ni swala la kawaida katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu. http://youtu.be/4EWvFDgDgpA

Aliyekuwa Mbunge wa Sikonge kwa tiketi ya CCM Said Nkumba, amekihama chama hicho na kujiunga na CHADEMAhttp://youtu.be/kxliGMJUNOA

Huduma ya usafiri wa treni ndani ya jiji la Dar es salaam imesitishwa bila taarifa yeyote huku wakazi wa jiji hilo wakibaki na sintofahamu juu ya swala hilo.

No comments: