Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) inashiriki
kwenye maonesho ya Nananane ambayo Kitaifa yanafanyika kwenye viwanja vya
Ngongo Mkoani Lindi.
Katika maonesho hayo ambayo yanabebwa na Kauli Mbiu ya
Matokeo Makubwa Sasa: Tuchague viongozi bora kwa maendeleo ya kilimo na ufugaji , NSSF itakuwa ikitoa huduma
mbalimbali zikiwemo elimu juu ya scheme zake za Wakulima na Wavuvi, kuandikisha
wanachama wapya, kutoa taarifa za michango na kutoa elimu ya mafao mbalimbali yatolewayo
na NSSF kama vile matibabu, kuumia kazini, uzazi, pensheni ya uzee,ulemavu na
urithi.
Kauli mbiu ya mwaka huu inaendana sana na azma ya NSSF
kuwafikia wakulima,wafugaji na watu wengine wasio katika ajira rasmi kujiunga
na mfuko huo na kupata mafao yote saba sawa na walio katika ajira rasmi.Aidha
Shirika limeshaandikisha wanachama zaidi ya elfu sabini kutoka katika sekta
isiyo rasmi na malengo ni kuhakikisha kila mtanzania anapata hifadhi ya jamii.
NSSF inawakaribisha wakazi wa Lindi na Mtwara kwenye
Banda lao ili waweze kupata huduma hizi kwa ajili ya kuboresha maisha yao na
familia zao.
Banda la NSSF linavyoonekana kwa mbele kwenye Maonesho ya
Nanenane kitaifa mkoani Lindi.
Kaimu Meneja wa Mkoa wa Lindi Kabonwa Kandoro (kulia)
akimpa maelezo mwanachama juu ya mafao mbalimbali yatolewayo na NSSF wakati
Afisa Uandikishaji Tuli Mwaipopo
akichukua taarifa za mwanachama mwengine kwa Lengo la Kumtengenezea kadi mpya
ya NSSF kwenye maonesho ya Nanenane Lindi.
Kaimu Meneja Mkoa wa Lindi Kabonwa Kandoro akitoa maelezo
kwa mmoja wa wanachama wa NSSF waliotembelea kwenye Banda la NSSF kwenye
maonesho ya Nanenane.
Afisa Uhusiano Mwandamizi, Salim Kimaro akimpa maelezo
mmoja wa watu waliofika kwenye Banda la NSSF kwenye maonesho ya Nanenane Lindi.
Afisa Teknohama, Rukia Penza akimpata taarifa za michango
yake mmoja wa wanachama aliyetembelea kwenye Banda la NSSF.
Afisa Uandikishaji wa NSSF Mkoa wa Lindi Tuli Mwaipopo
akichukua taarifa za Mwanachama kwa ajili ya kutengeneza kadi mpya ya
mwanachama huyo.
No comments:
Post a Comment