Baadhi ya viongozi wa vyuo vya ualimu nchini wakibadirishana mawazo nje ya ukumbi.
Baadhi ya washiriki katika picha ya pamoja na mgeni rasmi.
Mkurugenzi wa Uendeshaji wa NSSF , Crescentius Magori akitoa ufafanuzi wa masuala muhimu ya Mfuko wa NSSF kwa waandishi wa habari.
Washiriki wa warsha kuhusu mfuko wa NSSF ambao ni viongozi wa vyuo vya ualimu nchini wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi .
Washiriki wa warsha ya NSSF kubadirishana mawazo.
Washiriki wakisililiza jambo kutoka kwa mmoja wa watoa mada za NSSF.
Na John Nditi, Morogoro.
SHIRIKA la Taifa la Hifadhi ya Jamii ( NSSF), limewataka waajiri wa sekta mbalimbali nchini wanaodaiwa madeni ya makato kutoka kwa waajiriwa wao ambao ni wanchama wa mfuko huo kulipa madeni yao ndani ya mwezi mmoja kuanzia Septemba mwaka huu .
Mkurugenzi wa Uendeshaji wa NSSF , Crescentius Magori, alisema hayo Augosti 29, Mmwaka huu mjini Morogoro wakati alipokuwaakizungumza na waandishi wa habari baaada ya kufungua warsha ya siku moja ya kutoa elimu kwa viongozi wakuu wa vyuo vya ualimu nchini juu ya namna mfuko huo unavyofanya kazi ya kutoa huduma zake kwa wanachama.
Magori alisema wale ambao watashindwa kulipa madeni yao katika muda huo ,uongozi wa NSSF utawafikisha mahakamani kwa mujibu wa sheria na watalazimika kulipa na adhabu iliyowekwa.
Alisema , zoezi la kufuatilia madeni kutoka kwa waajiri sugu walioshindwa kuwasilisha kwa wakati makato litaanzia mkoa wa Dar es Salaam na baadaye litaendelea katika nchi nzima.
“ Kuanzia wiki hii ‘ Augosti 31’ NSSF itafuatilia wadaiwa wote ambao wameshindwa kulipa madeni ya makato ya michango ya wanachama wa NSSF na tunaanzia na mkoa wa Dar es Salaam na baada ya hapo zoezi litaendelea nchini kote” alisema Magori.
Alisema ,baada ya kipindi hicho kumalizika, waajiri ambao watakuwa wameshindwa kulipa madeni yao, NSSF utatumia sheria ilizopo kuwafikisha mahakamani ambapo watalazimika kulipa na adhabu .
Mkurugenzi wa Uendeshaji wa NSSF alitolea mfano kwa kusema katika waajiri 100 kati yao 20 hawaleti michango baada ya kuwakata waajiri wao , wengine ni kwa sababu za kiuchumi na baadhi ni wakorofi .
“ NSSF itatumia njia zote za kukutana na waajiri hawa na kuzungumza nao na endapo utaratibu wote ukishindikana tutawapeleka mahakamani “ alisema Magori.
Alitumia fursa hiyo kutoa rai kwa waajiri wote wa mkoa wa Dar es Salaam kulipa madeni yao ndani ya mwezi mmoja ,ambapo pia zoezi hilo maalumu litafanyika katika nchi nzima baada ya kukailika kwa mkoani humo.
Pia aliwataka wanachama kuhakikisha wanakuwa na taarifa sahihi za ajira zao na kufuatilia michango yao kama inawasilishwa kwa wakati kupitia Ofisi za NSSF ili kuwaondolea usubufu wakati wa muda wa kulipwa mafao hayo ya pensheni.
Magori alisema, NSSF inatarajia kusogeza huduma zake kwa kuwatumia mawakala katika maeneo mbalimbali watakaokuwa na jukumu la kuingiza wanachama nchini.
Alisema warsha hiyo kwa viongozi wa vyuo vya ualimzu nchini ni mkakati endelevu wa kutoa elimu pana zaidi kwa makudi mbalimbali ili wajiunge na mfuko huo wakiwa na uelewa mpana badala ya kuwavizia wakati wa wanapoajiriwa .
Mkurugenzi wa Uendeshaji wa NSSF Alisema , tayari warsha kama hiyo imefanyika kwa Mahakimu na Majaji kwa mkoa wa Dar es Salaam iliyolenga wao kuweza kuzijua sheria za mfuko huo hasa wanapokuwa wakiendesha mashauri yanaohusiana na waajiri dhidi ya NSSF.
Nao baadhi ya washiriki Baraka Mwakyeja , ambaye ni Ofisa Utawala wa Chuo Kikuu Mkwawa , pamoja na Maria Mdee , Ofisa Rasilimali watu wa Chuo Kikuu Kishiriki Elimu (DUCE), kwa nyakati tofauti walisema, elimu waliyoipata itawasaidia wao na wanachuo ambao ni waajiriwa watarajiwa serikalini kuwa na ufahamu na umakini wa kuchagua mifuko ya kujiunga nayo.
Walisema NSSF imeweka utaratibu mzuri wa kutoa kwanza elimu juu ya faida anazozipata mwanachama anayejiunga na mfuko huo tofauti na mingine ambayo inasubiri tu pale mwajiriwa akiwa tayari katika ajira na hivyo kukosa umakini katika maamuzi yake ya kuchangua mfuko huliosahihi.
No comments:
Post a Comment