Monday, August 10, 2015

NCCR-MAGEUZI WAANZA KUSHAMBULIA JIMBO LA VUNJO,WAWATAMBULISHA WAGOMBEA WA NAFASI YA UDIWANI

Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama cha NCCR-Mageuzi taifa ,Hemed Msabaha akizungumza wakati wa mikutano wa kutamburisha wagombea wa nafasi ya udiwani inayofanyika katika jimbo la Vunjo mkoani Kilimanjaro.
Baadhi ya viongozi wa NCCR-Mageuzi jimbo la Vunjo wa kiwa katika moja ya mikutano hiyo kata ya Makuyuni.
Msaidizi wa Mwenyekiti wa Chama cha NCCR-Mageuzi taifa na Mbunge wa kuteuliwa, James Mbatia ,Bw Hamis Athuman akitoa salamu za mwenyekiti huyo wakati wa mkutano wa utamburisho wa wagombea wa nafasi za udiwani kupitia chama hicho.
Baadhi ya wakazi wa kata ya Makuyuni wakiwasikiliza viongozi wa chama hicho.(hawako pichani).
Aliyekuwa kada wa Chama cha TLP,Stanley Temba akiwa ameibukia katika jukwaa la NCCR-Mageuzi akizungumza katika moja ya mikutano ya Utamburisho wa wagombea wa nafasi ya Udiwani katika kata zilizoko ndani ya jimbo la unjo.
Aliyekuwa Diwani kupitia chama cha TLP,Yolanda Lyimo akizungumza katika jukwaa la chama cha NCCR-Mageuzi.
Yolanda Lyimo akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika viwanja vya njia Panda.
Baadhi ya wananchi katika jimbo la Vunjo wakiitikia salamu za vyama vinavyounda UKAWA.
Kikundi cha sarakasi kikitoa burudani katika mikutano hiyo.
Baadhi ya wananchi katika kata ya Njia Panda wakifuatilia mkutano wa hadhara uliolenga kumtamburisha mgombea wa nafasi ya udiwani katika kata hiyo.
Baadhi ya wananchi katika kata ya Njia Panda.
Viongozi wa chama cha NCCR-Mageuzi wakicheza mara baada ya kumalizika kwa mkutano wa hadhara uliofanyika katika eneo la Njia Panda.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

No comments: