Thursday, August 20, 2015

MTANDAO WA WAANDISHI WA MASUALA YA HAKI YA AFYA YA UZAZI NA JINSIA WAZINDULIWA JIJINI DAR


Mratibu wa Uzazi Salama Kitaifa, Dk. Koheleth Winani akizungumza na waandishi wa habari za masuala ya haki jinsia na uzazi katika mkutano uliofanyika leo katika hoteli ya Land Mark jijini Dar es Salaam.


Kaimu Mwenyekiti wa Mtandao wa waandishi wa habari wa Haki na Afya  ya Jinsia na Uzazi TAMENET–SRHR nchini,Siyovelwa Hussein akizungumza na waandishi wa habari wa wa Haki na Afya  ya Jinsia na Uzazi TAMENET–SRHR leo jijini Dar  es Salaam.
Mratibu wa Uzazi Salama Kitaifa, Dk. Koheleth Winani akionyesha katiba ya chama hicho kuashiria uzinduzi wa chama cha TAMENET–SRHR leo jijini Dar es Salaam.
Meneja Msaidizi wa mradi wa TMEP ,Eugnia Msasanuri akizungumza na wadau wa Mtandao wa waandishi wa habari wa Haki na Afya  ya Jinsia na Uzazi TAMENET–SRHR jijini Dar es Salaam leo.


Baadhi ya wadau wa Mtandao wa waandishi wa habari wa Haki na Afya  ya Jinsia na Uzazi TAMENET–SRHR.
Wadau wa  Mtandao wa waandishi wa habari wa Haki na Afya  ya Jinsia na Uzazi TAMENET–SRHR wakiwa katika picha ya pamoja. Picha na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.

 Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
SERIKALI imesema kuwa imefikia lengo la nne la millenia ya kupunguza vifo vya watoto chini ya miaka mitano  kwa kufikia vifo 54 kwa kila vizazi hai 1,000.

Hayo ameyasema leo Mratibu wa Uzazi Salama Kitaifa,Dk. Koheleth Winani wakati wa uzinduzi  wa mtandao wa waandishi wa habari wa Haki na Afya  ya  Jinsia na Uzazi TAMENET–SRHR nchini,amesema kuazishwa kwa mtandao kutasaidia kusukuma harakati za kupunguza vifo hivyo.

Amesema anatambua mchango wa waandishi habari  katika mapambano dhidi ya Afya ya Uzazi na ukatili wa kijinsi  pamoja na ukatili dhidi ya watoto.

Dk. Winani katika kuboresha afya ya uzazi ,kutokomeza ukatili wa wa kijinsia  na ukatili dhidi ya watoto katika kupunguza vifo vya vitokanavyo na uzazi  pamoja na  watoto chini ya miaka mitano.

Aidha amesema waandishi katika  kwa kuazisha wametambua majukumu yao katika taifa  katika harakati za masuala ya afya hususani uzazi.

Kaimu Mwenyekiti wa Mtandao huo,Siyovelwa Hussein amesema kuwa kuazishwa kw amtandao huo inatokana na mafunzo mbalimbali pamoja na kujionea hali halisi  katika maeneo ambayo yako nyuma katika masuala ya afya ya uzazi.


Siyovelwa amesema kuzinduliwa kwake na kuaza kufanya kazi katika kuweza kujiimarisha kifedha katika kuelimisha wananchi katika masuala ya afya.

No comments: