Monica Mbega akimwombea kura mgombea ubunge jimbo la Iringa mjini leo |
Monica Mbega akimpongeza Mwakalebela |
Monica Mbega akijiandaa kumsalimia Kiponza. |
Mwenyekiti wa CCM Iringa mjini Bw Abeid Kiponza (kulia) akimtambulisha mgombea ubunge jimbo la Iringa mjini Frederick Mwakalebela leo |
Mwakalebela akizungumza na wana CCM leo. |
Mgombea udiwani wa kata ya Mtwivila Bw Jose Mgongolwa (kulia) akitambulishwa na Mwakalebela. |
Mgombea udiwani Bw Chatanda kulia akitambulishwa na Mwakalebela |
Mwakalebela akimtambulisha Ibrahim Ngwada (kulia) mgombea udiwani kata ya Mshindo |
Mgombea udiwani wa kata ya Mvinjeni akitambulishwa |
Mgombea udiwani wa kata ya Mkimbizi Bi Farida Mpogole akitambulishwa na Mwakalebela |
Mwakalebela akimtambulisha mgombea udiwani wa kata ya Gangilonga Bw Nicholina Lulandala |
Mwakalebela akimtambulisha mgombea udiwani wa Kwakilosa Bw Himid Mbata (kulia) |
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Iringa mjini Bw Abeid Kiponza akimtambulisha mgombea ubunge jimbo la Iringa mjini kupitia CCM Bw Frederick Mwakalebela (kushoto)
Na Matukiodaima BLog.
ALIYEKUWA mmoja kati ya wagombea wa nafasi ya urais kupitia chama cha mapinduzi (CCM) na mbunge wa zamani wa jimbo la Iringa mjini Bi Monica Mbega amesema kuwa mbali ya kuwa yeye alikuwa ni mmoja kati ya walioomba kuteuliwa kuwania nafasi ya urais na jina lake kukatwa bado hana kinyongo na mteuliwa wa CCM Dr John Magufuli kwani anamkubali kwa asilimia 100 kuwa ni chaguo la watanzania kama ilivyo kwa mgombea ubunge wa CCM jimbo la Iringa mjini Bw Frederick Mwakalebela .
Mbega ambae alikuwa ni mbunge wa jimbo la Iringa mjini kwa vipindi viwili kati ya mwaka 2000 -2010 alitoa kauli hiyo leo wakati akizungumza na wanachama wa CCM katika viwanja vya CCM wilaya ya Iringa mjini wakati wa mgombea mteule wa ubunge jimbo hilo la Iringa mjini Bw Mwakalebela kutoka kuchukua fomu kwa msimamizi mkuu wa uchaguzi jimbo la Iringa mjini kwa ajili ya kuwania ubunge kupitia CCM.
Alisema kuwa katika mchakato wa ndani ya chama wa kuwania kuteuliwa kugombea Urais yeye alikuwa ni kati ya wanachama zaidi ya 40 waliojitokeza kuchukua fomu akiwemo Dr. Magufuli na kuwa baada ya vikao vya juu vya chama kukamilisha taratibu za kumpata mgombea mmoja hakuwa na kinyongo cha kuhama chama wala kukaa nyuma katika mambo ya chama na ndio maana ameamua kurejea nyumbani kwake ili kuungana na wana CCM kurejesha jimbo hilo kwa CCM na kuwapigia kampeni wagombea wote wa CCM akiwemo mgombea wa nafasi ya urais Dr Magufuli na madiwani pia.
"Kweli nawapongeza sana wananchi wa Iringa mlinipa udhamini wa kutosha wakati wa mchakato wa kuomba kuteuliwa kuwa mgombea Urais wa CCM nilipata watu 45 kati ya 35 waliokuwa wakihitajika kweli ni watu wengi sana na baada ya mchakato jina langu halikupitishwa na jina la mwenzetu Dr Magufuli ndie aliyeteuliwa na kazi yetu ni kumuunga mkono kwani kati ya watu wote 41 ni nafasi mmoja pekee ndio ilitakiwa ....hivyo hakuna haja ya kuwa na kinyongo kwa kuhama chama chetu "
Mbega aliwataka wana CCM jimbo la Iringa mjini kuweza kuunganisha nguvu zao kwa mgombea ubunge Bw Mwakalebela ili kuweza kulikomboa jimbo hilo na kuhakikisha mgombea Urais na madiwani wa CCM wanapata kura za kishindo zaidi katika jimbo la Iringa mjini .
Alisema kwa wanachama wa CCM ambao waligombea nafasi mbali mbali na kura kutotosha katika nafasi walizoomba wanapaswa kuvunja makundi yao na kuunganisha nguvu zao kwa wale walioshinda ili kufanya kazi ya kujenga chama badala ya mtu .
Hata hivyo alisema kwa upande wake atapambana kwa nguvu zote kuhakikisha chama kinapata ushindi mkubwa katika jimbo hilo la Iringa mjini na kudai kuwa kazi kubwa iliyopo mbele kwa wana CCM ni kujenga utamaduni wa kusamehe na kusonga mbele.
Katibu wa CCM wilaya ya Iringa mjini Elisha Mwampashi akimkaribisha mwenyekiti wa CCM wilaya ya Iringa mjini Bw Abeid Kiponza kumtambulisha rasmi mgombea ubunge wa jimbo hilo ,alisema kuwa ni lazima watanzania na wananchi wa jimbo la Iringa mjini kuwapuuza wale wote wanaohama CCM mara baada ya kushindwa katika kura za maoni na kuwa watu hao hawana mapenzi mema na Taifa bali wapo kwa ajili ya maslahi yao zaidi .
Mwampashi alisema kuwa kinachoshangaza ni kuona UKAWA ambao walikuwa mbele kupinga vitendo vya ufisadi na kumtuhumu wazi wazi waziri mkuu mstaafu Edward Lowasa kuwa si mtu msafi leo wamempokea na kuwa mgombea wao wa nafasi ya urais jambo ambalo watanzania wanapaswa kujiuliza juu ya mwenendo wa UKAWA katika Taifa hili.
Mwenyekiti wa CCM Iringa mjini Bw Kiponza alisema kuwa kazi kubwa ya CCM jimbo la Iringa mjini ni kulikomboa jimbo hilo kutoka kwa aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo mchungaji Peter Msigwa (chadema) ambae hakuna maendeleo yoyote aliyoyaleta katika jimbo hilo kwa kipindi chote cha miaka mitano zaidi ya wana Iringa kusababishiwa kupigwa mabomu na lugha zisizofaa majukwaani .
Hivyo alisema wana Iringa wanayosababu ya kusema basi kuendelea kukosa maendeleo na kufanya maamuzi sahihi ya kukirejesha chama cha mapinduzi madarakani kwa kumchagua mchapa kazi Bw Mwakalebela ambae kwa muda wake mfupi wa ukuu wa wilaya ya wanging'ombe kazi kubwa amepata kuionyesha na hivyo ni zamu ya wana Iringa kushuhudia maendeleo hayo kwa kumchagua kuwa mbunge wa jimbo hilo .
" Toka ameondoka Mbega mwaka 2010 kwa kuanzisha miradi ya barabara na maji ya JR hakuna mradi ulioendelea chini ya ubunge wa Msigwa zaidi ya maandamano na mabomu kila wakati na kupinga wananchi kushiriki katika shughuli za kimaendeleo"
Kwa upande wake mgombea huyo wa ubunge jimbo la Iringa mjini Bw Mwakalebela alisema kuwa chini ya ilani ya CCM serikali imefanikiwa kuleta maendeleo kila kona ya nchi hii na hadi sasa wapo wanaopinga kuwa akili ndogo haiwezi kutawala akili kubwa ila ukweli upo wazi kwa wana Iringa kuona kasi kubwa ya miradi ya maendeleo iliyoletwa na CCM inayoongozwa na wenye akili ndogo kama mbunge wa jimbo hilo anavyojinasibu majukwaani na kuwa haja ya wananchi kumhoji mwenye akili kubwa ni ahadi gani aliyoahidi ambayo amepata kuwatimizia wananchi wake .
Mwakalebela alisema kuwa ni wakati mzuri kwa wana Iringa kupima akili ndogo na kubwa katika maendeleo na sio katika majukwa ya siasa na mwisho wa siku shughuli za maendeleo zinasimama na wananchi kushuhudia maandamano kila uchwao .
Alisema kuwa iwapo wananchi wa Iringa watamchagua kuwa mbunge wa jimbo hilo Octoba 25 mwaka huu wawe na matumaini mapya ya kimaendeleo ikiwa ni pamoja na kuanzisha mfumo mzuri wa kuwakomboa wanawake na vijana kiuchumi kwa kuwapa mikopo nafuu.
No comments:
Post a Comment