Saturday, August 22, 2015

MKURUGENZI MKUU WA AGPAHI AAGANA RASMI NA MKUU WA MKOA WA SHINYANGA

 Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Ally Rufunga (kulia) akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika lisilo la Kiserikali la Ariel Glaser Pediatric AIDS Healthcare Initiative (AGPAHI), Laurean Bwanakunu aliyekwenda kumuaaga ofisini kwake baada ya Rais Jakaya Kikwete kumteua kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD). (Picha na Francis Dande)
 Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Ally Rufunga (katikati) akizungumza na uongozi wa Shirika lisilo la Kiserikali la AGPAHI uliokwenda ofisini kwake wakati Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo alipokwenda kumuaga. 
 Meneja Miradi wa Shirika la AGPAHI kwa Mikoa ya Shinyanga & Simiyu, Dk. Gastor Njau (kushoto) akifafanua jambo.
 Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la AGPAHI anayemaliza muda wake, Laurean Bwanakunu akifafanua jambo.
 Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga akisisitiza jambo.... 
 Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga.
Mkurugenzi Mkuu wa AGPAHI akimsikiliza kwa makini Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Ally Rufunga. 
 Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Ally Rufunga akifafanua jambo wakati uongozi wa Shirika la AGPAHI ulipomtembelea ofisini kwake. 
 Mkurugenzi Mkuu wa AGPAHI anayemaliza muda wake.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la AGPAHI, Laurean Bwanakunu (kushoto) akimkabidhi cheti cha shukrani Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Ally Rufunga, wakati alipokwenda kumuaga ofisini kwake baada ya kuteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD). 
 Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Ally Rufunga akisoma cheti cha shukrani alichokabidhiwa na Mkurugenzi Mkuu wa shirika la AGPAHI anayemaliza muda wake.
Cheti cha shukurani alichokabidhiwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Ally Rufunga (wa pili kulia) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Shirika la AGPAHI. Wa pili kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo anayemaliza muda wake, Meneja Miradi wa Shirika hilo, Dk. Gastor Njau (wa kwanza kushoto) na Mratibu wa Programu ya Mawasiliano na Huduma za Jamii, Jane Shuma (wa kwanza kulia).

Na Mwandishi Wetu, 

Shinyanga


MKUU wa Mkoa wa Shinyanga, Ally Rufunga amesema kasi ya maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi mkoani hapa imepungua kutoka asilimia 9.1 mwaka 2011 hadi asilimia 4.9 mwaka 2014.

Rufunga alisema hayo ofisini kwake wakati akiagana na Mkurugenzi Mkuu wa Ariel Glaser Pediatric Aids Healthcare Initiative (AGPAHI), Laurean Bwanakunu ambaye ameteuliwa na Rais Jakaya Kikwete kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD) hivi karibuni.
Akizungumza mbele ya waandishi wa habari, Rufunga hakusita kupongeza juhudi za shirika hilo katika kuhakikisha linapambana na maambukizi mapya ya VVU ili kufika kwenye ziro tatu.

“Wakati mnaingia Shinyanga mwaka 2011 kasi yetu ilikua kubwa kuliko ile ya kitaifa na hadi kufika Juni,2015 tulifika asilimia 4.1 japo hili halijathibitishwa na Wizara ya Afya ila tumeshafika huko,” alisema mkuu huyo wa mkoa.
Alisema shirika la AGPAHI limejenga vituo bora vya kutolea huduma za tiba na matunzo (CTCs) kwenye vituo vya afya na zahanati mbalimbali mkoani humo na kuahidi kwamba ofisi yake itavitunza na kufanyia ukarabati pale itakapohitajika.

“MSD ndio uhai wetu hasa watanzania wanaoishi vijijini, nakutakia kazi njema… waliokuteua hawakukosea, umefanya kazi nzuri kwa kushirikiana na watumishi wengine wa AGPAHI".

“…Naamini utaendelea kuwa kiongozi bora hata huko uendako, usiogope maneno maana kazi za utumishi wa umma lazima maneno yawepo,” alisema Rufunga huku akisisitiza kwamba wakazi wa Shinyanga wataendelea kushirikiana na shirika hilo na kuenzi kazi wanazofanya.
Akimshukuru kwa ushirikiano, Bwanakunu alisema kazi ya AGPAHI mkoani Shinyanga ilikua rahisi kwa kuwa alipata ushirikiano kutoka kwa Mkuu huyo wa mkoa na watumishi wengine wa idara ya afya.
“Naamini ushirikiano nilioupata kwako utaendelea hata kwa atakayerithi nafasi yangu. AGPAHI tulipoanza kazi, mkoa wa Shinyanga ulikua katika hali mbaya ya maambukizi lakini sasa tunaamini tunaendelea kufanya kazi kubwa ya kupunguza na ikibidi kuondoa kabisa maambukizi,” alisema Bwanakunu kisha kumkabidhi cheti cha shukrani mkuu huyo wa mkoa.

No comments: