Mtaalam
wa Misitu ambae pia anafanya kazi na Mama Misitu kupitia Jumuiko la
Maliasili Tanzania (TNRF), Cassian Sanga akiendesha mjadala wa mada ya
kwanza ya usimamizi endelevu wa rasilimali za misitu nchini.
******************
Na Father Kidevu Blog.
Mtandao wa Jamii wa Usimamizi wa Misitu nchini (MJUMITA) leo imeanza mkutano wake Mkuu wa Siku mbili ambao kwanza umeanza na Warsha ya siku moja ya wadau wote wa mtandao huo. Wajum,be na wadau wa Mjumita kesho Agosti 18, watafanya mkutano mkuu ambapo mambo mbalimbali yatajadiliwa huku Kauli mbiu ya mwaka huu katika Mkutano huo unaofanyika mkoani Morogoro ikiwa ni 'TUCHAGUE VIONGOZI WATAKAO TETEA USIMAMIZI ENDELEVU WA MISITU".
Mtandao wa Jamii wa Usimamizi wa Misitu nchini (MJUMITA) leo imeanza mkutano wake Mkuu wa Siku mbili ambao kwanza umeanza na Warsha ya siku moja ya wadau wote wa mtandao huo. Wajum,be na wadau wa Mjumita kesho Agosti 18, watafanya mkutano mkuu ambapo mambo mbalimbali yatajadiliwa huku Kauli mbiu ya mwaka huu katika Mkutano huo unaofanyika mkoani Morogoro ikiwa ni 'TUCHAGUE VIONGOZI WATAKAO TETEA USIMAMIZI ENDELEVU WA MISITU".
Mtandao
huo umeandaa rasimu maalum ambayo wanakusudia kuigawa kwa wagombea wa
nafasi mbalimbali za uongozi pamoja na kutoa elimu kwa wananchi kuwa
katika mikutano yao ya kampenzi itakayoanza Agosti 22 mwaka huu nchini
kote wananchi wasisite kuwauliza wagombea hao juu ya mstakabali wa
rasilimali za misitu zilizopo katika maeneo yao kwa kuzingatia kuwa
misitu ni uhai kwa maisha ya mwanadamu.
Elias Monga, Meneja mradi wa MJUMITA akifafanua jambo wakati wa warsha hiyo.
Hii ndio kauli mbiu ya Mujumita katika Mkutano wake wa 15 mwaka huu unaofanyika mjini Morogoro.
Mmoja
wa Maafisa Misitu akizungumzia mikakati ya uhifadhi misitu na namna
bajeti Kuu ya Serikali inavyochangia fedha katika uendelezaji na
usimamizi wa Misitu nchini. Maafisa Misitu kutoka Wilaya Mbalimbali
wamealikwa kushiriki katika Warsha hiyo ambapo wamesema licha ya
Halmashauri zao kutenga fungu kwaajili ya uendelezaji Misitu lakini
hakuna fedha zilizoingizwa licha ya baadhi ya Halmashaurti kupata mapato
mengi yatokanayo na misitu.
Mjumbe
wa Bodi ya MJUMITA Kanda ya Mashariki, kutoka Kijiji cha Soga Kibaha
Mkoani Pwani, Subira Juma akizungumza juu ya umuhimu wa kuwachagua
viongozi walio na uwezo wa kutetea usimamizi endelevu wa Mazingira.
Mtoa mada ya ushiriki wa Wananchi katika Uchaguzi Mkuu
utakao fanyika Oktoba 25,2015 Pasience Mlowe kutoka Kituo cha Haki za
Binadamu, akiwasilisha mada hiyo kwa washiriki wa warsha hiyo.
Mjumbe
wa Bodi ya Mjumita Mstaafu, Juliana Mwenda akifafanua jambo kuhusiana
na mkakati huo wa kuwashirikisha wagombea na kuwajengea uwezo wa ufahamu
juu ya umuhimu wa utetezi wa rasilimali za misitu
Baadhi
ya washiriki wakifuatikia warsha hiyo leo ambapo mada mbalimbali
zilitolewa ikiwa ni pamoja na ushiriki wa Wananchi katika uchaguzio Mkuu
2015, Uchaguzi Mkuu na changamoto za wakulima wadogo wadogo na Umuhimu
wa Kiongozi bora katika kuhamasisha matumizi endelevu ya rasilimali za
misitu. SOURCE: Father Kidevu Blog
No comments:
Post a Comment