Tuesday, August 25, 2015

MASHINDANO YA KUTUNISHA MISULI KUFANYIKA AGOSTI 29, 2015 JIJINI DAR

Washindi wa mwaka jana wa Mashindano ya kutunisha misuli (The Most Musicular Man Tanzania 2014) wa kwanza kutoka kushoto ni msindi wa pili, Omary Lyombe, mshindi wa kwanza Mohamed Nouma (katikati) na mshindi wa tatu, Erick Majura wakionyesha utunishaji misuli wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika Gymkana jijini Dar es Salaam leo. Mbele yao (walioketi) ni waandaaji pamoja na wadhamini wa shindano hilo
 Mratibu wa mashindano ya kutunisha misuli, Mohamed Ali akionyesha kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) moja tuzo ya heshima atakayopewa mshindi wa kwanza wa mashindano hayo yatakalofanyika Agosti 29 mwaka huu kwenye ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere mjini Posta.
 Mkurugenzi wa Kampuni ya Torque Tyres, Mohamed Dewji, ambao ni wadhamini wakuu wa mashindano hayo ya kutunisha misuli akizungumza na waandishi wa habari.
 Msemaji wa Shirikisho la Watunisha Misuli Tanzania, Philibert Casmir akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu mashindano hayo yatakalofanyika Agosti 29 mwaka huu kwenye ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere mjini Posta.
 Msemaji Mkuu wa Tanzaned Limited, Carlos Mlinda akitolea ufafanuzi juu ya zawadi zitakazotolewa kwa washindi wa mashindano ya kutunisha misuli yatakalofanyika Agosti 29 mwaka huu kwenye ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere mjini Posta.
Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia maelezo kutoka kwa waandaaji wa mashindano kutunisha misuli yatakalofanyika Agosti 29 mwaka huu kwenye ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere mjini Posta.

Tanzaned Limited kwa kushirikiana na Torque Tyres wanakuletea pambano la mwaka la wanaume watunisha misuli (The Most Musicular Man Tanzania 2015) litakalofanyika Agosti 29 mwaka huu kwenye ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere mjini Posta.

Pambano hilo litawakutanisha wanaume zaidi ya 30 kutoka kila pembe ya Tanzania wenye misuli ili kuonyeshana ubavu na hatimaye kupatikana kwa washindi huku wakisindikizwa na mshindi wa mwaka jana wa kutunisha misuli nchini India na mchekeshaji maarufu Evans Bukuku.

Pambano hilo ambalo hufanyika kila mwaka, mwaka huu linatarajia kuwa na mvuto kutokana na idadi na uwezo wa washiriki kuwa juu na hivyo kujenga mazingira ya ushindani mkubwa.

 “Pambano la mwaka huu ni tofauti kabisa na miaka ya nyuma, mwaka huu tumefanya maandalizi ya kutosha kuanzia kwa washiriki wenyewe, vifaa na burudani zote kwa ujumla, hivyo nawaomba wapenzi na mashabiki wa mchezo huu wafike bila kukosa siku ya pambano” alisema Mratibu wa pambano hilo Mohamed Ali.

 “Mwaka huu kutakuwa na washindi sita, ambapo mshindi wa kwanza atapewa sh 1,500,000, mshindi wa    pili 1,000,000 na mshindi wa tatu 500,000. Washindi watatu katika nafasi ya nne, tano na sita watapata laki moja kila mmoja” alisema Mohamed

Alisema pambano hilo ambalo kiingilio chake kitakuwa ni shilingi 10,000 na shilingi 30,000 kwa VIP, litaanza kuwasha moto tangu saa saa moja na nusu usiku hadi saa usiku.

Waandaji wa pambano hilo wameweka majaji kutoka Tanzania ,Kenya na Uganda ili kuongeza ubora wa pambano hilo ambalo limedhaminiwa na Torque tyres na kuratibiwa Tanzaned, na kuandaliwa na Apex Media Limited.

No comments: