Friday, August 21, 2015

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AZINDUA MPANGO WA KAZI WA KIMATAIFA NA KANUNI ZA SHERIA YA KUZUIA USAFIRISHAJI HARAMU WA BINADAMU.

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizindua Mpangokazi wa Kimataifa na Kanuni za Sheria ya kuzuia usafirishaji haramu wa Binadamu, wakati wa hafla hiyo ya uzinduzi iliyofanyika leo Agosti 21, 2015 kwenye Viwanja vya Karimjee, jijini Dar es Salaam. Kulia ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mathias Chikawe (kulia) ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kimataifa ya kupambana na Usafirishaji Haramu wa Binadamu, Kinemo Kihonamo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Mpangokazi wa Kimataifa na Kanuni za Sheria ya kuzuia usafirishaji haramu wa Binadamu, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mathias Chikawe, baada ya kuzindua rasmi Mpango kazi huo, kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam, leo Agosti 21, 2015. 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mpangokazi wa Kimataifa na Kanuni za Sheria ya kuzuia usafirishaji haramu wa Binadamu, uliyofanyika leo Agosti 21, 2015 kwenye Viwanja vya Karimjee, jijini Dar es Salaam. 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mathias Chikawe, akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kuzindua mpango kazi huo, wakati wa hafla ya uzinduzi iliyofanyika leo Agosti 21, 2015 kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam. 
Baadhi ya Wanafunzi waliohudhuria hafla ya uzinduzi huo wakimsikiliza mgeni rasmi Makamu wa Rais, Dkt. Bilal, wakati akihutubia. 
Baadhi ya Wageni waalikwa waliohudhuria hafla ya uzinduzi huo wakimsikiliza mgeni rasmi Makamu wa Rais, Dkt. Bilal, wakati akihutubia. 
 Baadhi ya Wanafunzi waliohudhuria hafla ya uzinduzi huo wakijisomea vipeperushi walivyogaiwa katika uzinduzi huo.
11 hadi 16:- Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi na wanafunzi waliohudhuria hafla hiyo, baada ya uzinduzi.
Picha na OMR

No comments: