Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Rosalynn Mworia akiongea na waandishi wa habari kuhusiana na utoaji wa semina mbalimbali wanazozifanya kama wadhamini wakuu kwa waendesha badabado wakati wa maadhimisho ya wiki ya Usalama barabaranijijini dar es Salaam yaliyofanyika leo katika Viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar es Salaam, kwa Udhamini wa Vodacom Tanzania,Kulia kwake ni Mwenyekiti wa waendesha bodaboda Wilaya ya Kipolisi Buguruni Kanda ya Tabata, Ramia Mazwela.
Mgeni rasmi wa Uzinduzi wa wiki ya nenda kwa Usalama barabarani Mkoa wa Dar es Salaam,Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleman Kova ( watatu kutoka kulia) akiwa ameambatana na Maofisa wa jeshi hilo kukata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa wiki ya nenda kwa Usalama ikidhaminiwa na Vodacom Tanzania.
Ofisa wa jeshi la polisi Usalama barabarani,Koplo Wilbert Biamungu(kulia)akimwelezea Mgeni rasmi wa uzinduzi wa wiki ya nenda kwa Usalama barabarani Mkoa wa Dar es Salaam,Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleman Kova(kushoto) akimuonyesha ramani ya barabara inavyopaswa kutumiwa na kwa uadilifu na madereva wanaotumia vyombo vya moto wakati huu wa wiki ya nenda kwa Usalama barabarani mkoa wa Dar es Salaam inayodhaminiwa na Vodacom Tanzania.
Mkuu wa kituo Usalama barabarani Mkoa wa Kipolisi-Kinondoni jijini,Solomon Mangamiro(kushoto)pamoja na Ofisa Usalama barabarani Mkoa wa Kinondoni CPL Iyobu Madege(katikati)wakimsikiliza jambo Mkuu wa kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania,Rosalynn Mworia(kulia)wakati wa maadhimisho ya wiki ya nenda kwa Usalama barabarani Mkoa wa Dar es Salaam yanayodhaminiwa na Vodacom Tanzania.
Baadhi ya Maofisa wa Jeshi la Polisi la Usalama barabarani na Magereza wakiwa katika maadhimisho ya wiki ya nenda kwa Usalama barabarani Mkoa wa Dar es Salaam yanayoanza tarehe 24-28 na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania.
No comments:
Post a Comment