Mgeni
Rasmi ambaye ni Afisa Vijana Halmashauri jiji la Mbeya Onah Temu
akitoa hotuba katika siku ya Vijana Duniani ambayo kwa Mkoa wa Mbeya
ilifanyikia Ukumbi wa Chuo kikuu Cha Mzumbe Kampasi ya Mbeya.
Maandamano kuelekea katika Ukumbi ambapo vijana wanakutana kwa ajili ya Sherehe yao
Mratibu wa Mradi wa Restless Fadhiri Mtanga akitoa mada kuhusu Maendeleo ya Vijana
Wakili Stephen John akiwashauri vijana kuto tumika na wanasiasa
Muwezeshaji wa Sherehe hiyo ya Vijana Mwadawa Mbando akiendelea kutoa utaratibu
Mmoja wa vijana kulia akipokea zawadi baada ya kupokea zawadi
William Otuku akitoa Maada kuhusu afya ya Uzazi kwa vijana
Picha ya pamoja
KATIKA
maadhimisho ya siku ya Vijana duniani yaliyofanyika Kimkoa katika ukumbi wa
Chuo kikuu cha Mzumbe Kampasi ya Mbeya, Vijana wamekumbushwa kuhusiana na afya
ya uzazi kwa vijana pamoja na maendeleo yao.
Aidha
katika kongamano hilo ambalo liliandaliwa na mashirika binafsi ya Restless
Developmentna Young & alive initiative ambalo lilihudhuriwa na
Wanafunzi wa Vyuo vya Elimu na shule za Sekondari za Jiji la Mbeya.
Akizungumza
katika kongamano hilo mwakilishi wa Shirika la Young & Alive
Initiative, William Otuku, alisema lengo la maadhimisho hayo ni kuwakumbusha
vijana kuhusiana na maswala yanayohusu afya ya uzazi kwa vijana ili waweze kuwa
na uwezo wa kushiriki shughuli za maendeleo wakiwa salama.
Aliongeza
kuwa kauli mbiu ya siku hiyo ni kuhakikisha vijana wanashirikishwa na
kuhusishwa katika kupanga maamuzi mbali mbali hivyo hayo yote
yanaweza kutimia endapo wataelimishwa kuhusiana na afya ya Uzazi ili
waliomashuleni waendelee kufanya vizuri na kusaidia kutoa elimu kwa ambao
hawako mashuleni.
“Vijana
tunawapa elimuya afya ya uzazi ili waweze kuwa imara katika
kushiriki shughuli za maendeleo za kijamii pamoja na kuwaepusha na vitendo
ambavyo vitaweza kuwaondolea katika hatari ya kupata magonjwa yanayoweza
kuepukika” alisema Otuku.
Kwa
upande wake Mratibu wa Mradi wa Shirika la Restless
Development,Fadhili Mtanga, alisema lengo la kongamano hilo ni kujadiliana kwa
pamoja kuhusiana na changamoto ambazo zinawakabili vijana pamoja na
kubadilishana mawazo juu ya kuweza kutatua na kukabiliana na vikwazo vya
maendeleo kwa vijana.
Alisema
lengo la kuwahusisha wanafunzi ni kutokana na kuwa na kundi kubwa la vijana
wanaoanzia umri kati ya miaka 15 hadi 35 ambao ni kundi kubwa katika jamii
hivyo ni rahisi kwao kupeleka mabadiliko kwa wananchi wengine ambao
hawakubahatika kuhudhuria kongamano hilo.
“Sisi
tumewalenga zaidi vijana ambao ni wanafunzi kwa sababu tunaamini wanakubalika
kaika jamii na nirahisi kwao kutoa elimu ambayo iaweza kuwafikia wahusika kwa haraka
zaidi” alisema Mtanga.
Naye
Mgeni rasmi katika Kongamano hilo, Afisa Vijana wa Jiji la Mbeya, Ona Temu
kutoka Ofisi ya Maendeleo ya Jamii Jiji la Mbeya, alipongeza kwa wadau
kujitokeza na kuandaa kongamano hilo kwa kutambua mchango wa vijana katika
jamii.
Alisema
vijana wanapaswa kuutumia vizuri umri kati ya miaka 18 hadi 40 kwa kujenga na
kutafuta uchumi ili kipindi cha miaka 40 hadi 60 anabaki kuwa msimamizi wa
shughuli ambazo alizifanyia kazi kipindi cha ujana wake.
Aliongeza
kuwa kipindi cha umri wa zaidi ya miaka 60 ni muda wa kufaidi matunda na
kupumzika kwani utakuwa tayari umeshafanya kazi ya kutafuta na kuzisimamia
vizuri kwa malengo makubwa.
No comments:
Post a Comment