Michuano ya
U-17 ya Airtel Rising Stars mkoa wa Dar es Salaam chini ya Chama cha Soka Mkoa
wa Dar es Salaam (DRFA) jana ilimalizika rasmi baada ya kushuhudia Kinondoni
wakiibuka mabingwa kwa upande wa wasichana huku kwa upande wa wavulana Ilala
wakiibuka mabingwa.
Katika
mchezo wa awali ambao ulizikutanisha timu za wasichana wa Temeke na Kinondoni,
Kinondoni walifanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-1. Bao la kwanza la Temeke
lilifungwa katika dakika ya 20 na Maimuna Abasi baada ya kuachia shuti kali na
kutinga moja kwa moja wavuni.
Bao la pili
lilifungwa na Mwantumu Ramadhani dakika ya 30 kutokana na kuunganisha krosi
maridhawa iliyochongwa na Maimuna Abasi na kuzama ndani ya kimia.
Bao la
Temeke lilifungwa na Opa Clement mnamo dakika ya 25 kutokana na kuwatoka mabeki
wa Kinondoni na kumchambua kwa uzuri kipa wa Kinondoni na kuukwamisha mpira
moja kwa moja wavuni.
Mchezo wa
pili ulizikutanisha timu za wavulana za Kinondoni na Temeke na matokeo kuwa, Kinondoni
kuibuka na ushindi wa mabao 2-1.
Temeke
waliandika magoli yao yote mawili kupitia kwa Omari Ali baada ya mara zote
mbili kuwalamba vyenga mabeki wa Temeke na kuukwamisha mpira kimiani huku bao
la kufutia machozi la Temeke likifungwa na Mkomola Yohana dakika ya 80, baada
ya kuunganisha kwa kichwa mpira uliopigwa na nahodha wao Rajabu Jumanne.
Wasichana
wa Kinondoni wameibuka mabingwa kutokana kuwa na pointi 6 baada ya kushinda
michezo yao yote miwili, ikifuatiwa na Ilala yenye pointi tatu huku Temeke
wakiburuza mkia wakiwa hawana pointi.
Kwa upande
wa wavulana Ilala wamefanikiwa kutwaa ubingwa mara baada ya kuwa na pointi nne
sambamba na Kinondoni lakini wakiwa na wastani mzuri wa mabao ya kufunga na
kufungwa, Ilala wakiwa na magoli 3 ya kufungwa na 1 lakufungwa wakati Kinondoni
wakiwa na magoli 3 ya kufungwa mawili huku Temeke wakiburuza mkia baada ya
kupoteza mechi zote mbili.
Baada ya
mchezo kumalizika washindi walipata wasaa wa kuzungumza machache ambapo kwa
upande wa wasichana, nahodha wa Kinondoni Sylvia Mwacha alisema kuwa amejisikia
furaha sana kuwa mabingwa na kutoa pongezi kwa Airtel kutokana na juhudi zao
katika kuinua soka la vijana.
“Shukrani
kwa Airtel ambao wametupa nafasi na sisi wasichana kuonyesha vipaji vyetu, ni
matumaini yangu kuwa wataendelea kufanya hivi kwa siku zijazo pia”, alisema
Mwacha.
Nahodha wa
Ilala, Abdul Hassan alisema: “Juhudi zetu na kupambana ndio vimetuwezesha
kuchukua ubingwa na tunawashukuru sana Airtel kwa sapoti yao bila kusahau TFF
pia, hii ni fursa nzuri kwetu kuweza kujituma ili tufike mbali zaidi”, alisema
Abdul.
Kocha wa
Ilala, Saidi Ambua alisema. “ Mashindano ni mazuri na nashukuru kwa timu ya
yangu kuchukua ubingwa , nawashukuru pia Airtel na TFF kwa kuwezesha michuano
hii, ila ombi langu kwa Airtel na TFF ni kuweza kuvikaratbati viwanja vingine
view angalau kama Karume ili kutoa ffursa kwa vijana kujiendeleza zaidi”,
alisema
Kwa upande
wake Meneja wa Airtel Kanda ya Dar es Salaam Fredrick Mwakitwange alisema kuwa
amefurahishwa kuona vipaji vikubwa sana kwa vijana walioshiriki licha ya umri
wao mdogo.
“Nizipeleke
shukrani zangu kwa Shirikisho Soka nchini (TFF) kwa ushirikiano wanatupatia ili
kuhakikisha mashindano hayo yanaenda vizuri zaidi, na naahidi kuwa sisi kama
Airtel tutaendelea kutoa sapoti kubwa ili kuifanya michuano itoe vipaji vingi
zaidi kwa manufaa ya taifa”, alisema Mwakitwange.
Naye Mwenyekiti
wa Kamati ya Soka la Vijana TFF Ayubu Nyenzi alisema kuwa, anawashukuru kwa
ushirikiano wao katika kukuza vipaji kwa vijana ili kuweza kutimiza ndoto za
vijana wengi.
“Kwa niaba
ya TFF, ningependa kutoa shukrani zangu za dhati kwa Airtel kwa kuendelea
kusapoti vijana kuendesha michuano hii ya Airtel Rising Stars na naamini
ushirikiano huu utazidi kudumu zaidi”, alisema Nyenzi.
Mashindano
ya Airtel Rising Stars ambayo mwaka huu yanashirikisha mikoa ya Ilala,
Kinondoni, Temeke, Morogoro, Mbeya, Mwanza na Arusha inatarajiwa kuingia kwenye
hatu nyeti ya fainali za Taifa iliyopangwa kufanyika kwenye Uwanja wa Karume,
Dar es Salaam, kuanzia Septamba 11 hadi 21 mwaka huu.
Fredrick
Mwakitwange (Right), the Airtel Manager in Dar es Salaam Region, presents Airtel Rising Stars Trophy to Kinondoni girls
skipper Sylvia Mwacha, after winning the the U-17 soccer for girls category in
Dar es Salaam region at Karume Memorial Stadium in Dar es Salaam, yesterday
Fredrick Mwakitwange (Right), the Airtel Manager in Dar es
Salaam Region, presents Airtel Rising
Stars Trophy to Ilala boys skipper Abdul Hassan, after winning the the U-17
soccer for the boys category in Dar es Salaam region at Karume Memorial Stadium
in Dar es Salaam, yesterday.
No comments:
Post a Comment