Wednesday, August 26, 2015

BASATA YAIPONGEZA KAMATI YA MISS UNIVERSE TANZANIA

BASATA yaipongeza Kamati ya Miss Universe Tanzania
Na Mwandishi wetu
Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) limeipongeza kampuni ya Compass Communications Tanzania kwa kufanya mashindano bora ya Miss Universe hapa nchini.

Kauli hiyo imetolewa na  Mratibu wa mashindano ya Miss Universe Fausta Magoti wakati wa kufanya tathimini ya mashindano ya mwaka jana ambapo, Caroline Benard aliibuka mshindi.

Magoti alisema kuwa pamoja na kampuni ya Compass kuanza kushiriki katika mashindano ya Miss Universe mwaka 2007, waliweza kufanya vyema na kuitangaza Tanzania nje ya mipaka yake.

Mbali ya kufanya vizuri katika mashindano ya kimataifa, Magoti alisema kuwa wameridhishwa sana na utendaji wa kamati hiyo kwa kuteua majaji ambao wamekuwa wakiwatangaza washindi ambao ni mfano bora kwa tabia kwa jamii.

“Washindi wenu hawana kashfa katika jamii, mmeendesha mashindano yasiyokuwa na malalamiko, kwa kwa kweli mnahitaji kupongezwa pamoja na kupata changamoto nyingi kutoka kwa wadhamini,” alisema Magoti.

Alitoa wito kwa waandaaji kupanua wigo wa mashindano yao na kuyafanya katika mikoa mingi ili kujitangaza zaidi. “Najua changamoto kubwa ni kuapata wadhamini, tunaomba mjitahidi ili kuyatangaza zaidi mashindano yenu, Basata tumeridhishwa na utendaji wenu, tunataka mfanye bora zaidi ya hapa,” alisema.

Mrembo Flaviana Matata ambaye alimaliza katika hatua ya sita bora katika fainali za mashindano ya mwaka 2007, kwa sasa amekuwa akifanya vyema nje ya nchi katika sekta ya maonyesho ya mavazi au wanaminitindo.

“Ni mashindano bora ambayo kwa kweli yametuvutia sana, tunaomba muongeze bidii ili kuyaboresha zaidi kwani mashindano haya kwa sasa ni makubwa na warembo wengi wanayaulizia jinsi ya kujiunga nayo,” alisema.
Mkurugenzi wa Compass Communications ambaye pia ndiye mwandaaji mkuu wa mashindano haya Maria Sarungi Tsehai aliishukuru Basata kwa usimamiaji bora wa mashindano katika sekta ya sanaa nchini na kusema kuwa watajiathidi kuongeza wigo wa washiriki kaika mashindano ya mwaka huu.

Maria alisema kuwa pamoja na changamoto zote wanazokabiliana nazo, bado wanahitaji msaada kutoka Basata ili kupata wadhamini.
“Basata ni chombo cha serikali, mnaweza kutusaidia kupata wadhamini hata kwa Wizara ya Maliasili na Utalii, sisi tunatangaza jina la nchi na utalii pia, tunaamini kupitia kwenu, tunaweza kupata sapoti kubwa kutoka wizara hiyo, Bodi ya Utalii (TTB) na mamlaka ya zake kama Tanapa.

No comments: