Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli (wakwanza kulia) akipiga makofi mara baada ya kufungua nyumba za makazi ya Watumishi wa Umma zilizoko Mbezi Beach (E-NMC) jijini Dar es Salaam. Wa tatu kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Eng. Mussa Iyombe akifatiwa na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Arch. Elius Mwakalinga.
Nyumba ya Makazi ya Watumishi wa Umma ilioko Mbezi Beach (E-NMC) jijini Dar es Salaam kama linavyoonekana.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Eng. Mussa Iyombe akitoka kufanya ukaguzi wa jengo la Makazi ya Watumishi Sida Flats Kinondoni jijini Dar es Salaam.
SIDA FLATS za Wakala wa Majengo nchini (TBA) kama zinavyoonekana mara baada ya kukamilika.
Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli akikagua sehemu ya jiko katika mojawapo ya nyumba za Wakala wa Majengo nchini TBA.
Sehemu ya Maliwato katika nyumba hizo wa Watumishi.
Waziri wa Ujenzi akipiga ngoma ya kikundi cha Mganda mara baada ya kufanya ukaguzi wa Nyumba za Wakala zilizopo Bunju jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Ujenzi akiwa katika picha ya pamoja na Watumishi wa TBA mara baada ya ukaguzi wa nyumba.
Moja wapo ya Nyumba za Watumishi katika eneo la Bunju B, jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Ujenzi akiagana na Watumishi wa TBA mara baada ya kufanya ukaguzi. Picha zote kwa Hisani ya Kitengo cha Mawasiliano Wizara ya Ujenzi.
Na Lorietha Laurence- Maelezo
Waziri wa ujenzi Mhe. Dkt. John Magufuli amewataka watendaji wa Wakala wa Ujenzi (TBA) kuwapa kipaumbele zaidi watumishi wa umma katika miradi yao ya nyumba za makazi.
Aliyasema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati wa ziara ya ukaguzi wa miradi inayosimamiwa na TBA iliyopo maeneo ya Bunju B na Ada Estate ambapo Waziri, Mhe Magufuli alizindua jengo la EX-NMC lililopo Mbezi beach .
Aidha aliongeza kuwa serikali imefurahishwa na juhudi za TBA katika kuhakikisha kuwa watumishi wa umma wanapata makazi bora na yenye huduma zote za miundo mbinu ikiwemo barabara, maji na umeme.
“Nimefurahishwa na kazi inayofanywa na TBA kwa kweli ni hatua nzuri itakayowasaidia watumishi kupata makazi bora hata watakapostaafu hawatakuwa na msongo wa mawazo kuhusu mahali pa kuishi” alisema Mhe. Magufuli
Naye Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ujenzi (TBA) Elius Mwakalinga ameleeza kuwa mpango wao ni kuhakikisha wanajenga nyumba 10,000 nchini ambapo mpaka sasa wamefanikisha kujenga nyumba 1,816.
“Mpaka sasa tumeweza kujenga nyumba 1,816 ikiwemo hizi za Bunju B ambazo ni jumla ya nyumba 851 zilizogharimu shilingi Bilioni 6 mpaka kukamilika kwake” alisema Bw. Mwakalinga
Pia aliongeza kuwa wamefanikiwa kupata mkopo wa shilingi Milioni 23 kutoka benki ya CRDB ambapo baadhi ya benki kama Benki ya Afrika (BOA) wamehaidi kutoa shilingi milioni 18 wakati Benki ya Uwekezaji (TIB) nayo imeahidi kutoa shilingi Milioni 6 ili kuwezesha ujenzi wa nyumba hizo kukamilika .
Aliongeza kuwa kwa kuishukuru serikali kwa kuiamini kwa kuwapa usimamizi wa mradi wa kukarabati Ikulu ndogo ya Chamwino pamoja na ujenzi wa nyumba 149 zilizo chini ya Tamisemi.
Wakala wa Ujenzi ( TBA ni taasisi ya umma ilianzishwa chini ya sheria ya ujenzi na. 30 ya mwaka 1997 jukumu lake kuu ni kusimamia na kuendesha miliki za serikali ikiwemo viwanja,ofisi na nyumba za watumishi wa umma.
No comments:
Post a Comment