Tuesday, July 21, 2015

VIPAUMBELE VYA MGOMBEA UDIWANI KATA YA MTONI - GODFREY BENJAMIN

MTANGAZA NIA YA UDIWANI GODFREY BENJAMIN KEHOGO.

KERO ZINAZOKABILI KATA YA MTONI
Ø  Huduma hafifu za afya.
Ø  Viwanja vingi vya michezo kuingiliwa.
Ø  Ukusanyaji wa kodi usioridhisha katika masoko na sehemu husika.
Ø  Uchafu ( mitaa na maji taka).
Ø  Miundombinu isiyoridhisha ( barabara, mitaa, majengo ya shule zetu)
Ø  Ajira.
Ø  Ugumu wa upatikanaji mikopo hasa kwa watu wasio na ajira rasmi na dhamana ( vijana na wanawake).
Ø  Kutothamini vipaji haswa za vijana na watoto.
Ø  Ushirikishwaji hafifu wa wananchi katika kupanga mipango ya maendeleo.

MAJIBU YA MASWALI MENGI
Kusimamia mipango yote kwa kufuata mpango mkakati wa kata yetu ambao tutajipangia kutokana na mpango mkakati wa jimbo. Pia kuwa na msimamizi kila mtaa kusimamia utekelezaji wa mipango tuliyojiwekea kama kata. Tatu kuwa na vikao vya kutathimini utekelezaji wa mipango yetu kila baada ya miezi 4. Nne kuteua kamati maalum ya kusimamia mkakati huu na utekelezaji wake. Na taarifa kuwafikia wananchi kujua kile ambacho tumefanikiwa na ambacho bado.
NAMNA YA KUTATUA KERO ZA WANAKATA WA MTONI
Ø  Maeneo ya viwanja vyote vya michezo kuwa huru kama zamani.
Ø  Kusimamia ipasavyo kwa kuweka mfumo wa kisasa wa ukusanyaji wa kodi. 
Ø  Kuwa na siku maalumu ya usafi kila wiki, kuweka mapipa maalum ya takataka kila mwanzo na mwisho wa mtaa, kuweka utaratibu madhubuti wa kulinda eneo la kila mtu kuzuia takataka kutupwa katika eneo lako.

 Sheria kali za usimamizi wa mazingira zitatumika kulinda mazingira yetu. Magari ya kubebea taka ya halimashauri au zabuni yatumike katika zoezi hili. Pia kuanzisha vikundi vyetu vya kukusanya taka kwa malipo maalum, hili litatengeza ajira kwa wale ambao watakuwa tayari.

Ø  Kuzibua mitaro yote kwanza, kutengeneza njia sahihi za kuruhusu maji taka kupita zitakazo elekeza sehumu husika ya kumwaga maji taka hayo. ni lazima kata tuwe na sehemu ambayo maji yote taka yatakuwa na sehemu ya kwenda, haswa maji kipindi cha mvua.

Ø  Kuwa na njia sahihi ya kuvuna maji ya mvua pindi mvua ikinyesha na kuacha maji yakipotea. kutokana na uhitaji wa maji katika kata yetu, ni vyema tukaweka utaratibu wa namna ya kuvuna maji ya bure ya mvua kila mara pindi mvua ikinyesha. 

Ø  Kuweka mkakati wa kuhakikisha vijana wetu wanapatiwa elimu vitendo kwa kutumia vyuo vyetu vya VETA, kuanzisha mafunzo ya muda mfupi kutokana na uhitaji wa swala husika. sababu kubwa ya kushirikisha veta ni kuweza kuwajengea vijana uwezo wa kutengeza vitu kivitendo na sio kinazalia. 

wengi wana elimu ya darasani ambayo haiwezi kuwasaidia kutatua matatizo yao ya kila siku. 

Ø  kuwa na warsha kwa kualika watu mbalimbali kuzungumza kuhusu kubadilisha fikra, kilimo, ujasiriamali na uongezaji thamani wa bidhaa zetu.
Ø  kushirikiana na makampuni mbalimbali katika kupambana na matatizo mbalimbali katika kata yetu kama AFYA, michezo, burudani, elimu na ajira.

Ø  Kufungua tovuti yetu ambayo itaelezea mambo mazuri ambayo yanapatikana mtoni na vivutio tulivyonavyo, vipaji, kazi za sanaa za watu wetu, wamama, biashara zetu na kuwa njia moja wapo ya kujitangaza.
Ø  Kuwa na siku maalum ya maonyesho ya wakazi wa mtoni mara mbili kwa mwaka. Kila kitu kinachopatikana mtoni kitaonyeshwa na watu mbalimbali wataalikwa kuja kuona na kununua bidhaa pamoja na vipaji vyetu.

Ø  Kuwa na semina maalum kwa makundi maalum. Mfano wajasiliamali, michezo na elimu. Hili litawezekana kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo kama vile taasisi na mashirika ya wahisani.

VYANZO VYA MAPATO
Ø  Kuishawishi serikali kuwa sehemu kubwa ya pato linalotokana na kata yetu ibaki katika kusaidia mfuko wa kata wa kuendeleza miradi mbalimbali.
Ø  Kuwa na mfuko maalum wa maendeleo kwa ajili ya makundi maalum katika kata tutatenga asilimia kadhaa kutoka katika mapato
Ø  Kuanzisha ushirikiano na kata zingine zilizopo nje ya wilaya, mkoa na nchi yetu ili kujenga uzoefu na kutanua mawazo yetu katika kuleta maendeleo.
Ø  Kuandika maandiko mbalimbali ya kuomba ufadhili wa miradi mbalimbali ambayo tutabuni sisi kama wana kata ya mtoni; kama miradi gani? upembuzi yakinifu.


WASIFU WA GODFREY BENJAMIN KEHOGO
KUZALIWA:
Mtoni
ELIMU:
Shule ya msingi
Ø  Mtoni
Shule ya sekondari ( Kidato cha I - IV)
Ø  Jitegemee
Shule ya sekondari ( Kidato cha V - VI)
Ø  Azania
Chuo kikuu. Shahada ya kwanza ( Business Administration)
Ø  Tumaini dar es salaam
Chuo kikuu. Shahada ya uzamili ( Masters in Finance)
Ø  Daystar kenya

UZOEFU:
Ø  Mtaalamu wa maswala ya uongozi na usimamizi wa fedha kwa zaidi ya miaka 7
Ø  Mshauri wa maswala ya uwekezaji katika nyanja mbalimbali
Ø  Mtaalam wa muziki, mtungaji, muimbaji na mmiliki wa studio 

SIFA:
Ø  Mchapakazi kwa bidii, mpenda maendeleo, muajibikaji hasa katika kusaidia jamii kuondokana na changamoto mbalimbali
Ø  Jasiri, mvumilivu, msikivu na mpenda watu kulingana na makundi mbalimbali katika jamii
Ø  Ni mtu wa kusimamia maamuzi ya kikao na kuhakikisha yanafanyika
Ø  Ni mtu wa kufuata kanuni na kulinda taratibu za chama.

VIPAUMBELE:
Ø  Kuwashirikisha wananchi katika kupanga mpango wa maendeleo wa Kata na kuisimamia utekelezaji wake pamoja na tathimini yake.
Ø  Kuongeza huduma za afya haswa za wamama na watoto.
Ø  Kuongeza pato la kata kwa kuhakikisha kodi inakusanywa katika vyanzo vyote vinavyohitajika kulipa kodi ipasavyo.
Ø  kuandika maandiko mbalimbali ya miradi kwenda kwa wahisani mbalimbali.
Ø  Kuhakikisha vijana wetu na wakinamama wanapatiwa ELIMU ya vitendo, warsha na semina za kuwajengea uwezo
Ø  Kutangaza bidhaa, vipaji na vivutio vinavyopatikana mtoni kwa wawekezaji wa nje ya kata kwa kupitia maonyesho mbalimbali, vyombo vya habari na mitandao ya kijamiii.

Ø  Kujenga mahusiano mazuri na taasisi mbalimbali za ndani na nje ya nchi kwa ajili ya maendeleo ya jimbo.
Ø  Kuwa na siku maalum kwa ajili ya kutangaza Mtoni yetu na vitu vyetu.
Ø  Kuzishawishi taasisi za fedha kuweza kuwakopesha wanakata kupitia vikundi vyao vya biashara, vicoba na saccos.
Ø  kuziongezea thamani bidhaa zetu kwa kuelimisha wanakata namna ya uongezaji thamani.

MTONI MPYA NI KURA YAKO.
KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI

No comments: