Mkurugenzi
wa Kitengo cha Ubora wa Huduma za Afya Wizara ya Afya na Ustawi wa
Jamii, Dk. Ali Mohamed Ali (kulia), akizungumza katika mkutano na
waandishi wa habari Dar es Salaam leo, wakati akitoa tamko kwa niaba ya
Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dk. Donan Mmbando katika uzinduzi wa kampeni
ya awamu ya pili ya wazazi nipendeni uliofanyika Dar es Salaam. Kutoka
kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Msaidizi Kitengo cha Afya ya Uzazi na Mtoto
Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk.Georgina Msemo na Mshauri wa
Kiufundi wa Malaria kutoka Shirika la Marekani la Maendeleo ya
Kimataifa (USAID)
Ofisa Uzazi Salama, Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk.Heavengton Mshiu (kulia), akizungumza katika uzinduzi huo.
Mshauri
wa Masuala ya Afya ya Uzazi wa Taasisi ya Center for Comminication
Programs Johnns HopKins University, Dk,.Rosemarie Madinda (kulia),
akizungumza katika uzinduzi huo. Taasisi hiyo ndiyo inayoendesha kampeni
hiyo.
Kaimu
Mkurugenzi Msaidizi Kitengo cha Afya ya Uzazi na Mtoto Wizara ya Afya
na Ustawi wa Jamii, Dk.Georgina Msemo (kulia), akizungumza kwenye
uzinduzi huo.
Mwongozaji wa uzinduzi huo akiendelea na kazi.
Wanahabari wakiwa kwenye shughuli hiyo.
Ofisa Uzazi Salama, Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk.Heavengton Mshiu (kushoto), akimpongeza Mkurugenzi
wa Kitengo cha Ubora wa Huduma za Afya Wizara ya Afya na Ustawi wa
Jamii, Dk. Ali Mohamed Ali, baada ya kutoa tamko la Wizara hiyo katika
uzinduzi huo.
Mwanamuziki
Nyoshi Al-Saadat wa Bendi ya Muziki wa Dansi ya FM Academia "Wana wa
Ngwasuma" itakayotoa burudani katika maonyesho mbalimbali yatakayokwenda
sanjari na uzinduzi huo yatakayofanyika kuanzia kesho viwanja vya
Mwembe Yanga Temeke Dar es Salaam kuanzia kesho, akizungumza katika
uzinduzi huo utakaopambwa na burudani za kumwaga.
Na Dotto Mwaibale
SERIKALI
imesema imepiga hatua katika kupunguza vifo vya watoto waliochini ya
miaka mitano toka 157 mwaka 1990 hadi kufikia 54 kwa mwaka 2013.
Hayo
yalibainishwa na Mkurugenzi wa Kitengo cha Ubora wa Huduma za Afya
Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Ali Mohamed Ali wakati akitoa
tamko kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dk. Donan Mmbando katika
uzinduzi wa kampeni ya awamu ya pili ya wazazi nipendeni uliofanyika Dar
es Salaam leo
Alisema
kati yua watoto hai 1,000 wanaozaliwa na kufikia lengo la Melenia (MDG)
4 waliojiwekea kufikia mwisho wa mwaka huu Disemba 2015.
"Pamoja
na mafanikio hayo bado hari si shwari kwa upande wa vifo vinavyotokana
na uzazi kwani vimepungua kutoka 770 mwaka 1990 na kufikia 410 kwa mwaka
2014 kwa kila vizazi hai 100,000 tofauti na lengo tulilojiwekea kufikia
Disema 2015 kuwa vipungue kufikia 193 kwa kila vizazi hai 100,000"
alisema Dk.Ali.
Alisema
Kampeni ya Wazazi Nipendeni awamu ya kwanza ilitengenezwa na Serikali
ya Tanzania kupitia Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kwa kushirikiana
na msaada toka watu wa Marekani kupitia taasisi ya USAID, Mfuko wa
Malaria wa Rais wa Marekani na taasisi ya Kukinga na kuzuia Magonjwa.
Dk.
Ali alisema programu hiyo ilihusisha kutuma ujumbe uliolenga kuimarisha
afya ya mjamzito na mtoto na kuwa ilizinduliwa hapa nchini jijini
Mwanza kwa mara ya kwanza mwezi Novemba, 2012.
Alisema
katika kampeni hiyo ya masuala ya afya na ustawi wa jamii vyombo vyote
vya habari ni muhimu zaidi kuhabarisha na kuwa ujumbe mfupi wa simu za
kiganjani wenye taarifa anwai zitakuwa zinatumwa wakati wowote wa
ujauzito mpaka mwaka mmoja baada ya kujifungua.
Aliongeza
kuwa ili kujiunga mhusika, ndugu, jirani au rafiki atatuma ujumbe
"mtoto" kwenda namba 15001 jambo litakalosaidia kupunguza vifo
vitokanavyo na uzazi, mtoto mchanga na mtoto alie chini ya miaka mitano.
Alisema
uzinduzi wa kampeni hiyo unakwenda sanjari na maonyesho mbalimbali,
upimaji wa damu, masuala ya huduma ya VVU na Ukimwi yatakayoanza leo
asubuhi viwanja vya Mwembe Yanga Temeke jijini Dar es Salaam.
Dk.
Ali alitumia fursa hiyo kuwakaribisha wananchi wa mkoa wa Dar es Salaam
na mingine hasa wanaume na wanawake kufika kwenye maonyesho hayo kupata
huduma za afya ya uzazi ambayo yataambatana na burudani za muziki
kutoka bendi za Wanaume Familia, Ngwasuma, Wanaume Halisi na nyingine
nyingi.
(Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com.
No comments:
Post a Comment