Diwani
wa Kata ya Vituka, Kenny Makinda (kulia), akisaidia kumtwisha ndoo ya
maji Mwajuma Mikorota wakati wa hafla ya Kampuni ya Bia Tanzania (TBL),
ya kukabidhi kisima cha maji katika eneo la Nasizi, Vituka kwa Limboa,
Temeke, Dar es Salaam juzi.Kushoto ni Ofisa Uhusiano wa TBL, Doris
Malulu.
Ofisa
Uhusiano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Doris Malulu (katikati),
akisaidia kumtwisha ndoo ya maji Haisha Juma wakati wa hafla ya TBL,
ya kukabidhi kisima cha maji katika eneo la Nasizi, Vituka kwa Limboa,
Temeke, Dar es Salaam juzi.Kushoto ni Ali Limboa ambaye ni wa eneo la
Limboa.
Akina
mama wakazi wa eneo la Kwa Limboa, Temeke,Dar es Salaam, wakiteka maji
baada ya Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), kukabidhi kisima cha maji
kilichojengwa na kampuni hiyo katika Nasizi, Vituka, wilayani Temeke.
Hafla hiyo ya makabidhiano ilifanyika
Mkurugenzi
Mtendaji wa wa Kampuni ya Mo Resources Ltd, Onesmo Sigalla iliyojenga
kisima hicho, akimuonesha Ofisa Uhusiano wa TBL, Dorris Malulu ramani
ya kisima hicho.
Ofisa
Uhusiano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Doris Malulu (kushoto) na
Diwani wa Kata ya Vituka, Kenny Makinda wakifungulia maji kwenye bomba
wakati wa hafla ya TBL kukabidhi msaada wa kisima katika Serikali ya
Mtaa wa Vituka kwa Limboa, Temeke, Dar es Salaam
Mama
mkazi wa Yombo Vituka akifurahia baada ya kuteka maji katika kisima
hicho. Kushoto ni Dorris Malulu wa TBL aliyekabidhi kisima hicho.
Ofisa
Mtendaji wa Mtaa wa Yombo Vituka, Mary Jailos akimshukuru Ofisa
Uhusiano wa Kampuni ya Bia Tanzania TBL, kwa msaada wa ujenzi wa kisima
uliotolewa na kampuni hiyo kwa wananchi wa mtaa huo.
No comments:
Post a Comment