Monday, July 20, 2015

SIMU TV: HABARI KATIKA TELEVISHENI LEO

SIMUTV: Licha chupa kuonekana ni taka baada ya matumizi lakini kinyume chake katika baadhi ya maeneo zimeonekana kuwa chanzo cha ajira baada ya kutumika kama mali ghafi kwa bidhaa zingine

SIMUTV: Soko la hisa la Dar es salaam lakamilisha shindano lake la DSE lililolenga kuwajengea wanavyuo utamaduni wa kuweka akiba na kuwekeza kupitia soko la hisa la Dar es salaam.

 SIMUTV: Baadhi ya jamii nchini zaelezwa kutumia fedha nyingi katika sherehe badala ya kuwekeza katika elimu  jambo linalopelekea kudorora kwa maendeleo
  
SIMUTV: Chama cha mapinduzi wilaya ya Kigoma vijijini chaazimia kutowapitisha na kuwafuta wagombea watakao kiuka maadili maelezo na kanuni za chama.

 SIMUTV: Benki ya ushirika Kilimanajaro KCBL yaazimia kutoa mikopo kwa vyama vya ushirika ili kuweza kufufua uzalishaji zao la kahawa na kuinua kipato cha wakulima.
  
SIMUTV: Mkoa wa Dodoma umefanikiwa kuvuka lengo la uandikishaji wapiga kura huku zoezi hilo likiwa limekamilika kwa asilimia 109.6.

 SIMUTV: Vijana 18 wa kitanzania wakabidhiwa hundi ya mil.364 kwa lengo la kusaidia mawazo  ambayo yataleta mabadiliko nchini.
  
SIMUTV: Idadi kubwa ya Wanahabari waelezwa kujiingiza kwenye siasa huku wakongwe kama Lowassa na wengine wakiamua kutogombea tena.
  
SIMUTV: Wananchi wa wilaya ya Ludewa waipongeza serikali kwa kuwaboreshea huduma katika sekta za afya,umeme na miundombinu.
  
SIMUTV:Rais Kikwete asema kua njia pekee na ya uhakika ya kuondokana na ufugaji wa zamani ni kutumia teknolojia ya uhamilishaji. http://youtu.be/G1VbF9ug7vc   
  
SIMUTV:Mwenyekiti wa UDP Taifa John Cheyo asema chama hicho hakitosimamisha mgombea urais bali kitaunga mkono mgombea atakaye kidhi haja ya watanzania.
  
SIMUTV: Jeshi la polisi kupitia kikosi chake cha usalama barabarani latarajia kuendesha zoezi la upimaji afya kwa madereva wa masafa marefu.
  
SIMUTV: Wananchi wa wilaya ya Ludewa waipongeza serikali kwa kuwaboreshea huduma mbalimbali za kijamii zikiwemo sekta za afya,umeme na miundombinu.

No comments: