RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein ( Pichani) amesema kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
imeandaa mipango na sera nzuri za kuwasaidia vijana ili waweze kujiajiri
wenyewe hasa waliojiunga katika vikundi vya ushirika na SACCOS.
Dk. Shein alisema
kuwa Serikali imeanzisha Mfuko wa kuwawezesha Wananchi Kiuchumi na tayari watu
kadhaa wameanza kufaidika na Mfuko huo sambamba na kuwapatia mafunzo ya
kitaalamu pamoja na kuvipatia vikundi vya ushirika mbinu za kupata masoko na
kuwawezesha kuwa wajasiriamali wazuri.
Akisoma hotuba
kwa niaba ya Dk. Shein Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Idara
Maalum, Mhe. Haji Omar Kheir, aliyasema hayo leo katika uzinduzi wa Jumuiya ya
Watazania Wasio na Ajira (TUEPO) huko katika ukumbi wa afisi za Jumuiya hiyo
Rahaleo, mjini Zanzibar.
Aidha, Dk. Shein
alisema kuwa katika kuwasaidia vijana walioshindwa kuendelea na masomo yao,
Serikali imeyaimarisha mafunzo ya elimu ya amali katika vituo vya amali vya
Mwanakwerekwe na Mkokotoni Unguja na Vitongozi huko Pemba.
Dk. Shein alisema
kuwa kituo cha kuwaandaa wajasiriamali katika Taasisi ya Sayansi na Teknolojia
ya Karume imeshaanza kutoa mafunzo ya ujasiriamali na kupatiwa mikopo.
Alisema kuwa
katika vyuo hivyo vijana hufunzwa ujuzi wa kazi mbali mbali kama vile ufundi
umeme, ufundi magari, useremala, uhunzi, kutegengeneza mafriji na amali
nyengine ambapo tayari vijana wengi wameweza kunufaika na kujiajiri wenyewe.
Aidha, aliwaeleza
vijana hao kuwa mafunzo wanayotoa katika taasisi yao na taasisi nyengine
binafsi ni kuongeza fursa za mafunzo ya elimu ya amali kwa vijana ili waweze
kukabiliana na tatizo la ajira kwa vijana.
Dk. Shein alisema
kuwa ukosefu wa ajira nji tatizo linalozikabili nchi zote duniani hivyo,
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapindyuzi ya
Zanzibar zimekuwa zikichukua jitihada mbali mbali katika kukabiliana na tatizo
hilo kwa kushirikiana na jumuiya za Kimataifa, sekta binafsi na jumuiya hiyo ya
TUEPO.
“Hivyo kuwepo
kwenu hapa ni hatua ya juhudi za pamoja ambapo Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar wakati wote huwa inazishajihisha katika kukabiliana na tatizo la ajira
hasa klwa vijana wetu”,alisema Dk. Shein.
Aidha, Dk. Shein
alisema kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inatambua ukubwa wa tatizo la
ajira kwa vijana kutokana na uchache wa fursa za ajira serikalini na kuwepo kwa
ongezeko la vijana wanaomaliza masomo katika ngazi mbali mbnali kwa kila mwaka
na kutegemea ajira ziliopo.
Alisema kuwa
inatia moyo kuona hivi sasa, vijana wengi wasomi wameanza kushajihishana
kuanzisha vikundi vya ushirika na kujiajiri wenyewe bila ya kuendelea kusubiri
ajira Serikalinini.
Dk. Shein aliwanasihi
vijana hao kuhakikisha kuwa mafunzo wanayotoa yazingatie ubora na hali ya
mahitaji ya soko la ajira sambamba na kuhakikisha kuwa wanashirikiana na
Taasisi mbali mbali za Serikali kama vile Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali
yenye dhamana ya kuhakikisha ubora wa elimu inayotolewa kwa wananchi.
“Serikali itaendelea kushirikiana na Jumuiya
hii na taasisi zote zinazounga mkono mipango na jitihada mbali mbali za
Serikali katika kuleta maendeleo na Ustawi wa wananchi wetu”,alisema Dk. Shein.
Pia, Dk. Shein
alitumia fursa hiyo kutoa wito kwa wananchi kuzitumia vyema fursa
zilizoandaliwa na Serikali pamoja na Taasisi binafsi katika kuwawezesha katika
kukabiliana na tatizo la ajira hapa nchini.
Nae Mwenyekiti wa
Jumuiya ya Watanzania Wasio na Ajira
(TUEPO) Ussi Said Suleiman alisema kuwa lengo la Jumuiya hiyo ni kuwandaa
vijana kielimu kwa kufundisha fani mbali mbali pamoja na kuwatafutia fani mbali
mbali ndani na nje ya nchi, ili kuondosha tatizo la ajira.
Mwenyekiti huyo,
alisema kuwa jumuiya inashirikiana na itashirikiana na taasisi za Serikali na
zisizo za Serikali katika kupunguza tatizo la ajira nchini ambapo tayari
imeanisha chuo cha Tanzania star teachers college kwa lengo lam kwuasaidia
wanachama wa jumuiya hiyo.
Aidha, Mwenyekiti
huyo alitumia fursa hiyo kueleza mafanikio ya Jumuiya hiyo pamoja na changamoto
zilizopo, ambapo Waziri Kheir alichangia Tsh. milioni mbili kwa upande wake
akiwa kama Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Idara Maalum.
Jumuiya hiyo
imeenzishwa tarehe 23.4.2015 ikiwa na wanachama watano ambapo hadi sasa ina
wanachama 210 .
No comments:
Post a Comment