Tuesday, July 7, 2015

MBUNGE GODFREY MGIMWA ; NILIAHIDI KUWATUMIKIA WANANCHI WA KALENGA NIMEFANIKIWA KWA ASILIMIA 99 NDANI YA MWAKA MMOJA PEKEE

mbunge  Mgimwa akitimiza ahadi yake  ya bati 50 kwa kituo cha yatima  Tosamaganga
Mbunge Mgimwa katikati  akitazama nguzo  za umeme katika kata ya Mgama 


 Mbunge Mgimwa akiwa katika usafiri wa Baiskeli  wakati wa ziara ya  kutembelea  wananchi wake kushukuru

WAKATI   wabunge wakiwa  mbioni kumaliza muda wao   mbunge wa   jimbo la  Kalenga Bw Godfrey Mgimwa amesema kuwa kwa  kipindi chake cha mwaka mmoja kama  mbunge wa   jimbo hilo la Kalenga amesema anamshukuru Mungu katika  safari yake ya  kuwatumikia wananchi  wa  jimbo la Kalenga kwa kufanikisha  kutekeleza ahadi  zake kwa asilimia 99.9 ndani ya  mwaka mmoja .

Huku  akiwaomba  wananchi  wa  jimbo hilo la Kalenga  kuweza kumpima kwa kazi  alizozifanya kwa mwaka  mmmoja na zile zilizofanywa na wabunge waliotangulia katika  jimbo hilo na  wabunge  wa upinzani kwa  kipindi cha miaka  mitano walioongoza majimbo yao.

Bw Mgimwa  aliyasema  haya  jana   wakati akieleza  utekelezaji  wa ilani ya  CCM na ahadi  mbali  mbali zilizoahidi  mbunge aliyetangulia Marehemu Dr Wiliam Mgimwa kwa kila kata kati ya kata 13 za jimbo la Kalenga .

Alisema  kuwa katika  kata ya Kiwere ahadi  ambazo amezitekeleza ni pamoja na  mradi wa umeme vijiji vya Mgera ,kitapilimwa,Mfyome ambao unaendelea pia Mradi wa Maji, Mfyome na kiwere unaendelea,Bati 80 shule ya msingi Kiwere,Bati 50 Itagutwa,vikundi vya vicoba kata ya kirewe vimepewa Tsh milioni 3,ujenzi wa maabara shule ya sekondari Kiwere amechangia milioni 2 ujenzi wa bweni sekondari ya Kiwere amechangia Tsh milioni 1

kata  ya Nzihi  katika shule ya Dintyus sekondari amechangia Tsh milioni 2,saruji mifuko 100,Tsh milioni 2 ujenzi wa maabara shule ya sekondari Kidamali na mifuko 50 ya saruji, Tsh 400,000 kwa timu ya daraja la tatu ngazi ya Mkoa wakati  kata ya Ulanda Shule ya msingi Lukwambe Bati 100, ujenzi wao kituo cha afya Mlangali mchango wa Tsh 250,000,mradi wa maji kijiji cha Mwambao,kijiji cha Weru ,mradi wa umeme Kijiji cha Ibangamoyo ,Kibebe na Weru
Mchango wa Tsh milioni 2 ujenzi wa maabara Shule ya sekondari Kalenga
Mbunge  Mgimwa alisema kwa kata ya Kalenga  kwa  shule ya  msingi amechangia Tsh 660,000 kwa ajili ya ujenzi wa vyoo vya wanafunzi,Bati 50 na mabelu ya nguo za yatima Tosamaganga vyote vikiwa na thamani ya Tsh milioni 3.5 pia amechangia Tsh milioni 2 ujenzi wa maabara Sekondari ya Lipuli ,mifuko 50 ya Saruji,Vicoba kijiji cha kalenga Tsh 500,000 pamoja na vifaa vya michezo kwa vijana.
Huku kata  ya Mseke katika  shule ya  msingi Ugwachanya Bati 60 , shule ya msingi Sadani Bati 60 na saruji 50 na Tsh milioni 1, shule ya msingi Makota Bati 50 Mseke sekondari Tsh milioni 2 ujenzi wa maabara,kikundi cha Sliki Tanangozi Tsh 700,000
Mradi wa umeme kijiji cha Wenda unaendelea wakati kata  ya Luhota kwa  upande wa Shule ya msingi Wangama Bati 50 na saruji 50, kikundi cha siliki Tagamenda Tsh 500,000 na Luhota sekondari Tsh milioni 2 kwa ajili ya ujenzi wa maabara

Alitaja  kata  nyingine  ambazo amechangia  kuwa ni Magulilwa kwa shule ya msingi Nega B Bati 100,kijiji cha Mranda Bati 80, mradi wa umeme Nega B na Magulilwa unaendelea, shule ya msingi Ng'enza Saruji mifuko 50 ,Visiwa viwili vya maji na shule ya sekondari Muwana Tsh milioni 2 ujenzi wa maabara na kata ya Lyamgungwe Kijiji cha Malagosi Bati 80 za ujenzi wa zahanati,kijiji cha Lupembelyasenga saruji 50 , mradi wa umeme Wenda,Kikombwe,Ismila na maji kijiji cha Kikombwe unaendelea
Kuchangia Tsh milioni 2 ujenzi wa maabara shule ya sekondari Ismila

Pia kata ya  Mgama kwenye shule ya  msingi Mgama Bati 100 na Tsh milioni 2 kwa ajili ya ujenzi wa maabara, shule ya msingi Ibumila Bati 50 na saruji 50 ,shule ya msingi Itwaga saruji 20, shule ya msingi Luhato madawati 30 na mradi wa umeme kijiji cha Mgama unaendelea na kata ya Ifunda amechangia
Shule ya msingi Mibikimitali Bati 50, Shule ya msingi Udumuka saruji 100,kijiji cha Mfukulembe Bati 50 ,shule ya sekondari Lyandembela milioni 2 ujenzi wa maabara na Shule ya sekondari Lyasa Tsh milioni 2


Bw  Mgimwa alisema  kuwa kwa kata   Lumuli ,kijiji cha Isupilo Bati Bati 50 ,kijiji cha Muwimbi Bati 80 ,Lumuli sekondari Tsh milioni 2 ujenzi wa Maabara,mradi wa umeme Isupilo,Itengulinyi,mradi wa maji Isupilo ,Itengulinyi na Lumuli inaendelea pia kivuko cha barabara ya Itengulinyi - Magunga kimekamilika wakati kata ya Wasa ,Shule ya msingi Usengelendeti Bati 100,Mahanzi Bati 80,WASA sekondari Tsh milioni 2 ujenzi wa maabara,mradi wa umeme unaendelea

Alitaja  utekelezaji wa ahadi alioufanya pia kata  ya Maboga  katika Shule ya msingi chamgogo Bati 50 , Shule ya msingi Kidilo bati 50, Shule ya sekondari Kiponzero Milioni 2 ujenzi wa maabara , barabara ya Magunga - Makota umekamilika,shule ya msingi Makombe saruji mifuko 50 pia mradi wa umeme Kiponzero unaendelea.

Mbunge  huyo  alisema  kuwa jimbo la Kalenga kuna jumla ya kata 13 ila sasa ni kata 15 ambazo zimetokana na kata mpya na kuwa  kiasi cha zaidi ya  Tsh  milioni 110 amepata  kuzitumia kutimiza ahadi  zake kwa kipindi chake cha mwaka  mmoja pekee aliopata  kuwepo madakarani

Hata  hivyo  alitaja ahadi ambazo bado  kuzitimiza na atazitimiza  wakati  wowote kabla ya kumaliza  muda  wake  kuwa ni  ahadi ya Tsh milioni 1 kwa ajili ya Vicoba Ifunda  kibaoni ,bati 100 kwa ajili ya kuchangia ujenzi shule ya wasichana Ifunda ,ahadi ya Tsh milioni 1  kwa ajili ya ununuzi  wa vyombo vya muziki katika  Kanisa la Lutherani Ifunda kibaoni na ahadi ya  mwisho ni ya bati 60 kwa ajili ya shule ya  sekondari Lyandembela
Hivyo  aliwataka  wananchi  wa  jimbo la Kalenga  kuendelea kuwa na imani  zaidi kwani amefanikiwa  kutimiza ahadi zilizonyingi ambazo amepata  kuzitoa kwa  muda wa  mwaka  mmoja  pekee  na kuwa  iwapo  watamchangua tena basi  wawe  na imani ya   kupata maendeleo  makubwa  zaidi ya haya .
" Naomba  wananchi  wa Kalenga  niwahakikishie  kuwa nitagombea  tena  Ubunge kwa mwaka  huu  ili  niweze kupata miaka  yangu mitano ya  kushirikiana nanyi katika  kuleta maendeleo "

No comments: