OUR REF NO: KISSC/GC/02/07 03/07/2015
TAARIFA KWA VYOMBO VYA
HABARI
Klabu
ya Kimondo Super Sports inayoshiriki ligi daraja la kwanza Tanzania yenye
maskani yake wilayani Mbozi inapenda kutoa tamko juu ya mkanganganyiko wa
taarifa za kuptosha za usajili wa mchezaji wake Geofrey Bahati Mwashiuya.
Klabu
inasikitishwa saana na habari/taarifa zenye mkanganyiko zinazotolewa na msemaji
wa timu ya Yanga,Katibu wa timu ya Yanga na mchezaji wetu Geofrey Mwashiuya
katika vyombo mbalimbali vya habari;
Jerry
Muro alisikika katika vyombo vya habari akijinadi kuwa klabu ya soka ya Yanga
imemsajili Geofrey Mwashiuya tangu Oktoba,2014 kwa kandarasi ya miaka
mitatu,wakati huohuo Katibu wa Yanga Dkt,Jonas Tiboroha alidai mchezaji huyu
alisajiliwa na klabu ya Yanga tangu mwezi Februari,2015.
Klabu
ya KIMONDO inasikitishwa na taarifa hizi zenye mkanganyiko mkubwa kuhusu suala
la mchezaji huyu,na kwa kauli hizo mbili zinazokinzana Watanzania wanaweza
kuona ukweli wa mambo ukoje.
Taarifa
sahihi ni kwamba mchezaji Geofrey Mwashiuya ana mkataba wa miaka minne na timu
yetu ya KIMONDO na ndio muda sahihi
ulioandikwa katika TMS na uliopo katika mkataba wa maandishi. Zaidi klabu ya
KIMONDO inasikitishwa na taarifa hizi za upotoshwaji zinazofanywa na YANGA kwa
makusudi kabisa kuwa mchezaji wetu hana mkataba na sisi,
Pia
maneno ya mchezaji akijaribu kuudanganya umma wa Watanzania na wapenda soka
kuwa alipewa kijikaratasi tu cha kujaza,alipokwenda TFF na Uongozi wa YANGA
wakaarifiwa kuwa hiyo ni fomu ya uthibitisho wa mchezaji. Zaidi wanadai kuwa
TFF iliwaambia kuwa mchezaji wa daraja la kwanza mara ifikapo mwisho wa
msimu/ligi basi na mkataba wa mchezaji unakuwa umekwisha.
Pia klabu ya KIMONDO ilisikia maneno hayo
yaliyotamkwa na mchezaji yakiungwa mkono na katibu wa YANGA katika kipindi cha
michezo cha anga la michezo cha Ebony Fm na mitandao ya kijamii siku ya
jumatatu tarehe 29,June,2015 akijinasibu kuwa kwa uelewa wake ligi daraja la
kwanza haina mikataba na mchezaji huwa huru mara ligi inapomalizika.Kwa msingi
huo wanatambua kuwa ligi daraja la kwanza wachezaji wake wanakuwa na mikataba
,kama sivyo ni sababu zipi zilizowapelekea wao kudai kutuandikia barua sisi ya
kutaka ufafanuzi wa mikataba ya wachezaji wetu na zaidi kwenda TFF?
Klabu ya KIMONDO inahoji juu ya utaratibu
huu,ni kwa namna gani mkataba uishe mara tu ligi inapokwisha? Na ni nini maana
ya matumizi ya TMS kwa timu za VPL na FDL? Na ni kwanini katika utaratibu wa
kutumia TMS kuna kipengele cha kuandika muda wa mkataba wa mchezaji na sio
fixed time ya mwaka mmoja kama inavyodaiwa kwa timu za daraja la kwanza kama
linavyozungumzwa na viongozi wa Yanga? Klabu ya KIMONDO inahoji ni kanuni ipi
inayotumika/iliyotumika katika hili?
Kwa
suala hili, Timu ya Kimondo isingependa kuona TFF ikipakwa matope kuwa
ilishiriki kutoa go-ahead kwa timu ya Yanga kwa kigezo kuwa mchezaji wa ligi
daraja la kwanza hawana mikataba, na usajiri wao huishia msimu unapomalizika.
Tunaamini kuwa haya ni maelezo yaliyotolewa na uongozi wa Yanga kwa lengo la
kutetea maslahi yao.
Kuhusiana
na madai yanayotolewa na klabu ya YANGA kuwa klabu ya KIMONDO ilikuwa wapi
tangu muda wote huo hadi kuja kuibuka na kudai kuwa mchezaji Geofrey Mwashiuya
ni mali mara baada ya kung’ara katika mechi dhidi ya klabu ya Villa ya kutoka
Uganda katika uwanja wa Taifa?
Klabu
ya KIMONDO inaona hoja iliyotolewa na klabu ya YANGA ni dhaifu na haina mashiko
kwakuwa klabu ya KIMONDO isingeweza kukurupuka pasi na ushahidi wowote kuwa
klabu ya YANGA imemsajili mchezaji wetu zaidi ya hapo mwanzo kusikia tu kama
tetesi katika vyombo vya habari. Kwa kutumia vyombo hivyohivyo vya habari klabu
ya KIMONDO ilitoa angalizo dhidi ya timu zote zinazohitaji huduma ya mchezaji
huyu zifuate utaratibu unaokubalika ka kuwasiliana na klabu yetu.
Katibu
wa Yanga alienda mbali kwa kusema kwamba ,aliandika barua mwezi wanne kutaka
kujua status za mchezaji Geofrey Mwashiuya na Mateo Danny Silavwe lakini hadi
sasa hakupata majibu. Klabu inahoji kama alijua mchezaji mara ligi iishapo na
mkataba unakwisha je alikuwa anaandika barua kutaka kujua endapo Geofrey ana
mkataba na KIMONDO katika muktadha upi?na je hiyo barua alimwandikia nani,na nani alipokea?Katika hili mnaweza
kupima maelezo ya klabu ya YANGA dhidi yetu.
Uongozi
wa KIMONDO unazidi kusisitiza kuwa mchezaji huyu ana mkataba nasi wa miaka
minne na tunawashauri YANGA wafuate utaratibu unaotakiwa katika usajili na si
vinginevyo.
Kama
ni kweli walimsajili katika dirisha dogo mwezi Oktoba basi kuna shida kubwa hapa,kwakuwa klabu ya
KIMONDO ilimsajili mchezaji huyu mwezi wa nane tarehe 31,2014.Au kama ni kweli
walimsajili mwezi wa pili,2015 ilhali KIMONDO ilimsajili mwezi wa nane tarehe
31 basi kuna ukiukwaji mkubwa wa sheria za FIFA juu ya uhamisho/usajili wa
wachezaji.Kwakuwa sheria zinasema mchezaji ataruhusiwa kufanya mazungumzo na
klabu yoyote akiwa amebakiza miezi sita ya kumalizika kwa mkataba wake. Kwa
mtizamo wao kuwa mchezaji wa FDL husajiliwa kwa mkataba wa mwaka mmoja
mmoja.Izingatiwe kwamba kundi A ambalo klabu ya KIMONDO ilikuwepo mchezo namba
moja ulikuwa dhidi ya KIMONDO na VILLA
SQUAD ulichezwa tarehe 11/10/2014 katika uwanja wa CCM –VWAWA MBEYA,mchezaji
huyo alicheza akiwa amevalia jezi namba 22. Zaidi alicheza michezo yote
mfululizo ya raundi ya kwanza hadi tarehe 20/11/2014.
Swali
la kujiuliza,kama kweli mchezaji huyu alikuwa anaishi jangwani kuanzia mwezi
Oktoba ,alikuwa anatokea Jangwani kwenda kucheza mechi za KIMONDO au alikuwa
anacheza kwa mkopo?Tulitafakari hili kwa pamoja.Juu ya hili kumbukumbu zilizopo
katika klabu yetu,Bodi ya Ligi na TFF zinaonyesha mchezaji huyu amecheza mchezo
namba 129 wa tarehe 13/02/2015 kati ya KIMONDO dhidi ya MAJIMAJI FC ya Songea
akiwa amevalia jezi namba 22.
Pamoja
na hilo mchezaji huyu mwezi wa tatu mwaka huu amecheza katika ligi ya MSYETE
CUP akichezea timu ya ISANSA BOYS FC
wakicheza na MPITO FC. Mwezi wan ne mwaka huu alikuwa akishiriki katika
ligi ya JABU CUP hapo MPEMBA Katika viwanja vya Shule Ya Msingi Katete akiwa na
timu ya NANSERE BOYS FC ya Mpemba dhidi
ya CHAPWA FC.
Kama
hiyo haitoshi ameshiriki katika ligi ya KIMONDO CUP 13/05/2015 ,Pia tarehe
17/05/2015 amecheza katika ligi ya ZAMBI CUP katika fainali akiwa na ICHENJEZYA
FC dhidi ya VWAWA SMALL BOYS. Kama hiyo haitoshi tarehe 24/05/2015 amecheza
ligi ya DIWANI CUP kata ya Halungu
katika nusu fainali akichezea timu ya WASA FC
dhidi ya LWATI FC.
Tunajiuliza
kwa michezo yote hiyo hiyo katika tarehe mbalimbali za michezo tajwa hapo juu
je yote alikuwa anatokea jangwani? Na kama hakuwa anatokea jangwani kipindi
chote hicho hawa Yanga wanajua alikuwa anakula,anavaa nini kama walivyodai
katika hoja zao.
Katika
mkataba wetu na mchezaji kipengele cha nne sehemu c kinachosema;
Katika
kipindi chote cha mkataba mchezaji anaweza kufanya majaribio kwa makubaliano ya
kimaandishi kutoka kwa klabu ,hivyo basi mchezaji amekiuka kipengele cha nne
sehemu c.
Zaidi
tunaamini klabu ya YANGA kwa makusudi imevunja kanuni hii ambayo ambayo inasema
mchezaji hataruhusiwa kufanya majaribio bila kuwa na kibali au makubaliano ya
kimaandishi na klabu yenye mkataba na mchezaji. Kama ambavyo wao YANGA
hawakuafikiana na utaratibu uliofanywa na mchezaji wao SIMON MSUVA kwenda
kufanya majaribio nchini Afrika ya Kusini ya bila kuwa na kibali kutoka kwao.
Tunapenda
kuujulisha umma kuwa KIMONDO ndio klabu ya kwanza kumudu kusajili kwa wakati
kwa kutumia mfumo wa TMS. Kwa mujibu wa barua ya pongezi tuliyoandikiwa na TFF
ilisema kwamba endapo muda wa tarehe ya mwisho ya ufungaji wa dirisha la
usajili usingeongezwa basi ni klabu moja tu ndio ingekuwa imekamilisha usajili
kwa wakati nayo ni sisis KIMONDO SUPER SPORTS CLUB. Na pia hili lieleweke wazi
kwamba usajili wa 2014/2015 hakukuwa na ujazaji wa fomu ya aina yoyote kwa timu
zote za FDL na VPL kama ilivyodaiwa na mchezaji akichagizwa na uongozi
alioandamana nao kwenda TFF na katika vyombo vya habari. Kwa nyongeza vitu
vilivyotakiwa kuambatanishwa katika usajili ni vivuli vya mkataba,cheti cha
kuzaliwa, na cheti cha daktari.Zaidi tumeelekezwa kuwa mfumo huu ndio utatumika
tena kwa msimu wa 2015/2016 kuanzia tarehe 15/June
hadi August/2015
Tunapenda
kuufahamisha umma wa watanzania kuwa usajili wa dirisha dogo ulikuwa November
hadi December 2015 na si kama ulivyoelezwa na uongozi wa Yanga kuwa walimsajili
katika dirisha dogo la ,mwezi Oktoba.
Zaidi
tunaamini Geofrey Bahati Mwashiuya ni mchezaji halali wa KIMONDO na atatumika
kwa kipindi cha mkataba kama hakuna klabu itakayokuwa na uhitaji wa huduma yake
kwa kufuata taratibu ,kanuni na sheria za usajili. Kama hakutakuwa na sababu
nyingine yeyote ya kuvunja mkataba kwa pande zote mbili.
ASANTENI SAANA KWA KUNISIKILIZA
Imesainiwa
na
Elick
Ambakisye (0755-708828)
MKURUGENZI
Kimondo
Super Sports Club
No comments:
Post a Comment