Wednesday, July 8, 2015

KILOMBERO WAJIVUNIA KUONGOZA UJENZI WA MAABARA KIMKOA

 Na John Nditi
MADIWANI wa baraza la halmashauri ya wilaya ya Kilombero, mkoani Morogoro  waliohitimisha  muda wao wa kukaa madarakani kwa kipindi cha miaka mitano  Julai 7, mwaka huu wamesema kutokana na kushirikiano na watendaji wa halmashauri,wilaya imepiga hatua kubwa ya kimaendeleo  ikiwa na  kufikia lengo la ujenzi wa maabara .

Diwani zamani wa Kata ya Kisawasawa , Hasaan Goagoa  pamoja na Hassan Kidapa wa Kata ya Chita, kwa nyakati tofauti  walisema ushirikiano baina ya madiwani bila kujali itikati ya chama , na watendaji wa  halmashauri kupitia mkurugenzi mtendaji wake umewezesha kuibadiri wilaya iwe ya kimaendeleo katika nyanja ya kiuchumi,  kielimu na kijamii.

Madiwani wa baraza hilo walishiriki Kikao  maalumu  cha baraza kilichofanyika Julai 7, mwaka huu , mjini Ifakara , ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Mkuu wa mkoa , Dk Rajab Rutengwe.

Pamoja na kushiriki kikamilifu kuhamaisha ujenzi wa maabara, walisema wanajifunia kuiacha halmashauri ikiogoza kuwa na hati safi kwa muhula minne mfululizo hadi kufikia mwaka wa fedha wa 2013/2014 .

Kwa upande wake Mweyekiti wa halmashauri hiyo aliyemaliza muda wake ambaye alikuwa Diwani wa Kata ya Sanje, David Lugazio,alisema  kwa  ushirikiano huo uliwezesha  kuongeza kasi ya ukusanyaji wa mapato ya ndani  mwaka hadi mwaka.

“ Mapato haya yamesaidia kuongoza nguvu za wananchi kwa kutoa fedha za saruji na mabati kwa kila shule za sekondari ya kata kujenga vyumba vitatu vya maabara ya masomo ya sanyansi na wilaya imekuwa ya kwanza kukamilisha kimkoa” alisema Ligazio.

Awali, Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo, Azimina Mbilinyi, alisema halmashauri iliendelea kujenga uwezo wa kukusanya mapato ya ndani ambapo kwa  mwaka wa fedha wa 2014/2015, imekusanya kiasi cha sh 5,013,479,000 sawa na asilimia 81 ya makisio ya kukusanya kiasi cha sh 5,473,840,000.

Hata hivyo alisema, kutokana na kuwepo kwa makusanyo mazuri na usimamizi wa matumizi sahihi ya mapato hayo, halmashauri imeweza kununua vifaa vya aina mbalimbali vya kuhudumia jamii ikiwemo na mitambo ya ujenzi wa barabara za halmashauri hiyo.
 Baadhi ya Maofisa Tarafa za halmashauri ya wilaya ya Kilombero akisikiliza jambo.
 Dereva wa Greda akionesha uwezo wake.
 Hassan Goagoa , aliyekuwa Diwani mkongwe na wamuda mrefu wa Kata ya Kisawasawa, akibadilishana mawazo na Mkuu wa mkoa, Dk Rajab Rutengwe, Julai 7, mwaka huu mjini Ifakara.
 Viongozi mbalimbali wangalia mitambo mipya ya ujenzi wa barabara.
 Mkuu wa mkoa wa Morogoro, Dk Rajab Rutengwe ( mwenyesuti) akibadilishana mawazo na baadhi ya Madiwani waliomaliza muda wao wa halmashauri ya wilaya ya Kilombero.
 Mkuu wa mkoa wa Morogoro, Dk Rajab Rutengwe ( suti ) akifurahia jambo pamoja na watendaji wa halmashauri ya Kilombero na madiwani waliomaliza muda wao.
 Mkuu wa mkoa wa Morogoro, Dk Rajab Rutengwe ( wa kwanza kulia) akiangalia onesho ya mitambo ya ujenzi wa barabara iliyonunuliwa na halmashauri ya wilaya ya Kilombero.
 Mkuu wa mkoa wa Morogoro, Dk Rajab Rutengwe, akizundua mitambo ya ujenzi wa barabara ya halmashauri ya wilaya ya Kilombero.
 Mkuu wa mkoa wa Morogoro, Dk Rajab Rutengwe ( katikati walikaa) akiwa katika picha ya pamoja na madiwani waliomaliza muda wao sambamba na watendaji wa halmashauri ya wilaya ya Kilombero.

No comments: