mbunge
wa Ludewa Deo Filikunjombe kulia akiwa na mlemavu wa ngozi (ALBINO)
mara baada ya kumaliza mkutano wake wa kampeni za ubunge
Na Matukiodaima Blog Ludewa
WAKATI
wanachama wa chama cha mapinduzi (CCM) kesho wanashiriki zoezi la
kupiga kura za maoni kuwapata madiwani na wagombea watakao gombea
kwa CCM ,mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe amewashukuru
wanachama wa CCM katika jimbo hilo kwa kuonyeha imani kubwa kwake
ukilinganisha na wagombea wenzake wawili na kuwa hadi sasa anauhakika
mkubwa wa kushinda tena ila ushindi utakaompa heshima ni ule wa kupata
kura zote na wenzake kuambulia patupu
Filikunjombe
aliyasema hayo wakati wa mkutano wa kujinadi kwa wagombea wa
nafasi ya ubunge katioka kata ya Ludewa mjini ,kuwa hadi sasa kutokana
na mapokeo ya wananchi na wana CCM kote walikopata kupita kwenye kata
26 za jimbo hilo la Ludewa wamekuwa wakitamka bayana kuwa kura zote
kwake hivyo kuwaomba wana CCM kwa umoja wao kumpa moyo zaidi wa
kuwatumikia tena kwa kuhakikisha wanampatia kura zote za ndio.
Alisema
kwa kauli zao wagombea wenzake wawili waliojitokeza wanaeleza bila
kuficha kuwa wametumwa na watu ambao aliwaondoa bungeni kutokana na
vitendo vyao vya ufisadi ili waje Ludewa kugombea ubunge kwa ajili ya
kulipa kisasi kwa kumtoa jambo ambalo hadi sasa limegonga mwamba
kutokana na wananchi na wana CCM Ludewa kuliona hilo.
"Niliifanya
kazi ile ya kupambana na mafisadi bungeni kwa faida ya wananchi wa
Ludewa na watanzania kwa ujumla ila nashangazwa kuona leo wana Ludewa
wachache wanakubali kutumika na mafisadi hao kutumwa kuja kunitoa
ubunge kweli ni aibu kubwa kwa kazi kubwa ambayo mimi nimeifanya
katika jimbo la Ludewa sikutegemea kupata mpinzani tena ndani ya chama
changu.....ila naomba sana wana Ludewa tuungane katika vita hii ya
maendeleo na kupinga ufisadi kwa kuwanyima kura hawa "
Alisema
kuwa wilaya ya Luudewa itajengwa na wana Ludewa kwa kushirikiana na
yeye kama mbunge wao na sio wale wanaotumika kuwadanganya wananchi wa
Ludewa hata kupinga kazi kubwa iliyofanyika kwa kipindi kifupi cha miaka
mitano .
Filikunjombe
alisema kuwa hawezi kusema kuwa amemaliza changamoto zote za wilaya
hiyo ya Ludewa kwani kama atasema hivyo atakuwa anawadanganya wananchi
wake na kuwa pamoja na kuwa amefanya mengi ila hajamaliza changamoto
zote za jimbo la Ludewa hivyo iwapo watampa tena nafasi hiyo ua ubunge
atahakikisha anaendelea kupunguza changamoto zilizobaki.
"
nimefanya kazi kubwa ya kuleta maendeleo jimbo la Ludewa ila nitakuwa
nadanganya kama nitasema nimemaliza changamoto zote pia hata wabunge
wenzangu walifanya kulingana na wakati ule na kila mmoja a namchango
wake katika maendeleo ya Ludewa .....ninachowaomba wananchi mtupime
wagombea kwa kazi tulizofanya msitupime kwa maneneo kwangu mimi ni kazi
zaidi maneno kidogo"
Hata
hivyo alisema iwapo wananchi wa kata ya Ludewa watamchagua kuwa
mbunge kwa kura za kishindo atahakikisha kero ya maji anaanza kuitatua
kabla ya serikali kuanza kufanya hivyo kwani kati ya changamoto kubwa
kwa mji wa Ludewa ni pamoja na maji .
Pia
aliwataka wananchi kupuuza uongo unaosambazwa na wagombea hao kuwa
vikao vya juu vya chama vimepanga kukata jina lake baada ya
kushindwa na kudai kuwa huo ni upotoshaji na kuwa CCm ni chama makini na
hakuna mtu wa kukatwa iwapo ametekeleza sera vema za chama.
Huku
mgombea injinia Zephania Chaula akiwaomba wananchi hao kumchagua kuwa
mbunge kwani tayari ameahidiwa na na mwenyekiti wa DP mchungaji
Christopher Mtikila na aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo kabla ya
kuangushwa na mbunge filikunjombe mwaka 2005 Prof Raphael Mwalyosi kuwa
watamsaidia kufanya kazi pamoja .
Chaula
ambae alipingwa vikali katika mkutano huo kiasi cha kuzomewa baada ya
kudai moja kati ya kazi aliyoifanya ni kuanzisha mfereji wa umwagiliaji
kata ya Ruhuhu baada ya mkazi wa kata hiyo aliyekuwepo mkutanoni hapo
kunyosha mkono na kumpinga kuwa hakuna mradi huo ni uongo na kuwa wao
wanamtegemea mbunge wao Filikunjombe ambae amefanya mengi kwenye kata
hiyo.
Wakagti
Injinia Chaula ambae siku za hivi karibuni aliambulia kura 11 katika
nafasi ya ujumbe wa NEC akipingwa vikali mkutanoni hapo mgombea Kepten
(mstaafu) Jacob Mpangala akijikuta katika wakati mgumu kufuatia mbunge
Filikunjombe kuwasilisha vielelezo sahihi mbele ya viongozi wa chama na
kugawa kwa wananchi hao viinavyoonyesha mgombea huyo anavyodanganya
wananchi kuwa alistaafu kazi wakati kuna barua ya kufukuzwa kwake kazi
kutoka TAMISEMI.
Filikunjombe
alifikia hatua hiyo ya kukabidhi ushahidi huo kwa chama baada ya
kauli ya vitisho ya mgombea huyo Mpangala kumtaka aonyeshe hadharani
ushahidi unaoonyesha kufukuzwa kakwe kazi kabla ya kuchukua hatua .
No comments:
Post a Comment