Mkuu
wa kituo cha Kulelea Watoto yatima cha Al-Madina, Bi. Kulthum Juma
akizungumzia kuhusu kituo hicho pamoja na kutoa shukrani kwa kampuni ya
Multichoice Tanzania kwa kuendelea kukisaidia kituo cha hicho ambacho
kina takribani watoto 68 na pia kituo hicho kipo eneo la Tandale kwa
Tumbo jijini Dar.
Ustadhi Mashaka Salim akitoa neno.
Mkurugenzi wa Multichoice Tanzania, Peter Fauel akichukua chakula wakati wa kuwafuturisha watoto yatima wanaolelewa katika kituo cha Al-Madina kilichopo Tandale kwa Tumbo, Wa pili kutoka kulia ni Meneja uendeshaji wa Multichoice Tanzania, Ronald Shelukindo.
Meneja
Uhusiano wa Kampuni ya Multichoice Tanzania, Barbara Kambogi, akitoa
huduma ya chakula kwa watoto yatima hii ikiwa ni njia mojawapo ya
kuwasaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu.
Baadhi
ya Watoto yatima, Wafanyakazi wa Multichoice Tanzania pamoja na
viongozi wa kituo hicho cha Al-Madina wakichukua chakula katika futari
iliyoandaliwa na kampuni ya Multichoice Tanzania.
Baadhi
ya Watoto yatima, Wafanyakazi wa Multichoice Tanzania pamoja na
viongozi wa kituo hicho cha Al-Madina wakijumuika katika futari hii
ikiwa ni moja wapo ya kutoa msaada katika vituo mbalimbali hapa nchini.
Meneja
wa Fedha wa Multichoice Tanzania, Francis Senguji akitoa neno la
shukrani kwa niaba ya Kampuni ya Multichoice Tanzania kwa waliofika na
kujumuika nao katika futari iliyoandaliwa na Kampuni ya Multichoice
Tanzania.
No comments:
Post a Comment