Friday, July 10, 2015

BIMA YA RESOLUTION YAFUTURISHA WAUMINI WA DINI YA KIISLAM KATIKA MWEZI MTUKUFU WA RAMADHANI

 Picha ya baadhi ya waumini wa dini ya kiislamu wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kufutari katika ukumbi wa hoteli Serena, futari iliyoandaliwa na Bima ya Resolution.
 Baadhi wa waumini wa dini ya kiislam wakimsikiliza mgeni rasmi Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.
  Meneja Mkuu wa Bima ya Resolution, Oscar Osir, na Shehe Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhadi Musa Salim wakiwaongoza wa umini wa Dini ya kiislamu katika mwezi Mtukuru wa Ramadhani kuchukua futari iliyoandaliwa na Bima ya Resolution jana katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
 kushoto ni  Meneja Mkuu wa Bima ya Resolution, Oscar Osir wakifutari na Shehe mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Sheikh, Alhadi Mussa Salim katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
 Meneja Mkuu wa Bima ya Resolution, Oscar Osir, akiwatambulisha wageni waliaalikwa wa dini ya kiislam waliojumuika na Bima ya Resolution katika futari iliyoandaliwa na Bima ya Resolution katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Shehe mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Sheikh, Alhadi Mussa Salim akizungumzia mara baada ya kufutari futari iliyoandaliwa na Bima ya Resolution katika hoteli ya serena jijini Dar es Salaam jana.
Mwenyekiti wa Bodi ya Bima ya Resolution,Zuhura Muro akiwashukuru waumini wa dini ya kislam kwa kujumuika pamoja na Bima ya Resolution katika kufutari iliyo andaliwa na Bima ya Resolution katika hoteli ya serena jijini Dar es Salaam jana.

Dar es Salaam, Alhamisi 9 Julai 2015: Kampuni ya Bima ya Resolution leo hii imeaanda hafla ya kufuturisha wateja wake katika hoteli ya Serena, jijini Dar es Salaam. Hafla ilihudhuriwa na Sheikh Mkuu wa Dar es Salaam, Sheikh Alhad Musa Bin Salum.



Huu ni mwaka wa pili mfululizo kwa kampuni hiyo ya bima kushirikiana na wateja wake katika iftar kwa lengo la kuwaleta karibu wateja wao na kuwashukuru kwa ushirikiano wa mwaka hadi mwaka.



"Tunawashukuru sana kwa kuhudhuria hafla hii na tunawapongeza kwa uvumilivu wenu katika mwezi huu mkuu wa Ramadhan.” Meneja Mkuu wa Resolution Insurance nchini Tanzania, Bwana Oscar Osir alisema.


Katika hafla hiyo Shiekh Mkuu aliwakumbusha waumini wote umuhimu wa mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan.




“Ningependa kuwahimiza Waislamu wenzangu kutia maanani amri wakati wa Mwezi Mtukufu. Tuonesha upendo na uvumilivu kwa wote, kusameheana na kuwasaidia wale ambao hawana uwezo wa kujisaidia” Sheikh Alhad alisema.




"Tunashukuru sana kwa ushirikiano wenu kwani ndiyo inatupa motisha ya kuendelea kuwapa huduma bora zaidi. Katika shughuli za kuwapa Huduma zilizo bora zaidi na zinazoweza kuwahudumia ukiwa hapa nchini na hata sehemu yeyote duniani. Ningependa pia kuwahakikishia kuwa tutaendelea kuwapa bidhaa bora na kuwasikiliza ili tutimize mahitaji yenu", alisema Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Resolution Insurance Bi Zuhura Muro.

No comments: