Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia, Hemedi Mgaza, kushoto, akitembelea katika ofisi ya Taasisi ya Kifedha ya Bayport Financial Services katika futuru iliyoandaliwa na taasisi hiyo. Pichani ni wadau wengine walioalikwa katika futari hiyo.
Na Mwandishi Wetu,
Dar es Salaam
Dar es Salaam
TAASISI ya Kifedha ya Bayport Financial Services, jana imefuturisha wadau wake wanaoendelea na mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhan, huku ikiwataka kudumisha amani, umoja, upendo na mshikamano kwa Watanzania wote. Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Utawala wa Bayport Financial Services, Evelyine Hall, katika futari iliyoandaliwa kwa ajili ya wadau wake mwishoni mwa wiki, jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na watu mbalimbali.
Viongozi wa Taasisi ya Bayport Financial Services na wageni waalikwa wakijadiliana jambo katika futari ya Bayport iliyofanyika jana jijini Dar es Salaam. Mwenye koti jeusi na kofia ni Haruna Mbeyu, akifurahia jambo.
Akizungumza katika futari hiyo, Evelyine alisema ni vyema Watanzania wote, hususan Waislamu kuutumia vyema mwezi huo, ikiwa ni nguzo muhimu katika Dini ya Uislamu Tanzania na duniani kwa ujumla. Alisema Bayport inaheshimu misingi ya dini zote, hivyo kwakuwa mwezi wa Ramadhan ni sehemu ya ibada kwa Waislamu, vyema wakautumia vizuri, sanjari na kulinda Amani, upendo, umoja, mshikamano, bila kusahau jamii kuishi kwa kuheshimiana ili nchi yetu iweze kupiga hatua.
Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia, Hemedi Mgaza wa tatu kutoka kulia, akipiga picha ya pamoja na viongozi wa Taasisi ya Kifedha ya Bayport Financial Services, mara baada ya kumaliza kufuturu katika futari iliyofanyika jana jijini Dar es Salaam, huku ikiandaliwa na Bayport.
Wakati wanatembelea katika ofisi ya taasisi hiyo baada ya kumaliza kupata futuru, jijini Dar es Salaam jana.
Mkuu wa Wilaya ya Kilwa, Mhe. Abdallah Ulega, mwenye kanzu akizungumza jambo katika futuru iliyoandaliwa na Taasisi ya Kifedha ya Bayport Financial Services, iliyofanyika Makao Makuu ya Taasisi hiyo, mwishoni mwa wiki, jijini Dar es Salaam. Kulia kwa DC ni Meneja Utawala wa Bayport, Evelyine Hall na anayemuhoji DC ni Mwandishi wa Habari, Phillip Daudi, aliyeshika kipaza sauti. Picha na Mpiga Picha Wetu.
“Bayport Financial Services inajivunia kutoa huduma kwa Watanzania wote, ambao leo baadhi yao wapo katika ibada ya mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhan, hivyo tunaamini mwezi huu utakuwa na tija, endapo utatumiwa vyema,” alisema Evelyine. Naye Meneja Masoko na Mawasiliano wa Bayport Financial Services, Ngula Cheyo, alisema kuwa Watanzania wamekuwa wakiishi kwa kuheshimiana, hivyo wanaamini wataendelea kutoa huduma bora ya mikopo ya fedha, mikopo ya viwanja, mikopo ya bidhaa mbalimbali kama vile injini ya boti, vifaa vya ujenzi, ambapo huduma zote hizo zinapatikana kwa njia ya mtandao wa www.kopabayport.co.tz na kupitia mawakala
na ofisi zao zilizoenea sehemu mbalimbali za Tanzania Bara.
Mkuu wa Wilaya Kilwa, DC Abdallah Ulega kulia, akipiga picha na Meneja Utawala wa Taasisi ya Kifedha ya Bayport Financial Services, Evelyine Hall na Meneja Masoko na Mawasiliano wa Bayport Financial Services, Ngula Cheyo kushoto. DC alikuwa miongoni mwa wadau walioalikwa katika tukio la futari lililofanyika jana jijini Dar es Salaam na kuandaliwa na taasisi hiyo inayojihusisha na mambo ya mikopo.
Katika hatua nyingine, Mkuu wa Wilaya Kilwa, Abdallah Ulega, aliipongeza Bayport kwa kitendo chao cha kiungwana cha kuamua kuandaa futari hiyo kwa wadau wao. “Sisi serikali tutaendelea kuwaunga mkono wadau mbalimbali wenye kuamua kuanzisha mambo mazuri kama haya, hivyo tunawapongeza kwa dhati juu ya jambo hili muhimu linalojenga kuheshimiana kwa namna moja ama nyingine,” alisema Ulega.
Bayport Financial Services ni miongoni mwa taasisi za kifedha zinazojihusisha na mambo ya mikopo, ikiwa na mchango mkubwa kwa Watanzania wote wanaoamua kukopa ili kujikwamua kiuchumi, ambapo watumishi wa umma na wafanyakazi wa kampuni zilizoidhinishwa wamekuwa wakinufaika kwa kiasi kikubwa tangu taasisi hiyo ilipoanzishwa nchini.
No comments:
Post a Comment