Thursday, June 18, 2015

WIZARA YA MALIASILI NA UTALII KWA KUSHIRIKIANA NA ASASI ZA KIMATAIFA WILDAID, AFRICAN WILDLIFE FOUNDATION WAZINDU KAMPENI YA KUPAMBA NA NA UJADILI WA TEMBO

Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyarandu akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na uzinduzi wa kampeni mpya ya kupambana na ujangilli wa Tembo uliofanyika katika hoteli ya Sea Cliff jijini Dar es Salaam Juni 18, 2015. Picha zote na CATHBERT KAJUNA WA KAJUNASON BLOG.
Balozi wa Mpya wa Kampeni ya Kupambana na Ujangili wa Tembo, Msanii wa mziki wa kizazi kipya Ali kiba akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na uzinduzi wa kampeni mpya ya kupambana na ujangilli wa Tembo uliofanyika katika hoteli ya Sea Cliff jijini Dar es Salaam Juni 18, 2015.
Afisa Mtendaji Mkuu wa African Wildlife Foundation, Dk. Patrick Bergin akizungumza katika mkutano wa uzinduzi wa kampeni ya sifa ya wanyamapori katika hotel ya Sea Cliff jijini Dar es Salaam Juni 18, 2015.
Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhaji Mussa Salum akizungumza na waandishi wa habari leo katika hoteli ya Sea Cliff jijini Dar es Salaam Juni 18, 2015.
Balozi wa Mpya wa Kampeni ya Kupambana na Ujangili wa Tembo, Msanii Jacqueline Mengi kuhusiana na uzinduzi wa kampeni mpya ya kupambana na ujangilli wa Tembo uliofanyika katika hoteli ya Sea Cliff jijini Dar es Salaam Juni 18, 2015.
Balozi wa Mpya wa Kampeni ya Kupambana na Ujangili wa Tembo, Msanii wa mziki wa kizazi kipya Ali kiba akizungumza na waandishi wa habari.
 Viongozi wa Dini waliofika katika uzinduzi huo wakifuatilia kwa makini...
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyarandu akizungumza na Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhaji Mussa Salum.
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyarandu akiwa katika picha ya pamoja na Mabalozi wa kampeni hiyo.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyarandu akiwa pamoja na Viongozi wa dini na mabalozi wa kampeni hiyo.
---
Lengo la WildAid ni kukomesha biashara haramu ya wanyama pori kwa kupunguza mahitaji ya bidhaa zitokanazo na wanyamapori kupitia kampeni za uhamasishaji. 

 Pia lengo la WildAid ni kutoa hifadhi na ulinzi wa uhakika kwa viumbe wa baharini. Biashara haramu ya wanyama pori inakadiriwa kuwa na thamani ya zaidi ya dola bilioni 10 kila mwaka na imesababisha kupungua sana kwa wanyama pori sehemu mbalimbali duniani. 

Kama ilivyo biashara ya madawa ya kulevya, uwepo wa sheria dhidi ya biashara hiyo na jitihada za kuhakikisha utekelezaji wa sheria havijaweza kuleta ufumbuzi wa tatizo hili. Kila mwaka, mamia ya mamilioni ya dola hutumika kuwalinda wanyamapori, lakini kiasi kidogo kukomesha mahitaji ya viungo vya wanyama pori na bidhaa zitokanazo na wanyama pori. 

WildAid ndio shirika pekee ambalo limelenga kupunguza mahitaji kupitia ujumbe rahisi usemao: UNUNUZI UKIISHA, MAUAJI NAYO YATAISHA. 

WildAid inafanya kazi na mamia ya watu mashuhuri katika bara la Asia na nchi za Magharibi hususani wanasiasa mashuhuri, watu maarufu na viongozi wa makampuni makubwa wakiwemo Mrithi wa Ufalme wa Uingereza Prince William, Yao Ming, Jackie Chan, Li Bingbing na Sir Richard Branson ili kuwashawishi watu waache kununua bidhaa zitokanazo na wanyama walioko katika hatari ya kutoweka. Hivi sasa ujumbe huu na jitihada kuelimisha watu zinawafikia mamia ya mamilioni ya watu nchini China kila wiki kupitia matangazo mbalimbali.

No comments: