Mrajisi wa Baraza la Wauguzi na Wakunga Zanzibar Haji Haji
Khamis akieleza mchakato wa kulisajili Baraza la Wauguzi na Wakunga katika uzinduzi rasmi uliofanyika Chuo cha
Sayansi ya Afya Mbweni nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
Mwenyekiti wa Baraza la Wauguzi na
Wakunga
Zanzibar Bi. Amina Abdulkadir akitoa maelezo ya kazi za Baraza hilo
katika sherehe za uzinduzi zilizofanyika Chuo cha Sayansi ya
Afya Mbweni .
Waziri wa Afya wa Zanzibar Rashid Seif akizungumza na wajumbe wa Baraza la Wauguzi
na Wakunga Zanzibar kabla ya kulizindua rasmi huko Mbweni, Chuo cha Sayansi ya
Afya.
Baadhi ya washiriki wakimsikiliza mgeni rasmi
katika uzinduzi wa Baraza la Wauguzi na Wakunga Zanzibar kwenye sherehe za uzinduzi
wa Baraza hilo.Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.
Picha ya pamoja ya mgeni rasmi Waziri wa Afya
Rashid Seif na wajumbe wa Baraza la Wauguzi na Wakunga mara baada ya uzinduzi
rasmi.
Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.
Na Ramadhani Ali/Maelezo Zanzibar
Waziri
wa Afya wa Zanzibar Rashid Seif ameliagiza Baraza la Wauguzi na
Wakunga Zanzibar kusimamia kwa karibu watendaji wa kada hiyo ili waweze
kuendelea kutoa huduma bora kwa wananchi.
Akizungumza
katika uzinduzi rasmi wa Baraza Wauguzi na Wakunga katika Chuo cha
Sayanzi ya Afya Mbweni, Waziri Rashid Seif amesema wauguzi na wakunga ni
walezi wanaoshughulikia matatizo ya watu hivyo wanatakiwa kutekeleza
wajibu wao kwa uadilifu.
Amesema
wananchi wanapofika Hospitali na vituo vya Afya wanategemea hifadhi na
kinga ya wauguzi kabla ya kuonana na daktari na kumekuwa na malalamiko
mengi kutoka kwa wananchi ambayo yanahitaji kutafutiwa ufumbuzi na
Baraza hilo.
Waziri wa
Afya amelitaka Baraza kuwa karibu na kuwafuatilia wauguzi na wakunga
kwenye vituo vyao vya kazi ili kuhakikisha kada hiyo inajengewa
heshma yake inayostahiki.
Amesema kumekuwa
na malalamiko mengi kutoka kwa mama wajawazito wanapofika vituo vya
afya kujifungua na baadhi yao hukataa kujifungua kwenye vituo hivyo kwa
kuogopa kunyanyaswa na wakunga na wauguzi.
Amelishauri
Baraza kufuatilia kwa karibu vyuo vinavyosomesha afya ya binaadamu na
kuhakikisha vyuo hivyo vimesajiliwa rasmi na vinawataalamu wa fani
hiyo na wanafunzi wanaojiunga wanazo sifa zinazotakiwa ili kutoa wauguzi
wenye viwango vya taaluma hiyo.
Mwenyekiti
wa Baraza la Wauguzi na Wakunga Zanzibar Bi. Amina Abdulkadir
amemueleza Waziri wa Afya kwamba Baraza hilo litatekeleza wajibu
wake wa kusimamia wafanyakazi wa kada hiyo na halitakuwa na muhali kwa
mtu ama taasisi itakayokwenda kinyume na maagizo yake.
Amesema
miongoni mwa kazi kubwa za Baraza la Wauguzi na Wakunga ni kulinda
afya za raia, kuweka viwango katika maadili na utendaji wa wauguzi
katika kutoa huduma bora na kuhakikisha wauguzi wote wana elimu
inayoendana na teknolojia ya kisasa.
Amemuhakikishia
Waziri kwamba Baraza litaanza kazi zake mara moja kwa kuwasajili
wauguzi wote wenye sifa na wale ambao wataonekana wanadandia watakuwa
hawana nafasi.
Baraza
la Wauguzi na Wakunga limeundwa kwa sheria No.5 ya mwaka 2014 na
ilipitishwa na Baraza la Wawakilishi tarehe 22 Oktoba na linawajumbe 13
kutoaka Taasisi za Serikali na Taasisi binafsi .
No comments:
Post a Comment