Sunday, June 7, 2015

WANA CCM MKOANI SINGIDA, TABORA NA SHINYANGA WAJITOKEZA KUMDHAMINI WAZIRI MAGUFULI

Waziri wa Ujenzi ambaye pia ni Mbunge wa Chato Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikabidhiwa fomu yenye orodha ya Wadhamini waliojitokeza kumdhamini katika mbio za kuwania Urais wa Jamhuri ya Muungano kupitia chama hicho kutoka kwa Katibu wa CCM Wilayani Nzega Mkoani Tabora.
Waziri wa Ujenzi Dkt. Magufuli akikabidhiwa fomu yenye orodha ya Wadhamini waliojitokeza kumdhamini katika Mkoa wa Shinyanga.
Baadhi ya Wadhimini waliojitokeza kumdhamini Waziri wa Ujenzi ambaye pia ni Mbunge wa Chato Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli mkoani Singida wakimfurahia mara baada ya zoezi la uhakiki na kumdhamini katika mkoa wao kukamilika.
Wanachama wa CCM Wilayani Nzega wakiwa kwenye foleni kusubiri kuhakikiwa kwa kadi zao kabla ya kumdhamini Dkt. Magufuli.
Waziri wa Ujenzi Dkt. Magufuli akisalimiana na baadhi ya Wanachama wa CCM Wilayani Nzega waliojitokeza kumdhamini.
Waziri wa Ujenzi Dkt. Magufuli akisaini kitabu katika Ofisi za CCM Mkoani Singida.

No comments: