Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwamini Malemi (kulia) akimkabidhi
zawadi ya Ngao ya Utumishi Mrefu na Maadili Mema, Katibu Mkuu wa wizara hiyo,
Mbarak Abdulwakil, kwa niaba ya Wakuu wa Idara na Vitengo wizarani humo. Zawadi
hiyo ya kushtukiza iliandaliwa na viongozi hao wa Idara baada ya hivi karibuni Rais
Jakaya Kikwete kumvisha Nishani ya Utumishi Mrefu na Maadili Mema Daraja la
(I), Katibu Mkuu wao katika tukio lililofanyika Ikulu, jijini Dar es Salaam. Kushoto
ni Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa wizara hiyo, Lilian Mapfa. Picha
zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi.
Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwamini Malemi (kulia)
akimkabidhi zawadi ya ua Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Mbarak Abdulwakil, kwa
niaba ya Wakuu wa Idara na Vitengo wizarani humo. Zawadi hizo za kushtukiza ziliandaliwa
na viongozi hao baada ya hivi karibuni Rais Jakaya Kikwete kumvisha Nishani ya
Utumishi Mrefu na Maadili Mema Daraja la (I), Katibu Mkuu wao katika tukio
lililofanyika Ikulu, jijini Dar es Salaam
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwamini Malemi (kulia) akimkabidhi zawadi ya kitabu cha
kutunzia kumbukumbu, Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Mbarak Abdulwakil, kwa niaba
ya Wakuu wa Idara na Vitengo wizarani humo. Zawadi hizo za kushtukiza
ziliandaliwa na watendaji hao baada ya hivi karibuni Rais Jakaya Kikwete kumvisha
Nishani ya Utumishi Mrefu na Maadili Mema Daraja la (I), Katibu Mkuu wao katika
tukio lililofanyika Ikulu, jijini Dar es Salaam.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil (kushoto),
akimshukuru Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa wizara hiyo, Lilian
Mapfa, pamoja na Wakuu wa Idara wengine baada ya kupewa zawadi za kushtukiza na
wakuu hao baada ya Katibu Mkuu huyo hivi karibuni Rais Jakaya Kikwete kumvisha
Nishani ya Utumishi Mrefu na Maadili Mema Daraja la (I), katika tukio
lililofanyika Ikulu, jijini Dar es Salaam.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil (kulia),
akimshukuru Mkuu wa Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani wa wizara hiyo, Martina
Nguluma pamoja na Wakuu wa Idara wengine baada ya kupewa zawadi za kushtukiza
na watendaji hao baada ya Katibu Mkuu huyo hivi karibuni Rais Jakaya Kikwete kumvisha
Nishani ya Utumishi Mrefu na Maadili Mema Daraja la (I), katika tukio
lililofanyika Ikulu, jijini Dar es Salaam.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil (kulia),
akimshukuru Mkuu wa Kitengo cha Uhasibu wa wizara hiyo, Edwin Makene pamoja na Wakuu
wa Idara wengine baada ya kupewa zawadi za kushtukiza na viongozi hao baada ya
Katibu Mkuu huyo hivi karibuni Rais Jakaya Kikwete kumvisha Nishani ya Utumishi
Mrefu na Maadili Mema Daraja la (I), katika tukio lililofanyika Ikulu, jijini
Dar es Salaam.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil (wanne kushoto), akiwa
katika picha ya pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Mwamini Malemi (watatu
kulia), Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu, Lilian Mapfa (katikati),
Mkurugenzi wa Sera na Mipango, Haji Janabi (wanne kulia), Mkurugenzi wa Kitengo
cha Manunuzi, Manyama Mapesi (watatu kushoto), Mkurugenzi wa Huduma za Sheria,
Marlin Komba (kushoto), Mkuu wa Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
(TEHAMA), Jane Massawe (wapili kushoto), Mkuu wa Kitengo cha Uhasibu, Edwin
Makene (wapili kulia) na Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Christina Mwangosi. Wakuu wa Idara wa wizara hiyo walimpa zawadi ya kushtukiza
Katibu Mkuu wao baada ya hivi karibuni Rais Jakaya Kikwete kumvisha Nishani ya
Utumishi Mrefu na Maadili Mema Daraja la (I).
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil akiwa amepatwa na
mshangao mara baada ya kuingia Ukumbi wa Mikutano wa wizara hiyo baada ya kuona
Wakuu wa Idara wa wizara yake (hawapo pichani) wakiwa wamebeba zawadi
mbalimbali kwa ajili ya kumkabidhi baada ya hivi karibuni Rais Jakaya Kikwete kumvisha
Nishani ya Utumishi Mrefu na Maadili Mema Daraja la (I), katika tukio
lililofanyika Ikulu, jijini Dar es Salaam. Picha zote na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi.
No comments:
Post a Comment