Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO)
nchini Tanzania, Bi. Zulmira Rodrigues (kulia) akimwelezea Katibu
Tawala, Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro, Lemuel Kristian Kileo (wa
pili kushoto), namna mradi wa ujenzi wa kituo cha sanaa ikiwa ni pamoja
na kutoa mafunzo ya ujasiliamali wa bidhaa zinazotokana na mifugo kwa
akinamama na wasichana kutoka Kata tano za Wilaya ya Ngorongoro
utakavyotekelezwa juzi katika Kijiji cha Ololosokwan. Wengine ni maofisa
miradi kutoka UNESCO wakishuhudia.

SHIRIKA
la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) nchini Tanzania
linatarajia kutekeleza mradi wa ujenzi wa kituo cha sanaa ikiwa ni
pamoja na kutoa mafunzo ya ujasiliamali wa bidhaa zinazotokana na mifugo
kwa akinamama na wasichana kutoka Kata tano za Wilaya ya Ngorongoro
kama jitihada za kuongeza kipato kwa familia za jamii ya Wamasai.
Akitoa
maelekezo ya mradi huo juzi katika Kijiji cha Ololosokwan mbele ya
Katibu Tawala, Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro, Lemuel Kristian
Kileo, Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni
(UNESCO) Tanzania, Bi. Zulmira Rodrigues alisema mradi huo unatarajia
kutekelezwa kuanzia Mwezi Agosti, 2015.
Bi. Rodrigues alimueleza Kileo kuwa mradi huo unajumuisha ujenzi wa
kituo cha kisasa cha sanaa ambacho kitatumiwa na wajasiliamali wa jamii
ya Kimasai kwa ajili ya kuuza bidha zao za asili mbalimbali kwa watalii
wanaofika kutembelea vivutio anuai vya utalii ikiwemo Hifadhi ya Taifa
ya Ngorongoro inayozunguka vijiji hivyo.
Akifafanua
zaidi juu ya mradi huo, Ofisa Mradi Utamaduni wa Shirika la Kimataifa
la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) nchini Tanzania, Rehema Sudi
alisema mradi huo utajumuisha mafunzo ya ujasiliamali juu ya
utengenezaji wa bidhaa za ngozi, pembe za ng'ombe pamoja na shanga ili
kuziongezea thamani na kuuzwa kwa watalii anuai wanaotembelea vivutio na
kukuza vipato vya familia hasa akinamama.
Bi.
Sudi aliongeza kuwa kata zinazotarajia kunufaika na mafunzo na ujenzi
wa kituo hicho cha kisasa kwa ajili ya mauzo ya bidhaa hizo za asili za
Wamasai ni pamoja na Kata za Ololosokwani, Arash, Soit Sambu, Oloipili
na Kata ya Aoliani Magaidulu zote za Halmashauri ya Wilaya ya
Ngorongoro.
"Mradi
huu utajumuisha akinamama na wasichana kutoka kata tano ambazo ni
Ololosokwani, Arash, Soit Sambu, Oloipili na Kata ya Aoliani Magaidulu,
tutawapatia mafunzo juu ya utengenezaji wa bidhaa mbalimbali
zinazotokana na ngozi na pembe za ng'ombe pamoja na shanga ikiwa ni
hatua ya kuziongezea thamani kisha kuziuza kwa watalii ambao
wanatembelea vivutio vya utalii eneo hili hasa Kijiji cha Ololosokwan,"
alisema Ofisa Mradi Utamaduni Unesco, Bi. Sudi.
Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO)
nchini Tanzania, Bi. Zulmira Rodrigues (kulia) akimuonesha Katibu
Tawala, Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro, Lemuel Kristian Kileo (wa
pili kulia) kompyuta ndogo mpakato ambazo zimefungwa katika darasa moja
maalumu kwa mafunzo mbalimbali kwa watoto na wahitaji wengine. Darasa
hilo ni sehemu ya mradi wa kidijitali unaojumuisha Kliniki ya kisasa ya
matibabu ya macho na meno pamoja na huduma za uchunguzi magonjwa
mbalimbali kwa kutumia fipimo vya 'X-Ray' na 'Ultra-sound' na shule ya
kisasa kwa ajili ya mafunzo anuai Kijijini hapo.
Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO)
nchini Tanzania, Bi. Zulmira Rodrigues (kulia) akitembelea eneo la mradi
wa Kijiji cha kidijitali unaojumuisha Kliniki ya kisasa ya matibabu ya
macho na meno pamoja na huduma za uchunguzi magonjwa mbalimbali kwa
kutumia vipimo vya 'X-Ray' na 'Ultra- sound' na shule ya kisasa kwa
ajili ya mafunzo anuai Kijijini hapo. Katikati ni Katibu Tawala,
Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro, Lemuel Kristian Kileo pamoja na
Ofisa Mradi Utamaduni wa Shirika la UNESCO nchini Tanzania, Rehema Sudi
wakikagua mradi huo.
Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO)
nchini Tanzania, Bi. Zulmira Rodrigues (kulia) akitembelea eneo la mradi
wa Kijiji cha kidijitali unaojumuisha Kliniki ya kisasa ya matibabu ya
macho na meno pamoja na huduma za uchunguzi magonjwa mbalimbali kwa
kutumia fipimo vya 'X-Ray' na 'Ultra- sound' na shule ya kisasa kwa
ajili ya mafunzo anuai Kijijini hapo. Katikati ni Katibu Tawala,
Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro, Lemuel Kristian Kileo pamoja na
Ofisa Mradi Utamaduni wa Shirika la UNESCO nchini Tanzania, Rehema Sudi
wakikagua mradi huo.
Sehemu ya majengo ya mradi wa Kijiji cha kidijitali unaojumuisha
Kliniki ya kisasa ya matibabu ya macho na meno, huduma za uchunguzi wa
magonjwa mbalimbali kwa kutumia vipimo vya 'X-Ray' na 'Ultra- sound' na
shule ya kisasa kwa ajili ya mafunzo anuai Kijijini hapo. Mradi huo
unatekelezwa na Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni
(UNESCO) nchini Tanzania kwa kushirikiana na wafadhili wengine ikiwemo
kampuni ya Samsung Tanzania Kata ya Ololosokwan wilayani Ngorongoro.
Alisema
wataalam na wabunifu wataletwa katika vijiji vya mradi na kutoa mafunzo
kwa akinamama na wasichana kabla ya ujenzi wa kituo maalumu ambacho
kitatumiwa na wanufaika wa mafunzo hayo kama eneo la kuuzia bidhaa zao
ikiwa ni sehemu pia ya kulinda na kukuza tamaduni za jamii ya Wamasai.
"...Tutazunguka na kutoa mafunzo juu ya ubunifu na utengenezaji wa
bidhaa mbalimbali za ngozi, pembe za ng'ombe pamoja na shanga na
kutengeneza bidhaa za asili kwa ajili ya kuziuza kwa wateja hasa
watalii," alisema Bi. Sudi.
Hata hivyo Ofisa huyo mradi Utamaduni wa UNESCO alisema sehemu ya
maandalizi ya mradi huo unaotekelezwa kwa msaada wa UNESCO pamoja na
washirika wengine ambao ni Umoja wa Ulaya (EU) na Chuo Kikuu cha
Liechtenstein na pia Chuo Kikuu cha Ardhi cha Dar es Salaam imeanza
kutekelezwa tangu Februari 2015.
Mbali
na mradi huo UNESCO pia inatekeleza mradi wa ujenzi wa Kijiji cha
Dijitali, ambao unajumuisha ujenzi wa Kliniki ya kisasa ya matibabu ya
macho, Kliniki ya kisasa ya matibabu ya meno pamoja na huduma za
uchunguzi wa magonjwa mbalimbali kwa kutumia fipimo vya 'X-Ray' na
'Ultra-sound' na shule ya kisasa kwa ajili ya mafunzo anuai katika
Kijiji cha Ololosokwan huduma itakayosaidia jamii za wafugaji maeneo ya
Ngorongoro.
Sehemu ya majengo ya mradi wa Kijiji cha kidijitali unaojumuisha
Kliniki ya kisasa ya matibabu ya macho na meno, huduma za uchunguzi wa
magonjwa mbalimbali kwa kutumia vipimo vya 'X-Ray' na 'Ultra- sound' na
shule ya kisasa kwa ajili ya mafunzo anuai Kijijini hapo. Mradi huo
unatekelezwa na Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni
(UNESCO) nchini Tanzania kwa kushirikiana na wafadhili wengine ikiwemo
kampuni ya Samsung Tanzania Kata ya Ololosokwan wilayani Ngorongoro.
Sehemu ya majengo ya mradi wa Kijiji cha kidijitali unaojumuisha
Kliniki ya kisasa ya matibabu ya macho na meno, huduma za uchunguzi wa
magonjwa mbalimbali kwa kutumia vipimo vya 'X-Ray' na 'Ultra- sound' na
shule ya kisasa kwa ajili ya mafunzo anuai Kijijini hapo. Mradi huo
unatekelezwa na Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni
(UNESCO) nchini Tanzania kwa kushirikiana na wafadhili wengine ikiwemo
kampuni ya Samsung Tanzania Kata ya Ololosokwan wilayani Ngorongoro.
Sehemu ya majengo ya mradi wa Kijiji cha kidijitali unaojumuisha
Kliniki ya kisasa ya matibabu ya macho na meno, huduma za uchunguzi wa
magonjwa mbalimbali kwa kutumia vipimo vya 'X-Ray' na 'Ultra- sound' na
shule ya kisasa kwa ajili ya mafunzo anuai Kijijini hapo. Mradi huo
unatekelezwa na Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni
(UNESCO) nchini Tanzania kwa kushirikiana na wafadhili wengine ikiwemo
kampuni ya Samsung Tanzania Kata ya Ololosokwan wilayani Ngorongoro.
Sehemu ya majengo ya mradi wa Kijiji cha kidijitali unaojumuisha
Kliniki ya kisasa ya matibabu ya macho na meno, huduma za uchunguzi wa
magonjwa mbalimbali kwa kutumia vipimo vya 'X-Ray' na 'Ultra- sound' na
shule ya kisasa kwa ajili ya mafunzo anuai Kijijini hapo. Mradi huo
unatekelezwa na Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni
(UNESCO) nchini Tanzania kwa kushirikiana na wafadhili wengine ikiwemo
kampuni ya Samsung Tanzania Kata ya Ololosokwan wilayani Ngorongoro.
Imeandaliwa na thehabari.com,Ngorongoro.
No comments:
Post a Comment