Uongozi
pamoja na Wafanyakazi wa kituo cha radio ya EFM 93.7 kwa pamoja
wakikata keki kusherehekea kutimiza mwaka mmoja wa kituo hicho ambacho
kwa sasa kinakuja kwa kasi jijini Dar na kwingineko,hafla hiyo ilikwenda
sambamba na kuadhimisha miaka 16 ya msanii Mkongwe wa muziki wa kizazi
kipya Juma Nature,katika tamasha lililoitwa KOMAA CONCERT,ambalo
lilifanyika ndani ya kiota cha maraha cha Dar Live,Mbagala jijini Dar
mwishoni mwa wiki na kuhudhuriwa na maelfu ya mashabiki na wapenzi wa
muziki .
Lengo
la kuwaburudisha Mashabiki wa Juma Nature na wasikiliazaji wa 93.7 EFM
ilikuwa pia ni sehemu ya kuwashukuru mashabiki kwa ushirikiano wao kwa
miaka kumi na sita ya muziki tangu kuanza msanii huyo Juma Nature aingie
kwenye game ya Muziki nchini Tanzania.
Baadhi
ya Wasanii walioshiriki kulinogesha tamasha hilo ni pamoja na Profesa
Jay, Shetta, Snura, Makomando, Msagasumu na wengine wengi. Katika
tamasha hilo lililowavutia wakazi wa Mbagala na vitongoji
vyake,kiingilio kilipangwa kuwa ni shilingi 7,000 tu.
Meneja
Mwasiliano na mambo ya Sheria wa EFM 93.7 Deniss ssebo alisema kuwa
wanaamini Msanii Juma nature ni msanii mwenye kipaji kikubwa na
aliyewahamasisha wasanii kibao kuingia katika muziki huu wa kizazi kipya
hivyo anastahili kupewa heshima kubwa kwa mchango wake mkubwa katika
kukuza muziki wa kizazi kipya,alisema na kuongeza kuwa lakini kwa Efm
huyo ni msanii wa Kwanza tu na itaendelea kufanya hivyo kwa wasanii
wengine kwa kuwa wanaaamini Muziki unaongea.
Mkurugenzi wa Efm Dj Majay akiongoza jopo la wafanyakazi wenzake kukata keki
Pichani kulia ni Meneja
Mwasiliano na mambo ya Sheria wa EFM 93.7 Deniss Ssebo akizungumza
jambo mbele ya mwashabiki na wapenzi wa muziki na pia wasikilizaji
wakubwa wa kituo hicho kuhusiana na utaratibu mzima wa sherehe
hiyo,kulia ni Mkurugenzi wa Efm Dj Majay akigawa keki kwa mashabiki
waliofika kushuhudia tukio hilo ndani ya Dar Live.
Msanii
Mkongwe wa muziki wa kizazi kipya Juma Nature akitumbuiza jukwaani
mbele ya mashabiki wake,pia akiwashukuru kumpa sapoti ya kutosha tangu
ameanza muziki na sasa anatimiza miaka 16 katika tasnia hiyo adhimu.
Wakongwe pamoja Juma Nature na Prof.Jay wakishoo love kwa mashabiki wao.
Msanii Snura na Madansa wake wakilishambulia jukwaa la KOMAA CONCERT
Msanii
wa muziki wa kizazi kipya atambulikae kwa jina la kisanii Shetta
akitumbuiza mbele ya mashabiki kibao waliofika kwenye tamasha la KOMAA
CONCERT.
Makamuzi yalikuwa yakiendelea jukwaani.
amsha amsha za hapa na pale zikiendelea jukwaani.
Mashabiki walikuwa kibao.
Deejay Spar akionesha uwezo wake kwa mashabiki.
Shabiki wa ukweli kwa Juma Nature
Burudani ilipangwa sawa bin sawia huku Ma -Mc wakinogesha shughuli
Dar Live palinoga usiku huo wa KOMAA CONCERT
Mtangazaji mahiri wa EFM Capt.Gadn G Habash akizungumza jambo mbele ya mshabiki
Kila alieweza kuchukua kumbukumbu kwa aina yake,ilikuwa ruksaa.
Dj Majay akihakikisha mambo yanakwenda sawa
No comments:
Post a Comment