TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI - RELEASE NO. 98
TAREHE 15 JUNI, 2015
TAIFA STARS YAFUNGWA NA MISRI
Timu
ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) inayodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro
Premium Lager, leo imepoteza mchezo wake wa kwanza kuwania kufuzu kwa
fainali za AFCON mwaka 2017 baada ya kufungwa kwa mabao 3 - 0 na wenyeji
Misri.
Taifa
Stars ilicheza vizuri kipindi cha kwanza na hasa sehemu ya ulinzi
ilifanya kazi ya ziada kuokoa mashambulizi ya washambuliaji wa timu ya
Misri, na kupelekea kwenda mapumziko -0 - 0.
Kipindi
cha pili Misri walifanya mabadiliko yaliyowapelekea kupata mabao hayo 3
ndani ya dakika 10, kupitia kwa Ramy Rabia(60), Basem Morsy(64) na
Mohamed Salah (69).
Stars
ilifanya mabadiliko ya kuwaingiza Frank Domayo, Saimon Msuva na Salim
Mbdonde na kufanya shambulizi kadhaa langoni kwa Misri lakini
mashambulzi hayo yaliokolewa na walinzi wa timu ya Misri.
Mara
baada ya mchezo huo, Taifa Stars inaondoka leo Alexandria kuelekea
Cairo ambapo itaondoka na shirika la ndege la Ethiopia saa 8 usiku na
kufika jijini Dar es salaam jumanne saa 7 mchana.
Tanzania:
Deogratias Munish, Shomari Kapombe, Oscar Joshua, Aggrey Morris/Salim
Mbonde, Nadir Haroub, Erasto Nyoni, Jonas Mkude, Mwinyi Kazimoto/Saimon
Msuva, Thomas Ulimwengu, Mbwana Samata, Amri Kiemba/Frank Domayo.
Misri:
Ahmed El Shenawy, Ahmed Hegazy, Ramy Rabea, Mohamed Abd Elshafy, Hazem
Emam, Mohamed Elneny, Ibrahim Salah, Mahmoud Abd Elmonem/Ramadan Soffiy,
Mohamed Salah/Mostafa Ftahy, Doly Elgabay/Basem Morsy, Ahmed Hassan
Meky.
USAJILI WA WACHEZAJI KUANZA JUNI 15
Usajili
wa wachezaji kwa hatua ya kwanza msimu huu (2015/2016) unaanza Juni 15
hadi Agosti 6 mwaka huu wakati kipindi cha kutangaza wachezaji
walioachwa au kusitishiwa mikataba ni kuanzia Juni 15-30 mwaka huu.
Kipindi
cha kwanza cha uhamisho wa wachezaji ni kuanzia Juni 15 mwaka huu hadi
Julai 30 mwaka huu. Kupitia majina na kutangaza pingamizi ni kati ya
Agosti 7 na 14 mwaka huu. Kuthibitisha usajili hatua ya awali ni Agosti
15 hadi 19 mwaka huu.
Usajili
hatua ya pili utakuwa kati ya Agosti 17 na Septemba 8 mwaka huu.
Kupitia na kutangaza majina ya pingamizi hatua ya pili ya usajili ni
kuanzia Septemba 8 hadi 14 mwaka huu. Uthibitisho wa usajili hatua ya
pili ni Septemba 15 na 17 mwaka huu.
Wachezaji
wanaotoka nje ya Tanzania, usajili wa mtandao wa FIFA wa TMS utakuwa
wazi kuanzia kesho (Juni 15) hadi Septemba 6 mwaka huu. Klabu
zinazosajili wachezaji kutoka nje zinatakiwa kufanya hivyo kupitia
akaunti zao za mtandao wa TMS.
Kwa
klabu ambazo hazina akaunti ya TMS zinatakiwa kuwasiliana na TFF ili
mameneja wao wa usajili wapatiwe mafunzo ya TMS, na baadaye kuombewa
akaunti hizo FIFA.
Kwa
upande wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) inatarajiwa kuanza Agosti 22 mwaka
huu, na ratiba inatarajiwa kutoka mwezi mmoja kabla (Julai 22 mwaka
huu).
Ligi
Daraja la Kwanza (FDL) inatarajiwa kuanza Septemba 12 mwaka huu, wakati
Ligi Daraja la Pili (SDL) inatarajia kuanza Oktoba 17 mwaka huu.
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
No comments:
Post a Comment