NACTE yavifutia usajili
vyuo vitatu (3) na kuvishusha hadhi vyuo
kumi na sita (16)
Dar es Salaam, 24 Juni 2015 — Katika jitihada za kuinua ubora wa elimu
ya ufundi nchini, Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) limevifutia usajili
vyuo vitatu na kuvishusha hadhi vyuo
kumi na sita.
Akizungumza na waandishi wa habari
jijini Dar es Salaam jana, Kaimu Katibu Mtendaji wa NACTE Dkt. Adolf B. Rutayuga
alisema kuwa, hatua hiyo imefikiwa baada ya vyuo husika kushindwa kurekebisha
kasoro zilizobainishwa na NACTE.
“Kwa kutumia Sheria ya
Bunge Sura Na. 129 na Kanuni za Baraza za Usajili (2001) na zile za Ithibati na
Utambuzi (2001), mnamo tarehe 20 Februari 2015, Baraza lilitoa notisi ya siku
30 kwa taasisi na vyuo vilivyokiuka taratibu na vyenye mapungufu makubwa ya
Usajili na Ithibati kupitia taarifa yake kwa Umma. Notisi hii ililenga kuzipa
taasisi na vyuo nafasi ya kujitetea na kufanya marekebisho yaliyobainishwa,”
alieleza.
Kaimu Katibu Mtendaji huyo ambaye ni Mkurugenzi
wa Ushauri na Malezi ya Taasisi na Vyuo vya Ufundi NACTE aliwaambia waandishi
wa habari kuwa, Baraza linakiri kuwa taasisi na vyuo vingi vilivyopewa
maelekezo ya kufanya marekebisho vimechukua hatua mbalimbali za kurekebisha
mapungufu yabainishwa. Hata hivyo alisema hadi kufikia leo tarehe 24 Juni 2015
yaani siku 124 baada ya Notisi ya Baraza, kuna vyuo ambavyo havijachukua hatua
yoyote ya kurekebisha mapungufu yake.
“Baraza
limeamua kuchukua hatua kwa mujibu wa Sheria na Kanuni zake kwa taasisi na vyuo
vyote vilivyoorodheshwa kwa makosa yafuatayo, moja kumalizika kwa muda wa
Usajili wa Awali (Preparatory Registration) na Usajili wa Muda
(Provisional Registration); pili kutoanza mchakato wa kupata Ithibati baada ya
kupata Usajili Kamili; tatu kumalizika kwa muda wa Ithibati na kutochukuliwa
hatua ya kuomba upya Ithibati (re-affirmation); na nne taasisi na Vyuo kuamua
vyenyewe kusitisha kutoa mafunzo kwa sababu mbali mbali,” alifafanua
Vyuo vilivyofutiwa
usajili ni pamoja na Dar es Salaam College of Clinical Medicine cha jijini Dar
es Salaam kilichokuwa kimepatiwa usajili wa awali, Ndatele School of Medical
Laboratory Sciences cha Dar-es-Salaam kilichokuwa kimepatiwa usajili wa awali
na Institute for Information Technology
cha jijini Dar es Salaam pia
chenye namba za usajili REG/EOS/014.
Taassi/vyuo vilivyoshushwa
hadhi baada ya kushindwa kutiza mashart
ni pamoja na Sura Technologies – Dar es Salaam, Institute of
Management and Information Technology – Dar es Salaam, Techno Brain - Dar es
Salaam, Ministry of Agriculture Training Institute Igurusi – Mbeya, Mbozi
School of Nursing – Mbeya, KCMC AMO Ophthalmology School – Moshi, KCMC AMO
Anaesthesia School – Moshi, Advanced Pediatrics Nursing KCMC – Moshi.
Vingine ni, AMO Training Centre Tanga – Tanga, CATC
– Songea, CATC – Sumbawanga, COTC Maswa – Shinyanga, COTC – Musoma, Dental
Therapists Training Centre – Tanga, Ngudu School of Environmental Health
Sciences – Kwimba na KCMC AMO General School – Moshi.
Kuhusu NACTE
Baraza la Taifa la Elimu
ya Ufundi (NACTE) ni chombo kilichoanzishwa kwa Sheria ya Bunge Sura ya 129,
kwa lengo la kusimamia na kuratibu taaluma zinazotolewa na taasisi na vyuo vva
elimu ya ufundi nchini, ambavyo siyo vyuo vikuu au vyuo vikuu vishiriki. Jukumu
kubwa la Baraza ni kuendeleza na kuinua ubora wa elimu ya ufundi nchini kwa
kusimamia kikamilifu shughuli za kuendesha mafunzo ili tuzo zinazotolewa na
taasisi na vyuo ziwe na ubora unaokubalika kitaifa na kimataifa.
Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la
Taifa la Elimu ya ufundi(NACTE)Dkt. Adolf Rutayuga(katikati)akifafanua jambo
kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam(hawapo pichani)wakati wa kutangaza
ubora wa elimu ya ufundi inayotolewa na baraza hilo.Baraza hilo limevifuta usajili
vyuo vitatu na kuvishusha hadhi vyuo
kumi na sita.Kushoto ni Mkurugenzi wa Mitaala wa baraza hilo Twilumba Mponzi na
Msaidizi wa katibu Mtendaji Alex Nkondola.
Wakurugenzi wa Manejimenti ya NACTE wakiwa kwenye mkutano pamoja na
waandishi wa habari uliohusu kutangaza ubora wa Elimu ya ufundi
inayotolewa na baraza hilo lilitangaza kuvifutia usajili vyuo vitatu na
kuvishusha hadhi vyuo kumi na sita.
Mwandishi wa habari kutoka kituo
cha EAT, Noah Laltaila akimuuliza swali Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la
Taifa la Elimu ya ufundi(NACTE)Dkt. Adolf Rutayuga kwenye mkutano uliohusu kutangaza ubora wa Elimu ya ufundi
inayotolewa na baraza hilo lilitangaza kuvifutia usajili vyuo vitatu na kuvishusha hadhi vyuo kumi na sita.
Baadhi ya waandishi wa habari jijini
Dar es Salaam, wakiwa kwenye mkutano wa Baraza la Taifa la Elimu
ya ufundi(NACTE) uliohusu kutangaza ubora wa elimu unaotolewa na baraza
hilo.Baraza hilo limevifuta usajili vyuo vitatu na kuvishusha hadhi vyuo kumi na sita.
No comments:
Post a Comment