Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Mwantum Mahiza akifungua Mkutano wa wanajamii kuhusiana na Uundwaji wa mkakati wa mawasiliano wa kitaifa wa sekta ya Mafuta na Gesi Nchini, Mkutano ambao umewakusanya wadau mbalimbali wa mikoa ya Lindi na Mtwara, Mkutano huo unafanyika Mkoani Mtwara hivi leo.
Mkuu wa Wilaya Ya Mtwara,Fatuma Mafunda akikaribisha wageni waliohudhuria katika mkutano wa Wanajamii ulioandaliwa na Wizara ya Nishati na Madini ili kupata maonina kujadili Mpango mkakati wa sekta ya Gesi na Mafuta.
Wadau mbalimbali pamoja naKamati za Ulinzi na Usalama Lindi na Mtwara wakifuatilia kwa makini Mjadala unaoendelea hapa Mkoani Mtwara kujusiana na Majadiliano na matarajio ya Sekta ya Mafuta na Gesi, katika uundwaji wa Mkakati wa mawasiliano. Mkutano uliohusisha wanajamii.
Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mwantum Mahiza akiwa sambamba na Mkuu wa wilaya ya Lindi Ndg Yahaya E. Nawanda pamoja na Afisa Uhusiano wa Wizara ya Nishati na Madini, Badra Masoud wakiwa katika Mkutano wa wanajamii kuhusiana na Uundwaji wa mkakati wa mawasiliano wa kitaifa wa sekta ya Mafuta na Gesi Nchini, Mkutano ambao umewakusanya wadau mbalimbali wa mikoa ya Lindi na Mtwara, Mkutano huo unafanyika Mkoani.
Baadhi ya wadau wakiwa katika mkutano huo wa Uundwaji wa Mkakati wa Mawasiliano wa Kitaifa wa Sekta ya Mafuta na Gesi Unaofanyika Mkoani Mtwara leo Tarehe 9/6/2015.Picha na Abdulaziz Video,Mtwara
No comments:
Post a Comment